Edward Charles Manyama, kacheze mpira

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
3,189
8,217
IMG_0944.jpg

Hivi ulipata kumsikia mchezaji aliyeitwa Michael Paul "Naylon"? Umeambiwa nini kuhusu yeye? Kama umesikia ama hujasikia lolote kuhusu yeye chukua hii.

Michael Paul alikua fundi wa mpira hasa akiitumikia Biashara ya Shinyanga 1991/92, Simba ilihitaji huduma yake katika nafasi ya kiungo kipindi hicho Simba ina Hussein Marsha, Ramadhani Lenny, Michael, George Lucas "Gaza".

Siku ya kwanza Michael Paul anaripoti mazoezini pale Simba Sports aliulizwa kama anaweza kupata namba mbele ya mafundi hao? Alijibu, "hayo ni majina tu, miguu yangu ndio itaongea! Kilichofuata baada ya hadithi hiyo wanajua wale walioapata kumshuhudia Michael Paul.

Achana na hilo turejee kwa Christopher Alex Massawe, huyu alionekana ni wa kawaida mno wakati akitoka Reli ya Morogoro kuja Simba, hata ujio wake National Team ilionekana kama ni mbeleko ya kocha wake aliyekua akimnoa Reli na Taifa Stars pia.

Simba ya kipindi hicho ilikua na kina Matola, Shekhan Rashid, Shaaban Kisiga, Primus Kasonso n.k. Christopher Alex alipigania namba kama hujui nini alifanya nyanyua simu yako mpigie kocha msaidizi wa Simba.

Jambo moja tu wengi hatulijui kuhusu Edward Manyama, pamoja na ubora wa Tshabalala bado Edward Manyama anaweza ku-offer vitu vingi ndani ya Uwanja na si lazima acheze fullback wa kushoto.

Kile ambacho ameshindwa kukifanya Gadiel Michael nina imani Manyama atakifanya kwenye position yoyote ile Mwalimu atakapomhitaji atumikie, hasa ukizingatia Didier Gomes ndiye aliyemhitaji Manyama.

Nirejee tena kwako Charles Manyama, achana na waganga wa njozi, kaza buti ukafanye kazi Simba SC kwa jukumu lolote lile atakalokupa Mtaalam Didier Gomes, hii ndio nchi yenye binadamu wanaojua kesho za wenzao kesho zao zinawashinda!!

Simba ni timu kubwa na siku zote timu kubwa huchukua wachezaji wakubwa nawe ni mmoja wapo, umeonyesha hilo ukiwa Namungo, Ruvu Shooting, Taifa Stars na sasa Simba.

Ninachoamini wewe ni another Erasto Edward Nyoni, miguu yako haitatariki inapoona mpira, una uwezo wa kupiga mipira ya mbali, unaweza kupiga vichwa defensive and offensive, una kimo sahihi, unanyumbulika, ball brain ya uhakika walitaka ukacheze wapi?!
Only SSC!
 
Labda afuate hela tu ila si mpira, Gadiel Michael tu kashindwa kucheza sembuse mameat.........
 
Huyu Manyama alinishangaza sana kwenye mechi ya Namungo Vs Yanga pale alipowaginga hat trick. Kabla ya hapo sikuwa kumjua.

Vv
 
Back
Top Bottom