Tetra
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 1,520
- 764
::
Kila nikikutazama
Najawa na faraja
Yule aliyekuanzisha
Alijawa hekima
Akakuweka hapa
Ee jamiiforum
Kila la kheri 2013
::
Umenifanya nijivunie
Umenifanya nifikirie
Hukuniacha nizubae
Umenifanya nisituke
Umenifanya nielimike
Ee jamiiforum
Kila la kheri 2013
::
U chakula cha akili
Kwa hoja unazojadili
Unao watu makini
Hazina bora nchini
Kipenzi cha wakweli
Ee jamiiforum
Kila la kheri 2013
::
U bora ktk mitandao
Unatujenga ubongo
Huhadaiwi na uso
Unadadisi upeo
Usibadili mwelekeo
Ee jamiiforum
Kila la kheri 2013
::
Tuongoze kwa adabu
Na mola akupe nguvu
Udumu miaka elfu
Usifungiwe na wenye wivu
Udumu hadi dawamu
Ee jamiiforum
Kila la kheri 2013
::
Umeangazia siasa
Tukaondokewa shaka
Habari ukatupasha
Tukawajua watawala
Kwa ubaya na wema
Ee jamiiforum
Kila la kheri 2013
::
Umefanya tupendane
Mahusiano tudumishe
Familia tuzielewe
Urafiki tuujenge
Ukatutenga na upweke
Ee jamiiforum
Kila la kheri 2013
::
Tunapochoka kufikiri
Tunafurahia utani
Tunacheka kwa tani
Utalingana na nani
Kwa ulivyojisheini
Upekee ni yako shani
Ee jamiiforum
Kila la kheri 2013
::
Una majukwaa kibao
Yenye kuinua upeo
Usiupoteze mwelekeo
Ndio huu tuupendao
Uimarishe kila uchao
Ee jamiiforum
Kila la kheri 2013
::
Nakuomba ee Mungu
Members uwatunuku
Uwape hekima na utu
Washauri bila uchovu
Nchi ijawe utulivu
Ndoa zote zidumu
Ee jamiiforum
Kila la kheri 2013
=
Kila nikikutazama
Najawa na faraja
Yule aliyekuanzisha
Alijawa hekima
Akakuweka hapa
Ee jamiiforum
Kila la kheri 2013
::
Umenifanya nijivunie
Umenifanya nifikirie
Hukuniacha nizubae
Umenifanya nisituke
Umenifanya nielimike
Ee jamiiforum
Kila la kheri 2013
::
U chakula cha akili
Kwa hoja unazojadili
Unao watu makini
Hazina bora nchini
Kipenzi cha wakweli
Ee jamiiforum
Kila la kheri 2013
::
U bora ktk mitandao
Unatujenga ubongo
Huhadaiwi na uso
Unadadisi upeo
Usibadili mwelekeo
Ee jamiiforum
Kila la kheri 2013
::
Tuongoze kwa adabu
Na mola akupe nguvu
Udumu miaka elfu
Usifungiwe na wenye wivu
Udumu hadi dawamu
Ee jamiiforum
Kila la kheri 2013
::
Umeangazia siasa
Tukaondokewa shaka
Habari ukatupasha
Tukawajua watawala
Kwa ubaya na wema
Ee jamiiforum
Kila la kheri 2013
::
Umefanya tupendane
Mahusiano tudumishe
Familia tuzielewe
Urafiki tuujenge
Ukatutenga na upweke
Ee jamiiforum
Kila la kheri 2013
::
Tunapochoka kufikiri
Tunafurahia utani
Tunacheka kwa tani
Utalingana na nani
Kwa ulivyojisheini
Upekee ni yako shani
Ee jamiiforum
Kila la kheri 2013
::
Una majukwaa kibao
Yenye kuinua upeo
Usiupoteze mwelekeo
Ndio huu tuupendao
Uimarishe kila uchao
Ee jamiiforum
Kila la kheri 2013
::
Nakuomba ee Mungu
Members uwatunuku
Uwape hekima na utu
Washauri bila uchovu
Nchi ijawe utulivu
Ndoa zote zidumu
Ee jamiiforum
Kila la kheri 2013
=