Eight killed, nine injured in two separate Marsabit attacks

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,442
3,352
Pamoja na watu hao nane waliouawa, wengine tisa walijeruhiwa baada ya Watu waliobeba bunduki kufyatua risasi katika maeneo mawili tofauti hapo jana kwenye Kaunti ya Marsabit

Kamanda wa Polisi katika Kaunti hiyo, Steve Oloo amesema mashambulio hayo yalifanyika katika maeneo ya Forole na Sabareh yaliyopo mpakani mwa Kenya na Ethiopia

Inadaiwa Wavamizi hao walivamia sehemu ya kuchota maji katika eneo la Forole muda ambao Wafugaji walikuwa wamelala (majira ya saa kumi alfajiri) na kuua watu ambao miongoni mwao wapo watoto wawili wa miaka 13 na 15

Aidha, wavamizi hao wanaodhaniwa wametoka Ethiopia waliondoka Forole na idadi ya mifugo ambayo haikuweza kutambulika haraka na takribani ng’ombe 500 kutoka eneo la Sabareh
********

Eight people were on Sunday killed and at least 9 others injured after unknown gunmen orchestrated two separate attacks in Marsabit County.

Speaking to Citizen Digital, Marsabit County Police Commander Steve Oloo said the attacks were carried out in Forole and Sabareh areas on the Kenya-Ethiopia border.

The attackers reportedly stormed a watering point in Forole where herders were sleeping at around 4a.m and opened fire killing, among others, two minors aged 13 and 15 years old.

The attackers, suspected to have crossed over from Ethipia, made away with an unknown number of livestock from the Forole and about 500 heads of cattle from Sabareh.

Security officers have since been deployed in the area to tame insecurity and to conduct investigations into the attacks.
 
Poleni sana, ila hii tabia ya Kenya kujenga uadui na kila nchi inayowazunguka itawagharimu sana, sasa hivi uhasama kati ya Kenya na Ethiopia unaongezeka kwa kasi sana, mtakimbilia wapi?.
 
Poleni sana, ila hii tabia ya Kenya kujenga uadui na kila nchi inayowazunguka itawagharimu sana, sasa hivi uhasama kati ya Kenya na Ethiopia unaongezeka kwa kasi sana, mtakimbilia wapi?.
Wale nadhani ni wezi tu mkuu,

Sidhani kama kuna dalili zozote za uhasama katika hili.
 
Wale nadhani ni wezi tu mkuu,

Sidhani kama kuna dalili zozote za uhasama katika hili.
Lakini wezi wakitokea kwa jirani yako ambaye hampatani, sio rahisi kumkimbiza na kumfuata akiingia akivuka mipaka na kujificha kwa huyo adui wako.
 
Lakini wezi wakitokea kwa jirani yako ambaye hampatani, sio rahisi kumkimbiza na kumfuata akiingia akivuka mipaka na kujificha kwa huyo adui wako.
Unajua Marsabit kuna waoromo. Hawa wezi most likely ni Oromos from Ethiopia stealing from Oromos from Kenya. Ama somalis from ethiopia stealing from oromos ama somalis in the northern region of kenya. So si Kenya vs Ethiopia. Nikama Maasai wa Kenya na maasai wa Tz
 
Tatizo la cross border crime linadhibitiwa kwa urahisi sana kama kuna maelewano na ushirikiano kati ya nchi husika, umeona jinsi Tanzania na Msumbiji walivyoshirikiana kufuatia Yale mauaji yalivyotokea kule Msumbiji hivi karibuni?, isingewezekana kwa POLISI wa Tanzania kuruhusiwa kuingia Msumbuji kuwasaka na hatimaye kuwakamata wahusika kama Tanzania na Msumbiji hazinamaelewano mazuri, hiyo ndio siri ya Tanzania kuwa na Amani tangu tujipatie Uhuru WETU, jifunzeni kuishi vizuri na majirani zenu, punguzeni kujifanya wajuaji katika kila jambo.
 
Back
Top Bottom