Edward Lowassa special thread

Lowasa akipita 5bora hakuna wa kumzuia huko mbele.
 
Lowasa haendi popote.eti anatishia kwenye vyombo vya habari kwamba asipopitishwa patachimbika.hili zee mwehu kabisa na hai waganga njaa wanaompigia debe wajiandae kisaikolojia.
 
kaka umekula.chakula gani kinachokufanya uhalee uaroooo kama wakoo
 
Nimekuelewa...kwamba ni analzimisha kuwe na deal...yaani aendelee kula mema hata kama amekatwa na kukubali kuisupport ccm.it is a wise but not intellectual game!
Mkuu,
Lowassa anaifahamu vizuri sana CCM.

Mbinu anayotumia Lowassa ni copy and paste ya mbinu aliyotumia Rais Kikwete katika kutafuta kuteuliwa kuwa mgombea Urais.

Hoja ya msingi, kama Rais Kikwete alitumia mbinu hii na kupata alichokuwa anakitafuta, itakuwaje leo akione ni haramu?
 
Mtikila anamsubiri kisutu, Lowassa ngumu sana na wanaomshabikia mambulula kama yeye...
 
Reactions: G3T
kama ana tuhuma mbona mnasita kumfikisha mbele ya mahakama ili haki itendeke kama ilivyotokea kwa mramba na yona? au hamna ushahidi? whats behind all these secrets, kama hamna ushahidi mimi naamini huko ni kuchafuana
 
Mtu ulikuwa kiongozi mkubwa tuu tena waziri mkuu,na haukusaidia kubadirisha hali ya uchumi zaidi ya ufisadi na kuchumia tumbo lake tu.

Sipati picha hali alyonayo sasaivi,wa mkate tuu.
 
Kuirudisha tena ccm madarakani wakati huu ni kujitafutia majanga ya ajabu kwenye nchi hii
 
Kama atakatwa kwa hila atahama kweli na huo ndiyo utakuwa mwisho wa ccm.
 
pumba katika ubora wake.

 
Hayati Moringe Sokoine alimuamini ndugu yake Lowassa na ndio maana akampeleka akapigane Vita vya Idd Amin akiwa kati ya wasomi vijana toka Chuo Kikuu Dar-es-salaam, na baada ya vita kapelekwa na Nyerere UK kusomea Uchumi.

LOWASSA NA AWAMU ZOTE 4

Awamu ya 1: imani juu ya Lowassa ipo pale pale kwa Nyerere alipomteua katibu katika taasisi nyingi za Serikali japo alikuwa mdogo sana kiumri.

Awamu ya 2: Mzee Mwinyi alimuamini sana Lowassa na kumteuwa Mkurugenzi wa AICC japo alikuwa kijana mdogo, na pia kumpeleka katika Baraza la Mawaziri.

Awamu ya 3: Mzee Mkapa alimuamini sana Lowassa, alimpa Wizara zinazohitaji uchapaji kazi wa hali ya juu na uzalendo ulio tukuka.

Awamu ya 4: Prof Jakaya Kikwete kwa zaidi ilidhihirika imani juu ya umakini na utendaji wa Lowassa, kwani alimpa Uwaziri Mkuu wa Tanzania na hadi sasa Serikali nzima bado ina imani kubwa kwani yeye ndie Mwenyekiti katika Bunge Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.

CCM: Wadhamini aliowapata Lowassa peke yake ni zaidi ya 90% ya wagombea wengine wote wa CCM.
ZANZIBAR: Sultani wa Pemba Maalim Seif pamoja kuwa ni Kiongozi wa CUF lakini aliwataka Wapemba wachukue haraka Kadi za CCM ili Lowassa apate udhamini wa kutosha Pemba, na kweli Lowassa pekee alipata Wadhamini 450 ndani ya nusu saa, wengine walisota siku kibao na kuondoka bila udhamini.

Baada ya hayo, sisi Wananchi sasa ni zamu yetu, tuleteeni Lowassa tumpe kura za Watanzania wote hadi upinzani.
By Sipano Kilimanjaro
Kiwengwa Zanzibar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…