Edward Lowassa na Maalim Seif kuhudhuria mechi ya mpira baina ya Simba na Yanga

Lowasa kawakosea nini jamani..inamaana hana uhuru wa kwenda kuangalia mpira...?? Punguzeni kuogopa jamani
 
Ukiona hivyo ndo ujue tumeanza kukomaa kisiasa. Watu wakizuia mlangoni wewe unachungulia dirishani. Kenya ktk hili wako mbele sana. Shughuli yoyote ya inayovuta watu hata iwe msiba basi hapo politiki inapigwa vizuri. Siasa ni pamoja na branding na branding ni pamoja na kuwafanya watu wasikusahau. Walipo uwepo.
 
Lowassa na Malim Seif kuhudhuria Mechi baina Yanga na Simba.

Hatimae Lowassa na Malim Seif amekubali Ombi la Vijana wa CHADEMA la kumtaka kuhudhuria mechi ya Simba na Yanga, itakayochezwa Uwanja wa Taifa Tarehe 1/10/2016. Lowassa amekubali Ombi hilo na ataambatana na viongozi mbalimbali ambao ni Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa NCCR James Mbatia, pamoja na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu
Kwani vijana wa chadema ndio waandaaji wa mechi hiyo?
 
Nilipanga nisiende uwanjani, lakini baada ya kupata taarifa hii, nabadilisha gia juu kwa juu... Ma prezidaaaa atakua uwanjani.
 
wataundiwa zengwe,siku kadhaa kabla watakamatwa kwasababu uchwara,na kupangiwa tarehe moja iwe siku ya aidha kwenda mahakamani/kuripoti kituo cha polisi..
 
Lowasa kawakosea nini jamani..inamaana hana uhuru wa kwenda kuangalia mpira...?? Punguzeni kuogopa jamani
Kulikuwa na haja ya kitamgaza kuwa wataenda huko??
Huoni wanaweza geuza siki hiyo watu kuichukulia kama ya mikutano ya kisiasa kutokana na influence waliyonayo.
 
Back
Top Bottom