Mlyuha
JF-Expert Member
- Apr 27, 2015
- 239
- 94
Nimeshangaa sana nilivoenda TRA kupata leseni ya biashara nikaambiwa lazima nilipie kwanza Mashine ya EFD ndiyo nipate leseni!! NAAMINI katika kulipa kodi lakini huu utaratibu siyo mzuri kwani wengi wanaoanzisha biashara mitaji ni midogo sana haifikii hata laki 5 sasa hiyo ya kulipia EFD mashine laki 7 tutaipata wapi?
Nashauri TRA waangalie namna gani ya kudai kodi kwa wajasiriamali tunaoanza biashara na siyo kulazimisha EFD machine. Kuna namna nyingi ya kukusanya kodi na siyo lazima hizo mashine. Baada ya kipindi fulani basi ndo kuwepo na sheria ya kununua hizo mashine wakati mtaji umekuwa.