Electoral votes na namna rais wa Marekani anavyopatikana

Electoral votes na namna rais wa Marekani anavyopatikana

Iceman 3D

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2016
Posts
20,611
Reaction score
67,118
Kumekuwa kuna maswali mengi, kwa nini Trump amepitwa kwa kura lakini kashinda Uraisi? Nataka nitolee maelezo ili tupate kujua kama ifuatavyo, japo maelezo yatakuwa mengi kidogo.

Rais wa Marekani hupatikana kutokana na wingi wa 'electoral votes' ambazo ni kura maalum zinazo wakilisha maamuzi ya jumla ya watu wa majimbo mbali mbali ya marekani. Na hili ni jambo la kikatiba na kundi la wapiga kura za electoral votes huitwa electoral college

Kwanini electoral college?
Marekani ni muunganiko wa majimbo {federal state) na si jamuhuri ya watu wa marekani kama ilivo TZ (republic) hivo, rais lazima ashinde uwakilishi mwingi wa majimbo na si idadi ya watu.
Pia waanzilishi wa taifa la marekani waliona majimbo makubwa yata wanyanyasa majimbo madogo, kwani kama mfumo wa wengi wape ukitumika mwenye jimbo dogo ndio asingesikilizwa kila maamuzi yanapo fanyika yakiwemo ya uchaguzi

Idadi ya electoral votes
Zipo 538 amabzo zina wakilisha idadi ya viti vya majimbo yote kwenye baraza la wawakilishi (435) na seneti (100) pia kwa sababu washington si jimbo ila ni wilaya maalum yenyewe inapata nafasi (3) za upendeleo hapo unapata jumla ya 538. Ili uwe rais wa Marekani lazima ufikishe electoral votes kuanzia 270 ambayo ni zaidi ya nusu ya electoral college yote.
Majimbo mengi mshindi huchukua electoral votes zote, kasoro Maine na Nebraska ambapo mshindi na mshindwa hugawana electoral votes ikiwa mshindwa kashinda kwenye congresional district pia.

Electors ni kina nani?
Kwa kuwa katiba ya marekani hairuhusu wawakilishi au maseneta kupiga kura kama electors, kila jimbo huwa na utaratibu wake wa kupata watu watakao kwenda kupiga kura rasmi katika electoral college, ambao wengi hutokana na chama kilicho shinda kwenye jimbo hilo, pia wengi huwa hawajulikani kwani ni hatari kwa usalama wao na ili kuepuka vishawishi mbali mbali siku ya kuchagua yenyewe. Tukio la kupiga kura rasmi hufanyika siku tofauti na uchaguzi wa wananchi, mfano mwaka huu kura rasmi za electoral college zitapigwa disemba 19, na hapo ndio trump atathibitshwa rasmi kama rais mteule. Electors wanaweza kubadili mawazo kwa kuchagua mgombea ambaye jimbo lake halikumchagua. Kwa hiyo hata Rais mteule Trump bado hajapita rasmi kwani electoral college inaweza kuwageuka wana nchi wao hiyo tarehe 19 ya mwezi ujao. lakini hii huwa ngumu sana kwani majimbo mengi yana viapo vikali ili kuhakikisha hubadilishi kura yao kwa hiyo tuna tegemea apite

Kama wagombea wote hawata fikisha electoral votes270
Uchaguzi hupelekwa kwa baraza la wawikilishi ambao huchagua rais kwa niaba ya majimbo yao, lakini huchagua wanavo taka, hivo hii huwa faida kwa chama kilicho na wabunge wengi.

Faida na hasara za electoral college
Faida zake ni kuwa majimbo makubwa pekee ni ngumu kuamua mshindi, mfano county ya Los Angeles peke ina watu milioni 8.2, hii ni sehemu tu ya jimbo la California, lakini jimbo zima la idaho lina watu milioni 1 hivo inawezekana hata wakat wa kampeni wagombea wakapiga kambi LA na wasikanyage Idaho hivyo jimbo zima la Idaho kupoteza umuhimu katika maamuzi makubwa ya nchi. Pia mara nyingi watu walioko mijini ambao kwa kawaida huwa wengi si rahisi kuwa control watu walioko vijijini kwani huwa wachache, mfano uchaguzi huu watu wa vijijini ndio wame mpitsha Trump kwa wingi kuwa rais, faida nyingine ni kwa kuwa marekani huwa na wagombea wawili tu wenye nguvu hivo kila jimbo huwa na umuhimu kwani kila electoral vote huwa ina changia kushinda mfano clinton kashindwa Wisconsin kwa sababu hakwenda kupiga kampeni akidhani atashinda kwani ni jimbo linalopendelea kuchagua democrat hivo kapoteza electoral votes 10 zilizo enda kwa Rais mteule Trump

