* Ya Mbeya sio gharika wala mafuriko bali ni MARAMZAMISI...
* Kwa mara nyingine Lowassa avuna wadhamini zaidi ya elfu hamsini na tatu (53,000+)...
* Aweka historia Mbeya...
Baada ya ile gharika ya jana mkoani Kilimanjaro leo hii yaliyotokea mkoa wa Mbeya yamenifanya nikose jina sahihi. Ndipo nilipompigia babu yangu kisha kumueleza na kumuuliza haya yaliyotokea Mbeya tuyaiteje?, manake naona ni zaidi ya gharika ama mafuriko..
Babu akaniambia mjukuu wangu hayo yaliyotokea Mbeya ni maramzamisi, akimaanisha (Maporomoko ya mvua za radi yaliyokuwa yanatokea katika mlima SINAI)...
Ni wazi jiji la Mbeya limefanya kile ambacho hakijawahi kutokea katika historia ya nchi hii... Lowassa kwa mara nyingine kavunja rekodi kwa kuvuna maelfu na maelfu ya wadhamini kutoka katika mkoa huo (zaidi ya wadhamini 53,000+)....
Pamoja na hilo umati mkubwa sana umejitokeza kutoka pande na viunga vyote vya jiji hilo ili kumlaki na kumsalimia Lowassa, ambaye ameonekana akiwa na nyuso ya furaha alipoona wananchi walivyo na matarajio makubwa ya kuanza safari ya matumaini...
"Hii haijawahi kutokea na sijawahi kuona tokea nizaliwe, huyu ndio mkombozi wetu wa maendeleo tunayemtarajia. Nafikiri hapa ni suala la muda tu ndio linasubiriwa mafuriko haya yanatoa picha halisi ya nguvu ya Lowassa" amesikika Mzee Mole akiongea...
My take: Hii ndio safari ya matumaini, mchakamchaka wa maendeleo...
Nilikuwa nampinga sana ila imebidi nianze kumkubali tu kwani kinywa kimeonekana kuzidiwa na nafsi... Jamani enhee tusipoteze muda, huyu ndiye rais wa Tanzania. Upinzani tujipange na upya kwa mechi ijayo 2020, ila hii ya 2015 ina wenyewe , na wenyewe ni wa kina Lowasa na CCM yao.
N.B:Mimi ni #CHADEMA damu damu, hata ukinichanja damu inatoka CHADEMA.