Edmund Mndolwa: Awamu ya Tano tulilazimishwa kukalia misumari

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,650
218,130
Akizungumza kwenye kikao cha Wakuu wa Shule za Wazazi za Chama cha Mapinduzi, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Dk Edmund Mndolwa, amedai kwamba kwenye awamu iliyopita walilazimishwa kukalia misumali na wala hakukuwa na hata chembe ya Utawala bora.

Kikao hicho kimeitishwa na Katibu Mkuu wa CCM, ambaye pia alikuwa Mgeni Rasmi.

Chanzo: MwanaHalisi

Swali: Je, wale watetea Legacy bado wangalipo?
 
Hawa watu hawana kabisa hoja za maendeleo?

Kwamba kumsema alie kufa ndo kutapunguza ugumu wa maisha ya waTZ?

Tutegemee kuona Samia akitukanwa baada ya utawala wake.

Wanasiasa wa namna ya Mndolwa hawafai hata kiti cha ujumbe wa nyumba kumi maana hawana vision ya kuangalia mbele badala yake wanafanya mambo yasiyo na tija.
 
Hawa wanaolalamika ni viongozi wa juu wa ccm , Siku Mzee Mangula akipata ujasiri wa kuongea nchi itatikisika

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
Upuuzi mtupu, hata Mangula akiongea atakuwa anafanya siasa tu, kama vile tu pro-Chadema unavyoshupalia hizi siasa hapa za majitaka huku mtaani hakuna umeme mchana ni siku ya tano mfululizo sasa, wananchi tunawachora tu na siasa zenu ipo siku ya Gambia kuzidi Srilanka yatawafika tu.
 
Back
Top Bottom