Hasara
Mfumo huu hata wamarekani wenyewe wengine hawaujui ndio maana unaona kelele nyingi, askudanganye mtu kwa kuwa yuko USA wengi hawaujui na kwa kuwa hutokea mara chache mambo yakawa kama ya Rais mteule Trump basi wanakasirika halafu wanasahau na kupuuzia.
Pia kwa kuwa kuna majimbo ambayo siku zote yamekuwa yaki jihusianisha na vyama, mengine huwa democrat mengine huwa republican, wagombea hutumia muda wao mwingi kuwepo kwenye majimbo ambayo hubadilika badilika kama vile Ohio na Florida.
Hasara nyingine mtaongeza wenyewe.

Mwisho
Ni mara chache sana hutokea hali kama hii ambapo mshindi wa jumla aka shindwa kuwa raisi na imetokea mwaka 1824, 1876, 1888, 2000, na 2016.
Hivo kura za wamerekani zina umuhimu katika kuamua electoral vote ya jimbo la mpiga kura iende kwa nani, pia ina ondoa uwezekano wa watu wengi wa sehemu moja kuwa amulia watu wa maeneo mbali mbali, mfano rais mteule Ttrump kashinda majimbo karibu 30 kati ya 50 hivo majimbo mengi yana mtaka yeye.

*Karibuni kwa masahihisho au nyongeza
 
Umeeleza vizuri mkuu.

Ila kwa kuongezea ni kwamba mfumo wa upigaji kura wa Marekani unachanganya sana.

Inawabidi wamarekani waamue waachane na huo mtindo wa "electoral college" ambao si demokrasia bali ni disaster tu ingawa hata Trump mwenyewe hakutegemea kushinda.

Kwa sababu mgombea anaposhinda kura za umaarufu au "popular vote" kwenye jimbo moja, basi anachukua ushindi wa "electoral votes" zote kwenye hilo jimbo.

Na pia hata mgombea akipata kura moja ya "popular vote" basi anashinda kura zote za "electoral votes" jimboni humo!

Hivyo hiyo inamaanisha kwamba Donald Trump alishinda katika majimbo mengi lakini kwa kura chache yaani "narrow majority".

Na hivi ndivyo alivyoweza kushinda uchaguzi huo dhidi ya Hillary Clinton ambae alitegemewa kushinda kwa kura nyingi kumzidi Donald Trump.

Ni mara chache sana hali hii kutokea na katika uchaguzi wa Marekani mpaka sasa hali hiyo imetokea mara nne kama ulivyosema:

  • Al Gore, alishindwa na George W Bush mwaka 2000 kwa kura tano ingawa alishinda ile popular vote.
  • Grover Cleveland, ambae alishindwa na Benjamin Harrison mwaka 1888
  • Samuel Tilden, ambae alishindwa na Rutherford B. Hayes mwaka 1876
  • Andrew Jackson, ambae alishindwa na John Quincy Adams mwaka 1824
Haya mambo yapo kwenye rekodi na huwa ni dhahiri.
 
Ahsante nimekusoma Richard electoral votes si dizaster ila ndio mapungufi yake kwani katika marais 45 ni wa 5 tu wamekosa electoral votes
Tena ukiangalia Trump kapitwa hizo kura laki 2 lakini ameongoza kwa electoral zaid ya 300, bado majimbo memgi sana yame mkubali

Ukiondoa kura za California ambako ndio clinton kashindia hiyo popular vote , unakuta Trump ana ongoza kwa zaid ya kura milion 1, ukiondoa Oregon pia ambako Clonton kashinda asilimia 73 Trump ana bakiwa na mamilioni ya kura hivo Blame HRC na si electoral college, mama alifanya kampeni hovyo

Pia state ndogo kama idaho, dakotas na wyoming hazita kubali kutoa huo mfumo kwani zitakandamizwa hadi zikome

Wazo la kuondoa ni zuri ila kwa sasa sidhani kama lita tekelezwa
 
Certainly, there's no gainsaying the fact that the electoral college system is seriously flawed! The system represents a subtle departure from the doctrine of one man, one vote, because an electoral vote is like a loaded (biased) dice.

However, it protects citizens residing in certain areas of the country from being treated as completely irrelevant! Also, since all participants in the presidential race fully understand the rule of the game, they ought to craft a game plan that mitigates the flaws of the system or else they run a risk of paying a heavy price!
 
