Edward Lowassa Mwaka 2015 ataingia Ikulu au Segerea?

Edward Lowassa Mwaka 2015 ataingia Ikulu au Segerea?

If happen,lowasa akatupwa nje mgawanyo utakuwa hivi, lowasa kwa chama atakachogombea atapata 40%, ukawa kama watafanikiwa kuungana watapata 28%(ila wataongeza wabunge wengi) ccm itapata 30% itakuwa na wabunge sawa na ukawa kama watafanikiwa kuwa pamoja. So what formation of transitional gvt.lowasa president. Let wait and see, we like him bt they don. Silipwi my opinion
 
Kama kuna mtu atawaambia nyerere alisema, nimeangalia hizo clips ni uongo mtupu. Wapuuzeni msiwasikilie hao kwani wamejawa na chuki binafsi. Wala syo uzalendo walionao katika nchi hii ni maslahi yao tu.,mungu awabariki mungu ambariki ukipewa nafasi uwasaidie tanzania, wengine huwapi hata hela lakini wanakupigia debe, huo siyo ushabiki bali uaminifu walionao kwako
 
Lowassa hawezi kuwa raisi wa tanzania huyu ni fisadi mkubwa hafai siku zote ukiona mtu anamsifia mtu mchafu basi ujue naye ni mchafu zaidi ccm hakuna aliye msafi wote ni wachafu mafisadi wakubwa..ccm ni janga la taifa
 
Nilikusheshimu sana ulipoleta mada hii lakini kumbe ni wale wale wapuuzi wa wama, napenda utambue hivi, kama CCM itataka kuanguka 2015 ithubutu kutuletea mgombea mwingine tofauti na LOWASA
Endeleeni kujipa moyo sana ccm wote ni wachafu na mafisadi wakubwa hakuna mwenye sifa za kugombea uraisi 2015 ccm ni janga la taifa
 
Ndugu zangu, leo naomba tuweSERIOUS na tutoe maoni ya maana katika mustakabali wa taifa letu. Kwakuwa 2015inakaribia na kwakuwa hata CHADEMA wanajua fika Rais atatoka CCM na kwakuwa tukimchagua Rais feki ndio itakuwa imekulakwetu kwani atakaa madarakani hadi 2025, hivyo basi tuchangie maoni kuhusukufaaau kutofaa kwa ndugu yetu EDWARD NGOYAI LOWASSA aka LAIGHWANAN.Kuna makundi mawili yanayomuhusuhuyu bwana. Moja ni la wale wanaomuunga mkono kwa asilimia 100. SABABU ZAO KUMI za kumuunga mkono na kuona anafaa kwendaIKULU ni hizi
  1. Nimchapakazi hodari
  2. Sio mwoga wala mnafiki
  3. Nimwepesi kutoa maamuzi magumu sio kama viongozi wengi wa CCM
  4. Nimbunifu wa mikakati, mpenda maendelea na ndio maana jimbo lake la Mondulilimepiga hatua kubwa kimaendeleo
  5. Nimwepesi kutafuta njia mbadala mambo yanapokuwa magumu
  6. Anafikra mpya za kisasa, ni mkali sio mtu wa kuchekacheka
  7. Anathaminisana umuhimu wa vijana na elimu
  8. Nimtu wa watu na anafanana sana na kipenzi chetu EDWARD SOKOINE
  9. Siomtu wa kukaa ofisini bali huzungukia kwa wananchi kujua na kutatua matatizo yao
  10. Anauzoefu mkubwa wa masuala ya uongozi na masuala ya Kimataifa
Kundi la pili ni lile la watuwasiomuunga mkono ambao wanaona na kuamini kwa asilimia 100 kwamba LOWASSAhafai kwenda Ikulu bali anapaswa mwaka 2015 kwenda SEGEREA. Hoja zao KUMI zakuwa na mtazamo huo ni hizi hapa:
  1. NiFisadi numero uno hapa TZ
  2. Nimla rushwa mkubwa
  3. Nimtu mwenye kuamini ili uwe kiongozi lazma uhonge wapiga kura
  4. Nimtu anaeamini ili yeye mambo yake yawe mazuri lazma ihonge ili wapinzani wakewasipate kura za kutosha kama alivyofanya kwa Sumaye (Hanang) na akafanikiwa ambapoMARY NAGU alishinda na kama alivyotumia mabilioni kwa MEMBE-NEC Dodoma iliMEMBE asipite lakini familia ya JK na wengine wakamzidi LOWASA ujanja.
  5. Nimpiga dili mkubwa-akiwa kitengo cha mafaa kwa PM alipiga dili za kufa mtu,akiwa AICC alifanya hivyohivyo, akiwa Waziri wa Ardhi miaka ya 1990s aliwauziawahindi viwanja kwa mamilioni ya fedha na kutajirika vibaya sana. Kwa kugunduliwaoil and gas, jamaa akiingia MAGOGONI atapiga dili za kufa mtu.
  6. LOWASSAhafuati Rule of Law ambapo anaweza kuwafukuza wateuliwa wa Rais katika mikutanoya hadhala
  7. Nimtu mwenye chuki kali kwa wote wanaepingana nae na ana visasi sana
  8. Hapendikukosolewa
  9. Nidikteta
  10. Anauchu mkubwa wa kwenda Ikulu ambapo nimahala patakatifu lakini yeye na genge la marafiki zake "FRIENDS OF LOWASSA" wanatakakwenda kupageuza IKULU kuwa mahala pabiashara na kupiga madili.Haya ni maoniambayo kwa kipindi kirefu sasa yamekuwa yakisemwa na makundi haya mawili.ANGALIZO- Inawezekana mambo yote hapo juu sio ya kweli hivyo nawatakeni GREATTHINKERS mtoe mawazo yenu KWA HOJA NASIO KUTOA MAPOVU KAMA MMEKUNYWA OMO.JE EDWARD NGOYAI LOWASSA aka LAIGHWANAN ANAPASWAKWENDA IKULU AU SEGEREA?THE BALL IS INYOUR COURT.

