SIWEZI KUZINI MPAKA YESU ANARUDI
✍️Kwanza kabisa ukiona unaona haya kutamka maneno haya, ujue hiyo dhambi imeanza kukutafuna
Haya Ni Baadhi ya Mambo Yaliyo Nipa Uhakika Kuwa Inawezekana Kuishinda Zinaa na Matendo yake Jumla Kabisa
1.NILIGUNDUA KUWA NINAYE ROHO WA MUNGU NDANI YANGU
Huyu anajitambulisha Kama Roho Mtakatifu, Yani hakuna Namna Yoyote ile Nikaweza Kuwa nae alafu Nikaendelea Kukaa kwenye Uchafu au Zinaa.
Nilipata Uhakika siku Nilipo jiuliza Je Mungu anaweza Kuzini? NIkapata majibu kuwa hawezi Kuzini na akaniaminisha kuwa kwa Kukuwa Anaishi Ndani Yangu Basi Hatuwezi Kuzini maana si Mimi bali Kristo Ndani Yangu,
Warumi 8:11
[11]Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.
2.NILIGUNDUA KUWA HAKUNA DHAMBI YA BAHATI MBAYA, ZINAA NI JAMBO LA MCHAKATO NA LINA HATUA ZAKE KABISA
Hakuna Dhambi inayotokea kama Tukio tu mara Moja, Dhambi huwa inamchakato wake na Ndivyo Ilivyo zinaa, Mfano
- Huwa Kuna Mazungumzo,
- Haiishii hapa Kuna Kuanza Kuitana Majina Yasiyo faa yanayo anza Kuamsha Hisia za Mtu,
- Baada ya Hapa huwa Kuna Kupanga venue, Yani watu wanaamua Kuchagua eneo gani watakalo enda Kuzini,
- Na Mungu alivyo Mwema hata kama Mtu hajaokoka huwa kuna ile internal Motive ambayo Itakukumbusha kuwa huko unako enda Kuna jambo baya Linaenda Kutokea,
- Baada ya Venue kuna Kuanza Kushikana na Hapa bado Unakuta kuna mtu mmoja hashituki (anajipa Moyo kuwa itaishia hapo tuu)
- Hatimaye Mnakamilisha Zinaa kwa asilimia zote
- Je Huu Mchakato ni Ghafra au Ulijua Nini Kitatokea?
Yakobo 1:14-15
[14]Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.
[15]Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.
Baada ya Kugundua Kuwa Zinaa ni Jambo la Mchakato, Niliapa Kuwa Mtu wa Mipaka na Nidhamu ya Hali ya Juu Kuanzia Kwangu (Sirini) hadi kwa watu wa Jinsia Tofauti ,
1 Yohana 5:18
[18]Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hamgusi.
3.NILIAMUA KUTAFUTA KUUJUA UKWELI NA UHALISIA WOTE KUHUSU ZINAA
Usipo Ujua Uhalisa wa zinaa Utaendela Kuitenda Siku kwa Siku.
Kwa Muonekano wa Nje zinaa Imepewa Majina Mazuri mfano PENZI, MAHABA, PUMZIKO, OUTING, REFRESHMENT, ENJOYMENT N.K
ILA KATIKA UHALISA WAKE
- Zinaa ni Ubaya Mkubwa
- Zinaa ni Shimo linalozika Hatima
- Zinaa Inaua Kesho Bora
- Zinaa ni Mlango wa Kuzimu
- Zinaa ni Mkataba wa Kumkosa Mungu
- Zinaa ni Mauti
Mithali 7:17-18,21-22
[17]Nimetia kitanda changu manukato,
Manemane na udi na mdalasini.
[18]Haya, na tushibe upendo hata asubuhi,
Tujifurahishe nafsi zetu kwa mahaba.
[21]Kwa maneno yake mengi na ulaini akamshawishi,Kwa ubembelezi wa midomo yake akamshinda.
[22]Huyo akafuatana naye mara hiyo,
Kama vile ng’ombe aendavyo machinjoni;
Au mpumbavu kuadhibiwa katika pingu;
Mwanzo 39:9
[9]Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje UBAYA huu mkubwa nikamkose Mungu?
