Edward Lowassa: Pasipo Tume Huru ya Uchaguzi, CCM itaendelea kutangazwa mshindi kila siku

Kama tume sio huru wabunge wa chadema waliwezaje kushinda chaguzi na kuwa wabunge? Mfano akina mbowe,sugu,godbless Lema ,Msigwa,MDEE ,MNYIKA nk waliwezaje kuwa wabunge kama tume sio huru? hizo ni porojo baada ya kushindwa
No kwelibtume siyo huru lakini kipindi cha kikwete kulikuwa hakuna udikteta kwani wanaweza kulinda kura zao na wanaruhusiwa mawakala wao kuingia na hakutakuwa na urembo wa polisi kikulazimisha kulikopitiliza kama awamu hii chini ya utawala wa udikteta.
Maana mwenyewe dikteta amesema nikulipe mshahara na marupurupu halafu kutangazwa mpinzani? Ndiyo maana inabidi utumie nguvu nyingi hata kutoa roho za watu.
Hata 2015 mbona yalikamatwa mabox ambayo yamesha pigwa kura kabla ya kuiongoza vituoni? Vunjo waliamua kumfungia kada wa CCM na mabox yake mpaka uchaguzi umalizike, ingekuwa kipindi hiki cha dikteta hao waliokamata hayo mabox wangepigwa na polisi na kubambikiwa kesi.
Tatizo tume siyo huru + udikteta yaani kitu hatari kimeongezeka
 
Naona Viongozi wengi wa CHADEMA wamepamba moto. Wote wanaongelea juu ya Tume Huru ya Uchaguzi ama kususia uchaguzi.
Ndiyo sababu pekee iliyobakia Mkuu, watasema nini? Ndiyo maana tunasema hiki chama kitakufa kwasabbu hakitaki ku adress matatizo yake ya msingi inachokikabili.

Toka mfumo wa vyama vingi uanzishwe nchini, sababu yao kubwa ya kushindwa uchaguzi ni kuibiwa kura na Tume huru ya Uchaguzi. Lakini wanaposhinda kwenye majimbo huisikii hii sababu hata siku moja.
 
Hiyo nguvu imeisha?
Nguvu ya ziada haiwezi kutumia kwenye utawala huu wa kidikteta ukumbuke CCM wana jeshi, polisi na mahakama zote ni zao, lakini tawala zilizo pita polisi ilikuwa kazi yake ni kulinda raia na mali zake, hata kama kulikuwa na makosa madogo madogo, lakini polisi ya sasa ni kulinda CCM.
Mfano mzuri ni Ditopile alivyo mshoot dereva wa daladala alijikabidhi mwenyewe polisi na akiandika resignation letter kwa rais na akaendelea na kesi. Utawala huu leo afanye mtu kama Bashite kwanza ataambiwa piga kazi mfano mzuri tu naona polisi waliyo mpiga risasi Akwilina wameachiwa mchana kweupe hawana kesi ya kujibu
 
Mkuu kwenye uchaguzi wa 2015 chadema walishinda majimbo 34 swali LA kujiuliza,hayo majimbo 34 walishinda kwa time gani ya uchaguzi?
Tatizo kubwa LA upinzani wa Tanzania ni kupinga kila kitu wakati wananchi wanaona kitu serikali inafanya.
Hiyo moja lakini pili,viongozi wenu wanaohamia ccm wanazidi kuwaumbua kwa msimamp yenu ya kichama kwamba mbunge su diwani hawapaswi kuzungumza ns mawaziri au wakuu wa wilaya au mikoa au viongozi wa serikali,sasa unapoingia kwenye uchaguzi wananchi unawahaidi mini ikiwa hutakuwa na ushirikiano na watawala? Hapo mnapokosea.
kula like mkuu, kama wanaelewa watajirekebisha.
 
Kama kituo tu alichopiga yeye kura wamepata kura moja haoni chama kimepoteza mvuto?? Na inawezekana hata yeye amemchagua mgombea wa CCM.
mkuu. ana bahati. hata kupata hiyo moja. uvccm walidhamiria kuhakikisha chadema wanapata kura zisizopungua kumi kwa kila kituo.
 
Hao uliowataja hawajawahi kuingia kwenye system
Ndiyo hivyo tena serikali ya CCM ilielekeza jadho na damu ili kuwaingiza na wanaingia tu kwenye system ili juwa imprest wengine wa aina yao amepata Shonza!
 
Mpumbavu huyu

angeshinda ndo asingabadili tume kabisa

Kwa hili nakuunga mkono kwa asilimia 100. Lowassa ni mtu anayeamini kwenye utawala wa dhuluma na yeye ni mmoja wa waliokuwa wakihujumu tume huru ya uchaguzi inayoibeba ccm akidhani angekuwa ccm daima. Leo lile jini aliloshiriki kulifuga linamdhuru anajifanya kulipinga.
 
Maneno haya yalisemwa na mzee Lowassa mara baada ya uchaguzi mdogo wa ubunge Kinondoni ambapo mgombea wa chadema aligaragazwa vibaya na kijana wa CCM.

Lowassa aliwasihi Chadema wadai tume huru ya uchaguzi kabla ya kushiriki chaguzi zitakazofuata lakini ni Tundu Lisu pekee aliyeupokea ushauri wa mzee Lowassa kwa mikono miwili wengine walikuwa wanawaza ruzuku tu.

Lowassa kuendelea kubaki Chadema ilikuwa ni kupoteza muda kwani kilichompeleka pale siyo itikadi bali fursa ya kugombea urais.

Maendeleo hayana vyama!
 
Back
Top Bottom