El Chapo kuhamishiwa Marekani

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
160109044504_mexico_chapo_guzman_640x360_reuters_nocredit.jpg


Mexico imeidhinisha kuhamishiwa Marekani mlangunzi mkuu wa madawa ya kulevya, Joaquin Guzman, almaarufu El Chapo, ili ashtakiwe kwa mauaji na ulanguzi wa madawa ya kulevya.

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya imesema kuwa Marekani imehakikishia taifa hilo jirani kuwa Guzman hatahukumiwa kifo katika kesi zinazomkabili.

Hivi majuzi Guzman alihamishiwa gereza moja lililoko nchini Mexico hadi lingine lenye ulinzi mkali kwenye mpaka na Marekani.

Mawakili wa Guzman wamesema kuwa watakata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

El Chapo, aliyesimamia kundi la walanguzi wa madawa ya kulevya lijulikanalo kama Sinaloa alikamatwa Januari, miezi sita baada ya kutoroka kutoka gereza moja la Ulinzi Mkali kwa kuchimba mtaro chini ya ardhi hadi katika seli yake.

Source: BBC
 
El chapo.. Huyu jamaa ni mafia hatar atawasumbua sana
Wangempeleka guantanamo tu
 
Namkubali sana Guzman... Dunia inahitaji kuwa na watu hatari kama hawa ili kuongeza ubunifu na akili ya namna ya kujihami nao.. Biashara haramu hutoa majibu haramu siku zote..
 
Mexico ni hatari sana kwa dawa za kulevya hivi karibuni liligundulika bomba lililopo ardhini linalopitisha dawa za kulevya kutoka Mexico mpaka Marekani
 
Sijui kwanini mimi nayakubali sana makundi ya kiharifu ya Mexico, hayadili na raia yao yanadili na kusaka fedha kwa njia haramu tu. Kuna muvi moja inaitwa Sicario ya 2015 Cover lake hapo chini, haishoshwi kuiangalia.
220px-Sicario_poster.jpg
 
Back
Top Bottom