Electrical engineers nisaidieni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Electrical engineers nisaidieni

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by MIGNON, Oct 22, 2011.

 1. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2011
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,587
  Likes Received: 1,563
  Trophy Points: 280
  Naombeni msaada.

  Nina motor ya 20HP ambayo nimeifunga katika kinu cha kusaga lakini motor hii imenisumbua sana. Kwanza nilikuwa natumia star delta starter lakini consumption ya umeme ikawa kubwa mno.

  Nika consult mafundi na baada za kufunga amper meter tukagundua ya kuwa hakuna tofauti kati ya starting na running current,iko juu all the time. Fundi akaifungua na akadai ya kuwa kuna sehemu inagusa case na akasugua na msasa lakini baada za kuifunga ngoma ikawa hivyo hivyo.

  Next day fundi akadai kuwa inawezekana ilikosewa kiwandani na akaifunga star na consumption ya umeme ikad drop mno,inaanza na 33 ampere na bila load inashuka mpaka 7 ampere.

  Nilifurahi kuwa problem imekuwa solved lakini cha ajabu ni kuwa inapata moto mpaka unga ukiangukia juu yake inatoa moshi.Kwa uzoefu wangu joto inalopata ingekuwa motor ingine ingeungua lakini si kwa hii.

  Tumekagua kuwa labda kuna lose connection lakini hatukuona na pia tu mecheck earthing system na kwa utaalamu wa mafundi wangu wanasema ni nzuri. Kwa kuwa nafanya biashara mapato per unit consumed ndio kigezo changu kikibwa na muda wote huu kipato kipo chini.
  Nisaidieni wataalamu.
   
 2. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2011
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,587
  Likes Received: 1,563
  Trophy Points: 280
  Yaani wahandisi wote wanaishia kwenye siasa na habari mchanganyiko.Yaani mpaka saa hizi hakuna engineer alizepita hapa?
   
 3. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  hahahaha

  Si unaona hata kwenye siasa ndipo walipo ma engeeer. Na hata bungeni wapo wengi wanatunga sheria.

  Mimi si mtaaalama wa haya mambo laini kwa uwa wewe ni mtaalama najua uitumia maneo sahihi gogle utapata jibu naunaweza kuja kutupa somo hapa

  Mfano nime google nikakutana na hii white paper Choice f elecrtical motor avoid overheating  Kwenye hii article nimeona kihindi hindi laini kwenye
  Subheading ya PWM and motor Heating wewe unayju zaidi mmbo haya labda kuna jambo laweza kukupa jibu.   
 4. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2011
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,587
  Likes Received: 1,563
  Trophy Points: 280
  MTAZAMAJI niliogopa kusema wanaishia kweye "mahusiano na Mapenzi" hata hivzo nashukuru kwa ushauri wako.
  Nimeipitia website ulyoshauri na wameeleza vizuri ingawa reference zao ni motor za HP kubwa sana.
  Nilipenda sana ku solve hii problem kupitia watu walio na uzoefu zaidi kuliko theories kwani hata wiring zetu tunazofanyiwa si za kiwango.
   
 5. N

  Nkwama welding Member

  #5
  Oct 24, 2011
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa kukusaidia jaribu huyu expert ni electrical technician alistaafu urafiki textile miaka ya karibuni sasa hivi anafanya kazi za kujiajiri.anazijua mota kama kiganja chake namba yake ya simu ni 0756177615. anaitwa Hokororo.
   
 6. P

  Percival JF-Expert Member

  #6
  Oct 24, 2011
  Joined: Mar 23, 2010
  Messages: 2,567
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  Mie sio Electrician lakini ninajua kodogo kuhusu umeme.
  1. Angalia Fan la motor kama linafanya kazi vizuri na linasukuma upepo sawasawa
  2. Angalia motor Fins - mifereji au matuta yalyoko juu ya motor kama yamejaa unga au uchafu. hii inaweza kuzuia upepo kuipoza motor vizuri.
  3. Inawekekana kinu chako ni kikubwa kuliko uwezo wa motor yako. Angalia amperes unaposaga kama hizi zipo chini ya kiwango zinazo ruhusiwa na motor.
  4. Ondoa mikanda na uishughulihe motor , angalia ampere zinazotumika ikiwa ni kubwa basi tatizo ni kwenye motor, pia iache kwa muda ishughulike bila mikanda na angalia kama inapata moto au la.
  5. Tafuta mtaalam afanye winding resistance check.

  Basi ni hayo tu nimefikiria - lakini unavyosema hilo joto mpaka linachoma unga ukianguka juu yake - nini mashaka kama itadumu muda - sababu winding zitaharibika baada ya muda.
   
 7. m

  mchakato Member

  #7
  Oct 25, 2011
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 45
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  nipe kazi rasmi ifanyike.
   
 8. m

  mchakato Member

  #8
  Nov 13, 2014
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 45
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Upo wapi ninye kumaliza tatizo?
   
 9. MKANDAHARI

  MKANDAHARI JF-Expert Member

  #9
  Nov 17, 2014
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 1,017
  Likes Received: 700
  Trophy Points: 280
  The load is too heavy for the mator, check the motor ratings and either install the bigger motor or reduce the driven loads!
   
 10. alphonce.NET

  alphonce.NET JF-Expert Member

  #10
  Nov 20, 2014
  Joined: Jul 19, 2013
  Messages: 615
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 45
  Kama kazi inayofanya ni kuendesha kinu cha kusaga ni lazima iwe delta ili iweze kufanya kazi sawa sawa.

  Star inaokoa umeme lakini motor haiwezi kutengeneza enough uotput power, matokeo ndio hayo ukiwa under load lazima utapata over heat

  Hapo kwenye delta ambapo tatizo ni over consumption, kuna mambo ya kuangalia ambayo ni

  1. Hakikisha unatumia contactors nzuri (best quality) na ziwe 60A

  2. Hakikisha phase zako zote ziko na kiwango sawa cha voltage (kama kutakua na phase ina under voltage inabidi ushughulikie hili kwanza. Pima individual phases na neutral sio phase na phase)

  3. Hakikisha motor cooling fan inafanya kazi sawa sawa

  4. Hakikisha power cable zako zote tokea kwenye circuit breaker ni 16mm

  Hayo yakiwa sawa kwa vyovyote tatizo lako litaisha


   
 11. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #11
  Nov 20, 2014
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,587
  Likes Received: 1,563
  Trophy Points: 280
  Nakushukuru sana ingawa tayari niilsha solve hiyo problem palikuwa na lose connection somwhere.
  Thanks a lot,usicheze mbali na JF
   
Loading...