Ee JamiiForums, Kila la kheri 2013

Tetra

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
1,521
2,000
::
Kila nikikutazama
Najawa na faraja
Yule aliyekuanzisha
Alijawa hekima
Akakuweka hapa
Ee jamiiforum
Kila la kheri 2013
::
Umenifanya nijivunie
Umenifanya nifikirie
Hukuniacha nizubae
Umenifanya nisituke
Umenifanya nielimike
Ee jamiiforum
Kila la kheri 2013
::
U chakula cha akili
Kwa hoja unazojadili
Unao watu makini
Hazina bora nchini
Kipenzi cha wakweli
Ee jamiiforum
Kila la kheri 2013
::
U bora ktk mitandao
Unatujenga ubongo
Huhadaiwi na uso
Unadadisi upeo
Usibadili mwelekeo
Ee jamiiforum
Kila la kheri 2013
::
Tuongoze kwa adabu
Na mola akupe nguvu
Udumu miaka elfu
Usifungiwe na wenye wivu
Udumu hadi dawamu
Ee jamiiforum
Kila la kheri 2013
::
Umeangazia siasa
Tukaondokewa shaka
Habari ukatupasha
Tukawajua watawala
Kwa ubaya na wema
Ee jamiiforum
Kila la kheri 2013
::
Umefanya tupendane
Mahusiano tudumishe
Familia tuzielewe
Urafiki tuujenge
Ukatutenga na upweke
Ee jamiiforum
Kila la kheri 2013
::
Tunapochoka kufikiri
Tunafurahia utani
Tunacheka kwa tani
Utalingana na nani
Kwa ulivyojisheini
Upekee ni yako shani
Ee jamiiforum
Kila la kheri 2013
::
Una majukwaa kibao
Yenye kuinua upeo
Usiupoteze mwelekeo
Ndio huu tuupendao
Uimarishe kila uchao
Ee jamiiforum
Kila la kheri 2013
::
Nakuomba ee Mungu
Members uwatunuku
Uwape hekima na utu
Washauri bila uchovu
Nchi ijawe utulivu
Ndoa zote zidumu
Ee jamiiforum
Kila la kheri 2013
=
 

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,102
2,000
WOW! Tetra ngoja niongee na Invisible akupe walau bronze membership,,nice pome!!!
Mwone kwanza...

Kazi kuelekeza wengine tu! Nawe tangu ujiuge 2008 huchangii walau Tshs 20,000? Hujakusanya zikafika? Utafurahi kusikia tunawatangazia tumeelemewa tunasimamisha huduma?

Hahaha, najua ni utani unaochoma,,, tafakari na kisha chukua hatua!

:glasses-nerdy:
 

Madame B

JF-Expert Member
Apr 9, 2012
28,876
2,000
Mwone kwanza...

Kazi kuelekeza wengine tu! Nawe tangu ujiuge 2008 huchangii walau Tshs 20,000? Hujakusanya zikafika? Utafurahi kusikia tunawatangazia tumeelemewa tunasimamisha huduma?

Hahaha, najua ni utani unaochoma,,, tafakari na kisha chukua hatua!

:glasses-nerdy:

Na ujumbe huu uwafikie wooooote wasiopenda kuichangia JF yetu.
 

Nsiande

JF-Expert Member
Jul 27, 2009
1,649
1,195
Tutachangiaje ujue ni sisi yaani nsiande halafu usione my real name yaani nsiande aikaruwa makundi...halafu nikianza kuchangia point mnipersonolize kama le mutuz kila mtu anamjua na kumzodoa kisa sheaholda ?
 

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,102
2,000
Tutachangiaje ujue ni sisi yaani nsiande halafu usione my real name yaani nsiande aikaruwa makundi...
Seriously? Na hii ni sababu? OMG! Na ukienda M-PESA ukamwambia atume yeye umpe 1,000 kama gharama ya kutuma bado jina litakuja lako? Kuna bank inalazimisha anayetuma pesa kuandika real name? Eng. Nsiande, are you serious?

:confused2:
 

Madame B

JF-Expert Member
Apr 9, 2012
28,876
2,000
Duh, na wewe naona hujachangia. Nikurushie dongo? Ha ha ha... Hivi kweli hakuna lolote mnalofaidika na uwepo wa JF? Seriously?

Haaaaaaaaaaa....... Invisible vipi bhana, me nakusaidia kuwapa vipande vyao afu unanigeuka.
Kiukweli vipo vingi sana tulivofaidika navyo.
nasubiri January Mosi, Ni lazima nichangie Penyewe JF.

Usiku mwema...........tumemaliza mada au!!!
Haya
 
Last edited by a moderator:

Tetra

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
1,521
2,000
Oo! Invisible in the house,,THANKS A MILLION kwa jukumu zito linalotuachia faida nyingi,never give tutajitahidi kuchangia tunavyoweza.

TUNATAMBUA THAMANI YENU KWETU

I real appreciate you!
 

Tetra

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
1,521
2,000
Madame B, nimepata vema na najitahidi kuelewa uzito wa unachoongea! Give us time to prove ourselves right..THANKS,, FOR I ALWAYS LEARN FROM YOU
 
Last edited by a moderator:

Mentor

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
20,341
2,000
Mwone kwanza...

Kazi kuelekeza wengine tu! Nawe tangu ujiuge 2008 huchangii walau Tshs 20,000? Hujakusanya zikafika? Utafurahi kusikia tunawatangazia tumeelemewa tunasimamisha huduma?

Hahaha, najua ni utani unaochoma,,, tafakari na kisha chukua hatua!

:glasses-nerdy:


I have done the needful..nangojea kuona effects.

cc: Invisible
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom