Akiongea bungeni juu ya tukio la kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni kumtaka katibu wa bunge amtumie tiketi mbunge wa viti maalum ili aende DUBAI alaponde nae raha, na kusitisha ziara aliyokwenda kiserikali nchini Uingereza, Mwigulu Mchemba alisema;
"Hivi mimi nina mkosi gani jamani........"
hapo kwenye ........... alisema tukio zima lilivyofanyika. Pamoja na kukiri kuwa lalamiko lake Bw. Mwigulu lilikuwa la kisiasa zaidi, still uhalisia unabaki pale pale kuwa watanzania tumekuwa na bahati mbaya sana kuwa kwenye nchi ambayo watu wanapindisha ukweli makusudi kwa manufaa yao binafsi.
leo watu wengi akiwemo MAKO, wanadai kuwa wadhamini anaowapata EL ni baada ya kuwapa fedha ili wamdhamini. hapa ndipo unapokuja ule msemo maarufu wa "KUNYATA ANYATE KINYONGA, AKINYATA KICHECHE, ANANYEMELEA KUKU"
Pamoja na wapinzani wa EL kukiri kuwa "Mwakyembe" ni mnafiki baada ya kutetea muundo wa serikali mbili kwenye katiba mpya ili hali thesis yake ya PhD ali-recommend 3 kwa hoja za msingi, still wanajidai hamnazo juu ya hukumu ya kamati teule ya bunge dhidi ya EL.
Ikumbukwe kamati teule ya bunge chini ya uenyekiti wa "Mwakyembe" uliacha kumuhoji EL wa cheap judgement kuwa "Tuliona tungemuhoji, angeharibu ushahidi"
Miaka 8 baada ya tukio lile bado maadui wa EL wanahaha kuuaminisha umma kuwa EL anahonga ili kupata wadhamini. Wagombea zaidi ya 35 wamezunguka kutafuta wadhamini na kuwapata, watu hawalalamiki lakini kwa EL tu ndo wanabwabwaja
na hapa ndipo tusioshabikia siasa na badala yake reality tunapoamua kuu-edit msemo wa kunyata kinyonga na kuku kuwa;
"WADHAMINI APATE "MAKO", AKIPATA "EL" KAWAHONGA"