Pamoja na kuwa Bajeti ya Serikali ilipitishwa kwa mbwembwe hadi leo HAZINA haijaweza kutoa fedha za Matumizi ya Kawaida na wala za Maendeleo. Tunavyoandika hata Ankara za Mishahara hazijatoka na Mwezi Julai ndio unakwisha. Kawaida watumishi wa Serikali hupokea Mishahara tarehe 23 ya kila Mwezi. Watumishi wanaingia kwenye sikukuu ya EID bila senti. Mwenyezi Mungu wanusuru wasianze biashara ya viungo vya binadamu.