4.NILIFAHAMU KUWA AKILI NA UWEZO WA KIUNGU WA KUWEZA KUISHINDA DHAMBI NA ZINAA UNALETWA KWA KUAMUA KUJAA NENO LA MUNGU KWA WINGI NDANI YANGU
Kupima Kiwango chako cha akili jipime Kwa haya Mambo Mawili,
- Kwa Kiasi gani Neno limejaa Ndani Yako,
- Namna ulivyo weza Kulitumia Neno Kuishinda zinaa Jumla (Kuliingiza Neno kwenye Utendaji),
Zinaa Haijawai Kumshinda Mtu mwenye akili ya Kiungu, Kama Hupendi kuitwa Mjinga amua Kuikataa Zinaa Kwa Kulijaza Neno la Mungu Ndani Yako na Kuanza Kulitumia Mpaka Likupe Ushindi Jumla.
Mithali 7:7
[7]Nikaona katikati ya wajinga,Nikamtambua miongoni mwa vijana, Kijana mmoja asiyekuwa na akili,
(Mithali 7:7-27)
Mithali 6:32-33
[32]Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa;Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.
[33]Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima;
Wala fedheha yake haitafutika.
Wakolosai 3:16 A
[16]Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote,
Zaburi 119:11
[11]Moyoni mwangu nimeliweka neno lako,
Nisije nikakutenda dhambi.
5.NILIFAHAMU KUWA MAONO NI YA MUHIMU SANA KWANGU NA YATANISAIDIA KUILINDA LEO YANGU KATIKA SAFARI YA KUIENDEA KESHO BORA.
Zinaa Huwezi kuitenganisha na Mtu asiye na Maono, Mtu wa Jumla Jumla, Mtu wa Kwenda Kila Mahali, Mtu wa Kufanya anacho Jiamlia Kufanya, Mtu wa Mikumbo Mikumbo (Gen-z wanasema Vibes)
Bali Ushindi dhidi ya Dhambi zote na zinaa Unahitaji Mtu Mwenye Maono ya Wapi anaenda, Mtu wa Nidhamu Nyingi,
Mtu aliye amua Kuambatana na watu wenye taswira sawa za Kesho zao zenye Utukufu Mwingi.
Ukitaka Kujua Maono ni Ya Muhimu Sana Kasome habari za Daudi, Nikweli aliweka Historia ya kumwangusha Goliathi lakini Kosa la Kukosa Maono Likamfanya aweke historia Nyingine Mbaya ya kuanguka Kwenye Zinaa
(2 Samwel 11:1-4)
Mithali 7:7-12
[7]Nikaona katikati ya wajinga, Nikamtambua miongoni mwa vijana, Kijana mmoja asiyekuwa na akili,
[8]Akipita njiani karibu na pembe yake,
Akiishika njia iendayo nyumbani kwake,
[9]Wakati wa magharibi, wakati wa jioni,
Usiku wa manane, gizani.
[10]Na tazama, mwanamke akamkuta,
Ana mavazi ya kikahaba, mwerevu wa moyo;
[11]Ana kelele, na ukaidi;
Miguu yake haikai nyumbani mwake.
[12]Mara yu katika njia kuu, mara viwanjani, Naye huotea kwenye pembe za kila njia.
Mithali 29:18
[18]Pasipo maono, watu huacha kujizuia;
Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.
🩸Kama umewahi kuzini na umeshatubu na kurudi mbele za Mungu hakikisha uanvunja mkataba wa kiroho uliokuwa umefanyika kupita lile tendo
HIVYO BASI
"Kwa akiri zangu timamu na Aliyeko Ndani Yangu Bila Kushurutishwa na Yeyote Tunakiri Kuwa Hatuwezi Kuzini Mpaka Yesu anarudi."
✍️Kwa msaada na ushauri 0757801321 (Normal & WhatsApp)
"UNAWEZA KUAMUA KUTOZINI PIA MPAKA YESU ANARUDI"
#MwinjilistiElishaMusa
#UtukufuMkubwaUmekujia
#WeweNiUshuhudaUnaotembea