Ahsante nimekusoma Richard electoral votes si dizaster ila ndio mapungufi yake kwani katika marais 45 ni wa 5 tu wamekosa electoral votes
Tena ukiangalia Trump kapitwa hizo kura laki 2 lakini ameongoza kwa electoral zaid ya 300, bado majimbo memgi sana yame mkubali

Ukiondoa kura za California ambako ndio clinton kashindia hiyo popular vote , unakuta Trump ana ongoza kwa zaid ya kura milion 1, ukiondoa Oregon pia ambako Clonton kashinda asilimia 73 Trump ana bakiwa na mamilioni ya kura hivo Blame HRC na si electoral college, mama alifanya kampeni hovyo

Pia state ndogo kama idaho, dakotas na wyoming hazita kubali kutoa huo mfumo kwani zitakandamizwa hadi zikome

Wazo la kuondoa ni zuri ila kwa sasa sidhani kama lita tekelezwa
Hivi Hii Mnayoita Electoral Vote, inalindaje hizo Federal States? Maana ndio zinazosababisha Popular Votes zisitumike
 
Umesema tarehe 19/12/2016 wanaenda kupiga electrol votes,je hizi 278 alizopata Trump zilikuwa ni nini?
Alicho pata juzi Trump ni alocation ya electoral colleges, ndio maana mpaka sasa hivi matokeo ya jumla hayaja tangazwa, zile kura zimeonesha kuwa siku ya kura rasmi, mpaka sasa majimbo yame amua Trump apewe Electoral votes 306, Clinton 222 hivo siku ya kura rasmi tuna tegemea wapewe hivo.

Lakini katiba iliwapa uhuru electors ili kama mgombea ambaye watu walimchagua ana dalili zote za kuto faa kuwa rais(mfano amethibitika ni kichaa), wao wabadilishe matokeo kwa ajili ya maslahi mapana ya taifa.
 
Alicho pata juzi Trump ni alocation ya electoral colleges, ndio maana mpaka sasa hivi matokeo ya jumla hayaja tangazwa, zile kura zimeonesha kuwa siku ya kura rasmi, mpaka sasa majimbo yame amua Trump apewe Electoral votes 301, Clinton 222 hivo siku ya kura rasmi tuna tegemea wapewe hivo.

Asante,je ishawahi kutokea huko nyuma rais mteuliwa kutokuchaguliwa katika electral votes?
 
Hivi Hii Mnayoita Electoral Vote, inalindaje hizo Federal States? Maana ndio zinazosababisha Popular Votes zisitumike
Electoral college ina linda federal state kwani ina uhakika wa kumpa mshindi wa state nyingi urais at least kwa asilimia 95%
Hivo wagombea wanalazimika kufanya kampeni kila sehemu ya nchi na kusikiliza watu wana semaje, na hata rais kuna kuwa na uhakika wa kila state kufaidika na urais wake kwani alipitishwa na maeneo mengi.
Kama kungekuwa hakuna electoral colleges, wagombea wangekuwa wana piga kambi majimbo makubwa12 tu kati ya hamsini, hivi hayo majimbo 38 wagombea wengi wasinge yavalia njuga wala kuya shughulikia kama wakipita.

Hivi vi electoral votes ndio vina wapa uthamani wakati wa kuchagua na kutoa services.
 
Alicho pata juzi Trump ni alocation ya electoral colleges, ndio maana mpaka sasa hivi matokeo ya jumla hayaja tangazwa, zile kura zimeonesha kuwa siku ya kura rasmi, mpaka sasa majimbo yame amua Trump apewe Electoral votes 301, Clinton 222 hivo siku ya kura rasmi tuna tegemea wapewe hivo.

Lakini katiba iliwapa uhuru electors ili kama mgombea ambaye watu walimchagua ana dalili zote za kuto faa kuwa rais(mfano amethibitika ni kichaa), wao wabadilishe matokeo kwa ajili ya maslahi mapana ya taifa.

SWALI.
Kama tarehe 19 Dec watakaopiga kura wakimpa Clinton Electoral Vote nyingi zaidi ya Trump ina maana Clinton ndio atakuwa Rais wa Marekani au Uchaguzi utarudiwa upya au utaratibu gani utafuata?
 
Electoral college ina linda federal state kwani ina uhakika wa kumpa mshindi wa state nyingi urais at least kwa asilimia 95%
Hivo wagombea wanalazimika kufanya kampeni kila sehemu ya nchi na kusikiliza watu wana semaje, na hata rais kuna kuwa na uhakika wa kila state kufaidika na urais wake kwani alipitishwa na maeneo mengi.
Kama kungekuwa hakuna electoral colleges, wagombea wangekuwa wana piga kambi majimbo makubwa12 tu kati ya hamsini, hivi hayo majimbo 38 wagombea wengi wasinge yavalia njuga wala kuya shughulikia kama wakipita.