ataenda segerea
 
Endeleeni kujipa moyo sana ccm wote ni wachafu na mafisadi wakubwa hakuna mwenye sifa za kugombea uraisi 2015 ccm ni janga la taifa

Kajengeni kwanza office zenu kila kona ya tz ndo mje kupambana na CCM, huo ni ushauri wa bure tu niliokupa bila kusahau LOWASA ndio rais wa tz 2015
 
jinsi unavyomtetea bila shaka jamaa atakuwa anakufumua, sio hivi tu.
Lowasa ni mwizi, tunahitaji mtanzania muadilifu kuwatumikia wananchi.
mtu ambaye hata muasisi wa taifa hili alimkataa sisi ni akina nani hasa mpaka tumkubali huyu mwizi?



Hakuna wa kumzuia lowasa kuingia ikulu mwakani

Rais ajae wa Tanzania ni Lowasa.

Hakuna mwanasiasa mwenye maono ya uongozi zaidi ya lowasa

Lowasa mwakani anaenda ikulu. Watanzqnia tunamuhitaji sana

we mwenyewe huna hoja
 
Kuna ambayo hukuyaweka ktk uwezo wake wala udhaifu wake maana unasukumwa na upenzi. Hayo ndio kipimo na sisi tunaoyasema hatusukumwi na upenzi wala chuki bali Tz yetu. Ndio maana hatuna chama cha kupigia upatu kama ww ulivyojiaminisha kuwa rais atatoka ccm. Gosh! Katika mimi tangu nianze kumufahamu sijamsikia akimuong'elea mnyonge. Hajitaabanishi na maskini. Maskini wengi wa tz ni wakulima na wanaishi vijijini. Lowasa hajajihangaisha naojapo ndio 85% ya wtz. Kujali kilimo chao hadi masoko ya mazao hakuna. Maisha yao kielimu, afya, maji nk hakuna. Ukijua hana lolote kwao ww mufuatilie toka amekuwa bungeni hutamusikia akiweka bidii kutumia influence yake kuweka sheria, kanuni na mipango inayohusu maskini kama mfumo wa kodi, elimu hasa mikopo kwa elimu ya juu, jinsi ya mkulima kupata matibabu rahisi na bora, nk. Tunakubariana inawezekana kutokea akawa dikteta wakutupwa. Kama hachangii bungeni hapendi uamuzi wa pamoja. Pindi akiwa rais anaweza akapangua kwa kujipendekeza yy na marafiki zake akina Rostam,nk. Hafai
 
Lowassa wako ni kweli anaamini pesa ndio inatengeneza urais na hilo sio la yy tu ni la wengi wa chama cha ccm. Dr. Slaa naamini aliipelekesha puta ccm 2010 kwa alivyokuwa akiwaaminisha wengi wakulima vijijini kuwa atawajali. Aliwaaminisha kuwa watawezeshwa kujenga nyumba bora badala ya hizi wanamoishi kwa kwa kurekebisha mfumo wa kodi vifaa vya ujenzi vikapungua bei kwa 50% kuwezesha kipato cha chini kumudu huku wakifutia gharama za shule. Hili lilipandisha chati ya bdm. Hamna liwezalo kukonga nyoyo za watu walio wengi kama hili ambapo cdm ninategemea wataliongezea nguvu ktk manifesto yao ya 2015, Lowassa kwa kuhonga kutaweza pambana na muamko wa kampeini ya muamsho kama hiyo? Je Lowassa anajipambanuaje na hili la katiba mpya? Watakao jielekeza kwa Warioba watakoga nyoyo za wengi ktk uchaguzi wa 2015 na uendelezaji wake baada ya uchaguzi itakuwa ni trufu ktk kampaini. Kwa hapa nawapa tano UKAWA. Tunajua kunakuwa kuna nguvu za dola na uwezo wa shilingi ambalo ww unaonekana kulipa nafasi, lakini nachelea.
 
