Hii ndio Taarifa ya sasa kutoka Tamisemi
Sasa shule zote zitafunguliwa July 13
Sasa shule zote zitafunguliwa July 13
- Tunachokijua
- Kupitia mitandao ya kijamii kumekuwa na barua inayosambaa ikidaiwa kutolewa na serikali kueleza kuwa muda wa wa kufungua shule umesogezwa mbele kutoka Julai 6, 2025 hadi Julai 13, 2026 kutokana na sababu zilizotajwa kwenye barua.
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umejirirdhisha kuwa Taarifa hiyo si ya kweli na haijachapishwa na mamlaka husika kama ilivyodaiwa.
Taarifa hiyo imekuwa na baadhi ya dosari ikiwemo kutumia utambulisho wa Ofisi ya Rais TAMISEMI badala ya Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI kama wizara hiyo ilivyohamishwa kutoka ofisi ya Rais kwenda kwenye ofisi ya Waziri Mkuu.
Aidha jina la waziri wa elimu lililowekwa si sahihi wametumia jina la Dkt. Lyabwene Mtahabwa ambaye si Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia na badala yake Waziri ni Prof. Adolf Mkenda.
Wizara hizo pia kupitia mitandao yao ya kijamii wamekanusha taarifa hiyo na kueleza kuwa siyo sahihi. Sambamba na hilo kupitia akaunti yao ya JamiiForums wizara ya elimu wameweka kalenda yao ya mwaka wa masomo 2026 ambapo tarehe ya kufungua shule ni Jula6, 2026.