Hivi vi electoral votes ndio vina wapa uthamani wakati wa kuchagua na kutoa services.
[emoji122][emoji122]

Kwa hiyo December 19 Bado Uchaguz unaendelea?
 
Asante,je ishawahi kutokea huko nyuma rais mteuliwa kutokuchaguliwa katika electral votes?
Ndio alikuwepo John q Adams
Huyu hakushinda electoral college wala kura za jumla
Kwa kuwa wagombea wote hawakufikisha 270, ilibidi uchaguzi uende congress na ndipo congress ilipo mpa urais.
Huyu alishndwa kwenye kila category lakini alipata urais
Mwaka 1824
 
SWALI.
Kama tarehe 19 Dec watakaopiga kura wakimpa Clinton Electoral Vote nyingi zaidi ya Trump ina maana Clinton ndio atakuwa Rais wa Marekani au Uchaguzi utarudiwa upya au utaratibu gani utafuata?
Electors wasipo mpa Trump kura, ita angalia kama Clinton atapewa kura zika fika 270,atakuwa ndiye rais
Lakini ikitokea electors wengi waka haribu kura basi clinton asifikishe 270 wala Trump asifikishe 270 uchaguzi utapelekwa kwenye baraza la wawakilishi ambao hao wata mchagua rais.
 
[emoji122][emoji122]

Kwa hiyo December 19 Bado Uchaguz unaendelea?
Yes uchaguzi hauja isha lakini bado Trump ata shinda tu kwani
Sikuhiyo ni kama ceremonial tu, uchaguzi ni sawa na kutoa mahali halafu siku hiyo ni ya ndoa, wazazi ni vigumu kukupa mdogo wake wa bibi harusi, unless kuna sababu kubwa sana.

Na trump ana kadiriwa kuwa ata fikisha electoral votes 306, ni ngumu watu 37 waka mtosa ili waende kwa Clinton.
Pia clinton mwenyewe kasha kubali kushindwa hadharani hivo ni ngumu kusema arudi tena a revoke.
Inawezekana lakin chance ni ndogo sana. So Trump will likely remain the president
 
Electors wasipo mpa Trump kura, ita angalia kama Clintin atapewa kura zika fika 270,atakuwa ndiye rais
Lakini ikitokea electors wengi waka haribu kura basi clinton asifikishe 270 wala Trump asifikishe 270 uchaguzi utapelekwa kwenye baraza la wawakilishi ambao hao wata mchagua rais.

Safi sana kwa jibu.
Nafikiri ni wakati wa wale waandamanaji kumpigia kampeni Bi.Clinton kwa hao Electors.
By the way,Hao Electors wanachaguliwaje? Na uhakika kwamba hawatamsaliti Trump ukoje kwa majimbo ambayo kashinda?
 
Ni kweli uko sahihi, maandamano yana lengo ya kuwachanganya electors wa flip kura zao, hayata fanikiwa kwani sehemu nyingi alizo shinda Trump watu wamechill tuu. Maandamano yapo maeneno ya California, oregon, new York, vermont na baadhi ya sehem za Florida ambazo Trump hakuwa na influence.

Electors wengi hupelekwa na chama kilicho shinda kwnye jimbo hilo, hivo Repubkican watakuwa na electros 306 na democrats watakuwa na hao waliobaki, kuna majimbo huwataja electors wake ila mengi haya wataji, kwa kuwa Republicans wote washa mkubali Trump ni shda sana wao kutoka na kusema hawamtaki, pia state nyingi zimeweka sheria kali kwa elector atakaye flip kura, na hata wakisema wa flip watakuwa wana tafuta vita, na urais wa Clinton utakuwa mgumu kwani kwenye baraza la wawakilishi bado republicans ndio wengi na kwenye senet republicans ndio wengi, hivo electors wanahisiwa kuwa wata baki vile vile kwa Trump
 
Makofi Mengi Kwako Burroo,,[emoji122][emoji122]

Ila kuna kaswahi kaujinga wangu kuelewa hawa MaElectors,
Kwa hiyo kuna uchaguzi ambao hufanyika kabla ya mkuu ambao chama kinaposhinda kinampendekeza Elector wa college ambaye elector huyo anakuja kwenye uchaguzi mkuu na huo wa disemba au ikoje hapo,sorry kwa ujinga wang, nisaidie
 
Back
Top Bottom