Mwisho unashaka na wanaomuona Lowassa kutokuwa mwaminifu. Enzi za Kambarage Nyerere kulikuwa na ushushu uliojua kazi yake. Kila mtu alijulikana kila alichokuwa akikifanya hasa watumishi. Hata uende baa kesho yake ungetajiwa idadi ya bia ulinunua baa. Ufisadi wa Lowassa kama Nyerere alivyousema hadi leo Lowassa hajawahi kukana. Hivi leo Lowassa anazungumuzia kutokuwepo ajira kakini alikuwa jikoni wakati wa mipango ya awali ya nchi hii, wameharibu akiwepo, sifa za uthubutu, kuwa na maamuzi, nk, vinatoka wapi? Au vinaundwa kwa sababu ya pesa yake? Kulikuwepo mipango kwa kukuza kilimo sambamba viwanda ili kumaliza tatizo la ajira na kuongezea kilimo thamani. Vitu kama NMC, GAPEY, TANZ. PACKERS, VIWANDA VYA NGUO NA NYUZI, vimepotea akiwa ktk nafasi ya ushawishi. Sasa ndipo anakuja na taralira za kusema tatizo la ajira ni bomu linasubiri kupasuka! Rostam moja ya utajiri wake ni kugawiwa viwanda vile. Kwa bei aliyokuwa akinunua ilikuwa ni kugawiwa. Ilikuwa suala la muachie rafiki tutajuana huko ya safari. Ni mashoga
 
Huyu fisadi Lowassa miezi michache iliyopita alipokuwa anagawa mamilioni ya pesa katika nyumba za ibada makanisa na misikiti aliulizwa hizo pesa amezipata wapi? Akadai ni pesa za marafiki zake, akaombwa atoe list ya majina hdharani ya hao marafiki zake na kiasi ambacho kila rafiki ametoa akang'aa macho mpaka leo list hiyo haijatoa.

Juzi juzi alidai utajiri wake ni ng'ombe 800 miaka micahche ya nyuma aliweka mtandaoni marejesho ya mkopo wa shilini 450 ambazo fisadi Lowassa aliwakopesha Wasomali walioingia nchini kama wawekezaji katika sekta ya nyumba za kuishi. Cha kustaajabisha pamoja na kuweka documents hizo mtandaoni lakini hakuweka documents za kuonyesha Wasomali hao wakipokea mkopo huo wa shilingi 450 million toka kwa fisadi Lowassa. Kama aliweka documents za marejesho mtandaoni kipi kinamshinda kuweka documents hizo kuonyesha Wasomali hao kupokea mkopo huo wa shilingi 450 million?

Huyu ni fisadi ambaye hastahili kuingia Ikulu, Watanzania tumechoka Ikulu kuendelea kufanywa mahali haramu na hawa mafisadi ambao hawana sifa ya uongozi. Huyu fisadi pamoja na kushika nyadhifa mbali mbali za uongozi Serikalini tangu awamu ya kwanza hadi ya nne hana sifa hata moja ya kuonyesha kwamba anastahili kuiongoza Tanzania.

Like 10000
 
Lowassa ni Mashine ya kazi.
Hatuitaji viongozi wanao lialia

Kama ni suala la mashine ya kazi, Lowassa hamfikii Magufuli hata robo kwa utendaji kazi. Kwa nini Magufuli hapigiwi kampeni kuwa Rais? Jibu rahisi, kwa kuwa hajatoa rushwa kama anavyotoa EL.
 
jinsi unavyomtetea bila shaka jamaa atakuwa anakufumua, sio hivi tu.
Lowasa ni mwizi, tunahitaji mtanzania muadilifu kuwatumikia wananchi.
mtu ambaye hata muasisi wa taifa hili alimkataa sisi ni akina nani hasa mpaka tumkubali huyu mwizi?

Huyu Lowassa 2015 ni kumuweka Segerea tu nchi hii itulie na itawalike vizuri. Kesi iko wazi, kujilimbikizia mali kwa kutumia ofisi za umma. Hosea atolewe pale TAKUKURU awekwe mtu shupavu ampeleke mahakamani huyu Mamvi anyamazishwe once and for all.
 
Back
Top Bottom