nafikiri walikuwa wanafikiria kutunga sheria ya kuondoa rushwa kitu ambacho kwa masikitiko makubwa naweza kutangaza kuwa wameshindwa. Sheria hii inafungua mlango mpya kabisa wa matumizi ya rushwa katika chaguzi.
Ndugu Wananchi,
Sheria pia inaweka sharti la uwajibikaji wa vyama vya siasa, wagombea na washiriki wengine kuhusu michango, mapato na matumizi katika uchaguzi. Sheria inaelekeza kwamba:-
1. Kila mchango unaopokelewa na matumizi yatakayofanyika kwa ajili ya uchaguzi vifanywe na Chama na siyo vinginevyo.
2. Chama cha siasa kitawajibika kwa matumizi yote yatakayofanywa na chama au wagombea wake, na kwamba matumizi yote yanatakiwa kuwa na risiti.
3. Kila mgombea atawekewa mgawo wake wa matumizi ya kampeni na chama kitatoa taarifa ya fedha iliyokaguliwa kwa matumizi hayo.
4. Chama kitakachoshindwa kutunza taarifa hizo kitakuwa kimetenda kosa na kitastahili adhabu.
5. Kila mgombea atakayepokea mchango atapaswa kutoa taarifa kwa chama chake kuhusu mapato na matumizi yanayohusu mchango huo.
6. Kila chama cha siasa, taasisi ya kiraia, taasisi ya kidini au taasisi ya kijamii itakayohusika katika kuchangia shughuli za uchaguzi, inayo wajibu wa kutunza taarifa za fedha zinazoelezea mapato na matumizi yao....
Ndugu Wananchi;
Sheria imeainisha vizuri mambo yanavyokatazwa kwa upande wa matumizi ya fedha za uchaguzi. Sheria inakataza, kwa mfano, vitendo vifuatavyo visifanyike pamoja na matumizi ya fedha kwa ajili hiyo kuzuiliwa:
1. Kufanya malipo kwa wapiga kura ili wamchague mgombea fulani;
2. Kuahidi kazi au cheo au wadhifa kwa mpiga kura ili amchague mgombea;
3. Kutoa zawadi, ahadi, mkopo, au makubaliano yoyote kwa mpiga kura ili amchague mgombea;
4. Kukubali kurubuniwa kwa mambo yoyote yaliyotajwa hapo juu ili ampigie kura mgombea yeyote;
5. Kufanya vitendo vyovyote kati ya hivyo wakati wowote kabla au hata baada ya uteuzi wa mgombea;
6. Kutoa malipo kwa ajili ya takrima ya chakula, vinywaji au starehe yoyote kwa ajili ya kuwashawishi wapiga kura wamchague mgombea;
7. Kuwasafirisha wapiga kura ili wamchague mgombea. Hata hivyo Sheria inaruhusu wapiga kura wenyewe kujilipia nauli kwenda kupiga kura au Serikali kuwasafirisha wapiga kura pale ambapo kuna shida ya usafiri;
8. Kuweka mkataba wowote ule wa pango kwa niaba ya wapiga kura ili wamchague mgombea;
Mku Mwanakijiji,
Kama kweli hataki watu watoe ahadi basi hata Ilani ya uchaguzi ya CCM isiwepo...
naona anajichanga na maneno.
Unfortunately swali halijatulia, sheria imetungwa na bunge, Rais anafafanua.... sasa why do i have to agree or disagree with him?
Are we serious or we just trying to push our agenda for all means possible?
mwana kijiji plz toa zis picha bana vp lkn?
Kutoa zawadi, ahadi, mkopo, au makubaliano yoyote kwa mpiga kura ili amchague
sasa huu mtego.. nitoe picha ya shambani kwangu.. na mimi nikukuomba utoe kidole mdomoni?
Wapendwa,
Tunahitaji kuwa makini zaidi tukisoma mabadiko au sheria... haiwezekani unataka ubunge unaenda kumuahidi mtu mmoja... sheria imesema mpiga kura... "singular" kiswahili "mamoja".
Usually ahadi za mbunge ni kwa huduma zinazokumba jamii nzima sio mpiga kura mmoja. hivyo ingesema ahadi kwa wapiga kura that is different.
si uweke ile nyingine?mm kidole kikitoka mdomoni ntakiweka wapi bana?
2. Kuahidi kazi au cheo au wadhifa kwa mpiga kura ili amchague mgombea;
3. Kutoa zawadi, ahadi, mkopo, au makubaliano yoyote kwa mpiga kura ili amchague mgombea;
koh koh koh.. haya tuyaache. Naitafuta picha ya jembe sijui wajukuu wameiweka wapi. Mama nanino amenilalamikia hataki anione na picha ya shambani tena..
wrong. kwani kuna mtu anapiga kura zaidi ya moja. Wagombea hawaombi kura nyingi, wanaomba kura moja moja tu! ndio maana ya kusema "mpiga kura"..
Rais hajakosea wala sheria haina matatizo, matatizo mumesoma hayo maneno mkiwa na agenda zenu...
Someni tena vizuri mkiwa na open minded.
Hapa rais anazungumzia mbunge mtarajiwa kumuahid kasheshe cheo, etc. kosa wapi wandugu... mbona mnaturudisha nyumba?