Ikulu siyo chaka la majambazi na mafisadi.asilimia kubwa ya watz ni masikini na wanahitaji mtu mwenye uchungu na upeo wa kuliondoa kundi hili kubwa kutoka katika lindi la umaskini.huyo Lowasa nimjuaye mimi leo hii awe rais wa nchi hii maskini tutakimbilia wapi? si ndio utakuwa muda wa akina karamagi,Rostam na marafiki zao kugawana rasilimali za nchi hii.
Lowasa ameonyesha tabia ya wizi na ufisadi tangu akiwa kijana wakati akiwa kitengo cha maafa.
Nashangaa sana watu wanaomtetea Lowasa,sijui wamepatwa na nini au wana maslahi binafsi.kwa akili ya kawaida Lowas amekuwa kiongozi wa nchii kwa miongo kadhaa utajiri alionao ni kodi za watz....Najua hoja hii ya utajiri wa Lowasa kutokana na kodi za walalahoi itapingwa lakini huo ndo ukweli.kuna wasukuma wangapi na wamasai wanamiliki maelfu ya ng'ombe lakini hawajapata kuwa matajiri kama huyu mwizi Lowasa.
Nawasihi watz tuache ushabiki wa kikanda na kichma tuchague mtu sahihi kwa maslahi ya wengi na hasa tabaka la chini.
Wasalam