Edward Lowassa: Chui wa makaratasi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Edward Lowassa: Chui wa makaratasi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by frank m, Mar 16, 2012.

 1. f

  frank m Member

  #1
  Mar 16, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waziri mkuu aliyelazimishwa kujiuzulu kwa kashfa ya Richmond na mbunge wa Monduli Edward Ngoyai Lowassa si chochote kama anavyotaka tuamini. Ni chui wa wakaratasi, ni mbwa anayebweka sana lakini hakika hawezi kung'ata. Ni mwigizaji by profession na maisha yake yote ya kisiasa amekuwa anaigiza na kuna watu wa kutosha wanaoamini maigizo haya ni halisia! Of course alisoma degree ya "Theater Art"

  Anajua fika hawezi kuwa rais wa nchi hii, afya yake haimruhusu na hawezi kuteuliwa na chama chake licha ya ukweli kwamba hata akiteuliwa uwezekano wa chama chake kushinda Urais kwa wapiga kura na mwamko utakaokuwepo 2015 ni mdogo na yeye anafahamu hilo. Swali: Kwanini anajifanya urais anautaka wakati anajua kamwe hili haliwezekani? Ili kuendelea kuwa relevant lazima atuaminishe anaweza kuwa raisi wa nchi hii siku moja, hicho kinafanya wajinga kadhaa wambabaikie na anakusudia kuliendeleza hilo kwa kipindi. Siku akisema hautaki uraisi he is finished!

  Nikiangalia juzi alivyokuwa akihangaika kupenyeza pesa ya kuhonga wajumbe Arumeru Mashariki na namna ambavyo alilazimika kutumia watu wa Monduli zaidi nabaini hana mtandao mkubwa kama nilivyodhani awali. Ndio ana watu wake ndani ya CCM na serikalini aliowaweka katika kipindi chake kifupi cha uwaziri mkuu lakini nje ya hapo he is almost nothin! Nafahamu juhudi zake kuwanunua baadhi wa watu CDM lakini hazitafanya kazi. Nje ya CCM na serikalini hana lwake na ataendele akuanguakia pua kama alivyoangukia pua alipojaribu kumweka Batilda Arusha mjini.

  Karibu Arumeru Mashariki Edward!
   
 2. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Mnaweweseka kusikia mzee mzima anaingia Arumeru kwa vishindo!
   
 3. f

  frank m Member

  #3
  Mar 16, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama tulivyoweweseka wakati anambeba Bi Batilda! Mshauri mzee apumzike tu kwa sasa maana siasa yataka walau macho yote mawili wafanye kazi ipasavyo.
   
 4. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Haya ni matapishi ya mtu aliyekunywa chan'gaa bila kula.
   
 5. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Bear in your mind that, alichokibariki Mungu mwanadamu hawezi kukilaani.
   
 6. f

  frank m Member

  #6
  Mar 16, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  mungu wako anabariki uporaji wa maskini, hakika si MUNGU wangu, hilo MUNGU wangu hawezi kulibariki kamwe!
   
 7. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Chui wa makaratasi ndio nini
   
 8. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #8
  Mar 16, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  paper tiger
   
 9. Young Tanzanian

  Young Tanzanian JF-Expert Member

  #9
  Mar 16, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,740
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nazan Frank M wewe ni mmoja wa wale waliotumwa kupima maji ya bahari na rula mm ni mwana arumeru mashariki unadanganya umma wambie waliokutuma kama Lowasa hawawezi wasubiri 2015..elewa chama si CCM tu..
  Wambioe eti akna M na S bado mapema wasiwe na papara...2015 mbivu na mbichi itajulikana..kuna viwili Lowasa kuwa Rais au CCM kuvunjika ...karbu arumeru mashariki..
   
 10. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #10
  Mar 16, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hivi kumbe ulibwia chan'gaa nyingi sana. Naona unaendelea kuitapika tu.
   
 11. m

  mharakati JF-Expert Member

  #11
  Mar 16, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Mwanasiasa yeyote anataka kusikika na kua relevant kwa sababu inampa nguvu mbele ya maadui (wa kweli na wengi wa kuhisi).

  Kingine ukiwa relevant unaweza usipate unachotaka lakini ukawa sehemu ya wanaunda serikali ijayo na hivyo kuendelea kujilinda...

  EL anajua hawezi kua rais ila anataka kua relevant machoni mwa watu na viongozi wengine ili afanikishe niliyoyataja hapo juu.
   
 12. m

  mharakati JF-Expert Member

  #12
  Mar 16, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Lowassa hawezi kuvunja chama sana sana atakimbia na wachafu wenzake wawili watatu toka CCM na hii itakua ndiyo a ticket to political mortuary.

  bwana dogo karibu Tanganyika
   
 13. F

  FOEL Senior Member

  #13
  Mar 16, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 141
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kaka ungeweka na PICHA kaka, unajua hizi zama za sayansi na teknohama ni vizuri habari kama hii ikaambatana na PICHA.
   
 14. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #14
  Mar 16, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  wezi wamekuwa wanasiasa
  na wanasiasa wamekuwa wezi...........

  mungu ibariki Tanzania........
   
 15. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #15
  Mar 16, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  siasa za tanzania = wizi, ubazazi, ufisadi, uuaji, utapeli, vitisho, visasi, njaa kali nk.
   
 16. Foundation

  Foundation JF-Expert Member

  #16
  Mar 16, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,458
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  Mungu wa YAKOBO, ISAKA NA IBRAHIMU? Au unazungumzia mungu? Fafanua mkuu
   
 17. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #17
  Mar 16, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,870
  Likes Received: 6,610
  Trophy Points: 280
  Lowassa hatafika mbali...
   
 18. S

  Sanare S Member

  #18
  Mar 16, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kimsingi Mh Lowasa yupo sawa na anafaa licha ya katiba ya jamhuri ya muungano kumruhusu, tumechoka na viongozi wa kutengenezewa, mwacheni Mh Edward na kama kuna mwingine ajitokeze mapema ili watz wawe na muda wa kutosha wa kuwapima, kama wewe umampinga Lowasa watanzania wenzako wanamkubali na huo mchezo uliochezwa na akina Mwakiembe na Sita watanzania hawdanganyiki tena. Usibaki tuu kumpinga bali tuambie huyo unaedhani anafaa ili watz wawe na fursa ya kuchagua. Wana JF tuwe makini sana na hawa wanaotaka kukandamiza demokrasia ya mtu, kila mtu ana haki isipokua asivunje sheria.
   
 19. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #19
  Mar 16, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Sheikh Yahya at work.
   
 20. m

  mharakati JF-Expert Member

  #20
  Mar 16, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  nyie wameru bwana hatujasema hana haki, la hasha haki anayo mkuu huyu, ila dola ya CCM isimpitishe kwa sababu ya siasa zake za chuki, ubinafsi, ufisadi, makundi, kupenda mno madaraka, kurithishana na kubinafsisha vyeo, na umafia mwingine wa kudhuru wenzake n.k Tanzania haitaji mtu wa aina hii hata kidogo..tunaowadhani watajitokeza tu muda ukifika hawana kwani hawana haja ya kusafishwa" kama mkuu wenu huyu
   
Loading...