EFD: Arusha Mgomo wa wafanyabiasha

EFD: Arusha Mgomo wa wafanyabiasha

Status
Not open for further replies.

Alvin Slain

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2011
Posts
6,375
Reaction score
3,665
Ujumbe mzito unaosambazwa kwa kasi ukihamasisha wafanyabiasha na wenye Maduka kugoma kuanzia kesho,

Mgomo huu ni kugomea mashine za kieletronic kwa ajili ya kutolea resiti,

Mikoa kadhaa ikiwemo Mwanza,Dar,Morogoro nk
wamegoma mapema wiki hii.

Updates..............
Niko eneo la stend kuu ya Mabasi ya Mikoani,
huku maduka mengi yakiwa yamefungwa watu walioko maeneo haya wamesimama kwa makundi wakijaribu kulichambua suala hili kwa undani zaidi.

Baada ya wafanyabiashara wengi hapa Mkoani. Arusha,
Kikao Maalum kimeandaliwa katika ukumbi wa Golden Rose Mjini hapa,

Updates.........
Mwenyekiti wa Maduka Stendi ya juu anajitambulisha hapa

Hoja iliyoko hapa ni EFD.
 
Ujumbe mzito unaosambazwa kwa kasi ukihamasisha wafanyabiasha na wenye Maduka kugoma kuanzia kesho,

Mgomo huu ni kugomea mashine za kieletronic kwa ajili ya kutolea resiti,

Mikoa kadhaa ikiwemo Mwanza,Dar,Morogoro nk
wamegoma mapema wiki hii.

Madai yenu hayana msingi kabisa bora mngelalamikia lugha ya mawasiliano kwenye hizi mashine kuliko kulalamikia kiwango cha bei ya mashine. Mimi lalamiko langu ni kuwa zinaniongezea gharama maana lazima niwe na mtu anaayeelewa kutoa risiti, kutuma Z report kila siku na mwenye kujua kidhungu.
 
Mashine hizi zinasadikika ni Mpango wa Mafisadi kupata fedha za Uchaguzi Mkuu Mwakani.
Kwani tulipokua tunatumia Vitabu vya Riziti nini kilikua kinaharibika?
 
Mlikuwa mnadanganya mauzo ya bidhaa zenu na hivyo kulipa kodi kidogo.
 
Kutumia hizi machine sio ombi, ni lazima, wagome, waandamane, wazire etc watazitumia tu! huu ndio ukweli mchungu!
 
Sio kila kitu kipelekwe kisiasa wameibia sana serikali ktk kulipa kodi.
Watazinunua na kodi walipa.
 
Kutumia hizi machine sio ombi, ni lazima, wagome, waandamane, wazire etc watazitumia tu! huu ndio ukweli mchungu!

We MSALANI jaribu kutumia muda kufikiri kujibu hoja sio unakurupuka tu???
 
Last edited by a moderator:
mashine hizi zinasadikika ni mpango wa mafisadi kupata fedha za uchaguzi mkuu mwakani.
Kwani tulipokua tunatumia vitabu vya riziti nini kilikua kinaharibika?

mlikuwa hamtoi risiti kwa wateja,mnatoa risiti bandia ambazo tra hawazitoi,kwa kifupi hamkatwi kodi halali.zamu yenu kulipa halali sio wafanyakazi tu
 
kutumia hizi machine sio ombi, ni lazima, wagome, waandamane, wazire etc watazitumia tu! Huu ndio ukweli mchungu!

asiyetaka mashine arudishe leseni ya biashara mashamba yapo mengi,wengine wanagoma hata hawajui wanachogoma
 
Unajua hili jambo la kuishi kwa kutumia njia za mkato mkato limeshakuwa utamaduni wa mtanzania. Kila sehemu lipo. Sasa hawa wafanya biashara hawataki kueleza ukweli kuwa tatizo kodi ni kubwa hivyo ipunguzwe, bali wametoa sababu za kitoto kabisa.
 
Sioni kama izo mashine zina tatizo lolote I think watu wanaogopa coz itakua ngum ku evade tax
 
Madai yenu hayana msingi kabisa bora mngelalamikia lugha ya mawasiliano kwenye hizi mashine kuliko kulalamikia kiwango cha bei ya mashine. Mimi lalamiko langu ni kuwa zinaniongezea gharama maana lazima niwe na mtu anaayeelewa kutoa risiti, kutuma Z report kila siku na mwenye kujua kidhungu.

.....ni kweli mimi nimelazimiswa tu kufunga lkn sijawahi kuona mgomo wa kipuuzi kama huu , maana tunagoma kwa kufunga maduka yetu na waathirika wakuu ni sisi wenyewe , mgomo unatakiwa ulete madhara kwa yule unaemlalamikia. hata hivyo tunalipa kodi kwa mujibu wa sheria na hatuwezi kupindisha sheria na kamwe serzkali haiwezi kughairi mashine maana hata wafadhili wanataka waone tunavyojitahidi kukabiliana na matatizo yetu.
 
Mashine hizi zinasadikika ni Mpango wa Mafisadi kupata fedha za Uchaguzi Mkuu Mwakani.
Kwani tulipokua tunatumia Vitabu vya Riziti nini kilikua kinaharibika?

Hawa watakuwa Bavicha wenye akili za mgando mmmmmmm hatari kweli kweli
 
Ujumbe mzito unaosambazwa kwa kasi ukihamasisha wafanyabiasha na wenye Maduka kugoma kuanzia kesho,

Mgomo huu ni kugomea mashine za kieletronic kwa ajili ya kutolea resiti,

Mikoa kadhaa ikiwemo Mwanza,Dar,Morogoro nk
wamegoma mapema wiki hii.

mlipe tu kodi,mbona wafanyakazi tunachuliwa kiasi kikubwa tu cha kodi
 
Acheni basi kazi za kuajiriwa fungua biashara na wewe Kama unaona wafanya biashara tunafaidi kutolipa kodi, sa Kama hatulipi kodi sijui huo mshahara mngelipwa na nini hela za EPA, faida zitokanazo na pembe za ndovu ama madawa ya kulevya?
 
Watu wanagoma kulipa kodi mara mbili huyo anasaport nini?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom