multmandalin
JF-Expert Member
- Sep 8, 2012
- 2,034
- 584
TAARIFA KWA 4U MOVEMENT DODOMA.
Habari, Wana 4u movement mliopo Dodoma na Watanzania wote wenye mapenzi mema na Edward Lowassa tunawaasa kutovaa T-shirt zozote za 4u movement au zenye jina la Edward Lowassa katika kipindi chote cha mikutano ya Chama.
Najua na kutambua hadi jana tarehe 07/07/2015 zaidi ya wana 4u movement 3600+ plus wamewasili Dodoma lakini wingi wetu usiwe sehemu ya kuwa chanzo cha vurugu ya Aina yeyote.
Tuna Taarifa za kuaminika kuna watu wenye mpango wa kutumia T-shirt zetu za 4u movement kufanya vurugu ndani ya Mji wa Dodoma kwa makusudi ili kuiondelea sifa ya utulivu na umakini wa Movement yetu. Yeyote atakae husika kufanya fujo au vurugu zozote kwa Makusudi huku akitumia jina letu tutakuwa msatari wa Mbele kumshughulikia.
Tunawaasa na kuwaomba wana 4umvt na Watanzania wote kuwa watulivu na wavumilivu na kuwapa nafasi Wajumbe wote wa vikao vya Maamuzi kwa kutii na kufuata kanuni za chama kufanya maamuzi kwa Utulivu maana ule wakati mabadiliko uliotabiriwa na Baba wa Taifa kuwa ukifika Basi mabadiliko tutayapata ndani ya CCM na tukikosa tutayapata nje ya ccm lakini ipo nafasi kubwa sana ya kuyapata Mabadiliko haya ndani ya CCM chini ya Balozi wetu wa 4u movement Mh Edward Lowassa.
Ahsanteni
Hemedy Ally
Mratibu Taifa (National Coordinator)
@4u movement
# UTUMISHI
# UWAJIBIKAJI
# UMOJA
# UZALENDO
kweli huna akili, lowasa ni nani katika nchi hii.
utamjua baada ya kupata NGEU
Nyambaf umezoea kumeza dushelele ya zitto sasa unafikiri kisu ni rahisi hivyoPamoja na nguvu kubwa ya mazingaombwe aliyokua nayo ya kucheza na media pamoja na fedha chafu hizi ndo sababu maalum hawezi kupita hata mchujo wa kwanza wa NEC(5 bora)
1.Ana tuhuma nzito za ufisadi wa richmond uliosababisha kujiuzulu na kutikisika kwa serikali 2008.Tuhuma hizi hakuweza kusafishwa mahakamani(walimbeba ) jambo linalopelekea tuhuma kusimama palepale kisheria
2.Operation VUA GAMBA, target ya hii kauli mbiu ilikua ni lowassa,Mara baada ya kujeruhiwa bungeni 2008 chama chake kiliona ufisadi ni tatizo kikaanzisha operation ambayo ilipanga kumwangamiza kabisa kisiasa ndugu Ngoyayi alikwepaje tumuulize NAPE ,hapa maana yake chama chake chama chake HAKIMTAKI
3.Amekiuka sheria ya fgarama za uchaguzi ya mwaka 2011 kifungu Namba 14(1_2)mma kifungu namba 20(1-4) sambamba na kifungu namba 24 cha sheria hiyo ambayo inakataza mgombea yoyote wa nafasi ya urais,ubunge au udiwani .Ikumbukwe hadi sasa Lowassa ametumia zaidi ya billioni 50 kwa ajili ya kuwahonga waandishi wahabari,wenyeviti wa CCM wa mikoa,wabunge,waandesha bodaboda,maaskofu,mashekhe na hivi juzi ametumia zaidi ya shilingi billion 35.5 kuwahonga REDET
4.Lowassa amezungukwa na wapambe ambao wana criminal records za kifisadi baadhi ni Rostam,Andrew chenge,Nazir Karamagi,Anna Tibaijuka,Kingunge etc....
5.Ugonjwa wake ,mzee ana mgogoro wa Afya si vizuri kuweka details zote hapa lakini hata nyie wenyewe mmeshajionea ameanguka mara kadhaa katika safari tu za kutafuta wazamini kutkana na power ya media manipulation hamkutangaziwa
6.Alianza kampeni kabla ya wakati ,hamna asiyetambua yeye na wenzake walianza kampeni mapema hadi ikasababishia adhabu ,hata hivyo kipindo cha adhabu alikua bado anaendelea na kampeni hii tafsiri yake ni UTOVU WA NIDHAMU
Ni hayo tu
Jamani hatunywi viloba? Lowasaaaaaaa lowasaaaaaa! Aaaaaaaaaaaagh!
Eti Watz wote kwa ujumla hakuna Mtanzania mwenye akili timamu akamshabikia fisadi, sema wasakatonge wenzako ndio wawe na utulivu.
Pamoja na nguvu kubwa ya mazingaombwe aliyokua nayo ya kucheza na media pamoja na fedha chafu hizi ndo sababu maalum hawezi kupita hata mchujo wa kwanza wa NEC(5 bora)
1.Ana tuhuma nzito za ufisadi wa richmond uliosababisha kujiuzulu na kutikisika kwa serikali 2008.Tuhuma hizi hakuweza kusafishwa mahakamani(walimbeba ) jambo linalopelekea tuhuma kusimama palepale kisheria
2.Operation VUA GAMBA, target ya hii kauli mbiu ilikua ni lowassa,Mara baada ya kujeruhiwa bungeni 2008 chama chake kiliona ufisadi ni tatizo kikaanzisha operation ambayo ilipanga kumwangamiza kabisa kisiasa ndugu Ngoyayi alikwepaje tumuulize NAPE ,hapa maana yake chama chake chama chake HAKIMTAKI
3.Amekiuka sheria ya fgarama za uchaguzi ya mwaka 2011 kifungu Namba 14(1_2)mma kifungu namba 20(1-4) sambamba na kifungu namba 24 cha sheria hiyo ambayo inakataza mgombea yoyote wa nafasi ya urais,ubunge au udiwani .Ikumbukwe hadi sasa Lowassa ametumia zaidi ya billioni 50 kwa ajili ya kuwahonga waandishi wahabari,wenyeviti wa CCM wa mikoa,wabunge,waandesha bodaboda,maaskofu,mashekhe na hivi juzi ametumia zaidi ya shilingi billion 35.5 kuwahonga REDET
4.Lowassa amezungukwa na wapambe ambao wana criminal records za kifisadi baadhi ni Rostam,Andrew chenge,Nazir Karamagi,Anna Tibaijuka,Kingunge etc....
5.Ugonjwa wake ,mzee ana mgogoro wa Afya si vizuri kuweka details zote hapa lakini hata nyie wenyewe mmeshajionea ameanguka mara kadhaa katika safari tu za kutafuta wazamini kutkana na power ya media manipulation hamkutangaziwa
6.Alianza kampeni kabla ya wakati ,hamna asiyetambua yeye na wenzake walianza kampeni mapema hadi ikasababishia adhabu ,hata hivyo kipindo cha adhabu alikua bado anaendelea na kampeni hii tafsiri yake ni UTOVU WA NIDHAMU
Ni hayo tu
Sioni mtu wa kukata jina la Lowasa mpaka sasa,Lowasa ni mtaji wa ccm na kama atapitishwa atakuwa Rais wa kwanza kupita bila kupingwa.
baada ya kesho ukamtembelee lowassa ICUhuwezi kupata comment coz ni upuuzi tu ulioandika, so watu wamekupuuza kama wapuuzi wengine!!