EL CLASICO, Barcelona Vs R.Madrid; Live from Camp Nou, Barcelona

EL CLASICO, Barcelona Vs R.Madrid; Live from Camp Nou, Barcelona

Mourinho

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2012
Posts
4,619
Reaction score
2,328
Ukiwa ndio uwanja mkubwa zaidi wa soccer barani Ulaya, wenye uwezo wa kuchukua watu 99,354, leo hii kwenye majira ya saa 19:00 (EAT) uwanja wa Camp Nou utageuka uwanja wa mapambano kati ya mahasimu wakubwa wawili wa soccer katika sayari hii.

Barcelona wakiwa nyumbani watawakaribisha mahasimu wao wakubwa Real Madrid( the Galacticos) katika mtanange wa ligi kuu ya Spain, maarufu kwa jina la La Liga.

Ikumbukwe kuwa uhasimu wa club hizi mbili ni zaidi ya mpira tu, kuna masuala ya kisiasa na kiutamaduni yanayozigawa club hizi kubwa duniani, Barcelona kama alama ya wacatalunya wakati R.Madrid wakiwakilisha Spain.
Ndio maana slogan ya Barcelona inasema 'mēs que un club' ikiwa na tafsiri sisisi ya 'more than a club'/ zaidi ya club'

Mpambano huu utaleta tena mpambano mwingine mdogo ndani yake, Messi Vs CR7. Wachezaji nyota wa kila team, Messi akionekana kama mchezaji bora zaidi wa kizazi chake huku CR7 akibishana na hilo akijiaminisha yeye ndio mchezaji bora zaidi wa Dunia kwa sasa.

Mpaka sasa Messi kacheza mechi 7 kwenye ligi, kafunga goli 8, akitengeneza mengine matatu/3 na akiwa na shot accuracy ya 84%.
CR7 kacheza mechi 9, magoli 8, assist 1, na shooting accuracy yake ni 78%.

Wakati Messi kafunga magoli 8 baada ya kupiga mashuti 29, CR7 kapiga mashuti 57 na kufunga magoli 8 tu.

Mpaka sasa Messi ndiye mwenye magoli mengi katika mtanange huu, magoli 18, sawasawa na nguli wa Madrid di Stefano, na kama leo akiwa uwanjani utategemea aongeze idadi ya hayo magoli.

Katika mechi mbili za mwisho kuwakutanisha hawa mahasimu, Real Madrid waliibuka vinara wa mechi zote, wakiwafunga Barca umamani na ubabani.

Lakini kuna mambo yamebadilika, makocha wa team zote mbili wakiwa ni wapya na kuna baadhi ya wachezaji wakiondoka na wengine wapya kudajiliwa.

Kwa R.Madrid mchezaji watakayemkosa sana leo ni Mesut Ozil aliyeuzwa Arsenal na Higuain aliuzwa Napoli lakini wana wachezaji wapya kama Bale aliyenunuliwa kwa record ya dunia, Isco na wengine, lakini mpaka sasa hakuna aliyeweza kuwa na maafa uwanjani kama Ozil.

Barcelona wao hawajapoteza wachezaji muhimu, ila wameongezea mchezaji mwingine mkali, Neymar. Mpaka sasa kacheza mechi 6 kwenye ligi, magoli 2 na assists 5, na hii itakua mara yake ya kwanza kwenye el clasico.

Mpaka sasa Barcelona ana rekodi ya kushinda el Clasico nyingi, 105, dhidi ya hasimu wake,90, huku mechi iliyotoa magoli mengi ikipigwa mnamo mwaka 1948, Madrid 11 - 1 Barcelona.

Tukutane hapa majira ya saa moja jioni kuona historia nyingine ikiandikwa siku ya leo.
 
Possible Line-ups

Barcelona (4-3-3) - Valdez, Alves, Pique, Puyol, Adriano, Busquets, Xavi, Iniesta, Sanchez, Messi, Neymar

Real Madrid (4-2-3-1)
Lopez, Arbeloa, Ramos, Verane, Marcelo, Illarramendj, Khedira, Di Maria, Modric, Ronaldo, Benzema
 
Mkuu tunashukuru kwa uchambuzi mzuri. Wengine kutokana na mambo kadhaa huwa shida kufuatilia statistics za michezo kama hizi!
 
Mkuu tunashukuru kwa uchambuzi mzuri. Wengine kutokana na mambo kadhaa huwa shida kufuatilia statistics za michezo kama hizi!

Karibu.
Zipo nyingi sana Mkuu kuhusiana na mtanange huu, ntaendelea kuwa naweka kadri niwezavyo wakati tunausubiria huu mpambano.
 
Nawapa nafasi Real Madrid na dogo Verane ndio mechi yake hii kung’aa!
 
Pia Madrid watamkosa Alonso kwa kuwa ni majeruhi, na Barcelona watamkosa Jordi Alba.
 
Pia Madrid watamkosa Alonso kwa kuwa ni majeruhi, na Barcelona watamkosa Jordi Alba.

Nadhani ni pigo kubwa sana kwa Real kuliko kwa barca, Alonso hayupo na Ozil naye hayupo.
 
Taarifa zaidi zinasema Carlo Ancelotti amesema huenda Gareth Bale akaanza mechi ya leo, hivyo kuna uwezekano mkubwa Di Maria akaanzia bench.
 
Taarifa zaidi zinasema Carlo Ancelotti amesema huenda Gareth Bale akaanza mechi ya leo, hivyo kuna uwezekano mkubwa Di Maria akaanzia bench.

Saa ngapi inapigwa?
 
Ang'ae wakati Neymar yupo uwanjani.
ALEYN, Neymar nimchezaji mzuri na nina muheshimu!

Verane nae ni mzuri sana kwenye kukaba, na anatumia akili tofauti na pepe!

Ndio maana nikasema ni wakati wake wa kung’aa kwakua ndio mara ya mwanzo Neymar atakutana na Verane!
 
Last edited by a moderator:
Nadhani ni pigo kubwa sana kwa Real kuliko kwa barca, Alonso hayupo na Ozil naye hayupo.

Umenena ukweli mtupu, yule mwanaume akisimama na Khedira pale kati akina Messi walikuwa hawapumui.
 
Back
Top Bottom