Edibily Jonasi Lunyamila Vs Marcus Rashford

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
EDIBILY JONAS LUNYAMILA RASHFORD ALIEZALIWA SHINYANGA

‌Rashfoooord ........he scored his dream goal he was looking for and maybe he will never ever forget .......ilikuwa ni saut ya mtangazaji wa mchezo wa utd dhidi ya midjtland Uefa Europa League 2016, akitangaza goli la Kwanza la Rashford akiwa na Jezi ya utd wazungu huita debut goal akiwa na umri wa miaka 18 tu , siku tatu mbele anafunga tena kwenye mechi yake ya Kwanza EPL dhidi ya arsenal baada ya mechi na arsenal, Rashford alirudi darasani kumalilizia mitihani yake . Naam huu ulikua Mwanzo wa Rashford kutambulika kwenye Ulimwengu wa mpira wa miguu na yaliyofatia kila mpenzi wa mpira wa miguu ni shahidi

‌fast flash back
‌Mwaka 1992 kwenye viunga vya shule ya sekondari Buhangija Shinyanga huko tajiri Abas Gulamali alikuwa amekaa Ndani ya gari yake Aina ya shangingi akimsubiri kijana Mdogo amalize mitihani aweze kuondoka nae kuelekea Mwanza kujiunga na team ya taifa (Kaka kuona) Abas alisafiri kilometa nyingi kutoka Dar then kilometa nyingine nyingi zilikuwa zinamsubiri kuelekea Mwanza, naam Edibily Jonas Lunyamila alifanya jamaa atembee kilometa zote hizo, msukuma aliezaliwa na miguu ya dhahabu na ubongo wenye kufanya kazi haraka akiwa na mpira miguuni mwake Edibily alikuwa anasoma huku akiichezea klabu ya Biashara Shinyanga iliyokuwa ikishiriki ligi kuu(daraja la kwanza wakati huo). Hii ilikuja baada ya kutoka kuacha gumzo kwenye UMISETA 1992 iliyofanyika Zanzibar. Baada ya hapo Lunyamila alirudi shule kufanya mitihani.

Mwaka huo CECAFA Senior Challenge Cup ilifanyika Tanzania.
CECAFA kama wenye mashindano na FAT (siku hizi TFF) kama wenyeji walipanga kuwe na vituo viwili; Mwanza na Arusha.
Tanzania kama mwenyeji ilipewa nafasi ya team mbili; timu A ikaitwa Victoria, iliyokuwa kituo cha Mwanza na timu B ikaitwa Kakakuona ikapangiwa kituo cha Arusha.

Kocha wa Victoria, Paul West Gwivaha, alimtaka chipukizi Lunyamila kwenye timu yake hivyo mmoja wa wafadhili(Abbas Gulamali) alikwenda Shinyanga kumfuata kijana Lunyamila aling’aa na Victoria japo ilitolewa kwenye robo fainali kwa kipigo cha 2-1 kutoka kwa Zambia(KK 11) Bao pekee la Victoria lilifungwa na Lunyamila.

Safari ya Lunyamila iliendelea na mwaka huo huo akajiunga na Yanga ambayo 1993 aliisaidia kutwaa kombe la klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati huko Uganda mwaka 1996 huku akifunga bao la ushindi wa 2-1 mbele ya wenyeji SC Villa Jogoo. Lunyamila aliacha gumzo jijini Kampala na hata mabasi mengi yaliandikwa jina lake.

Lunyamila aligeuka kutoka kuwa kijana Mdogo Kule Shinyanga hadi kuwa shujaa aliyeimbwa sana na mashabiki uwanja WA taifa pale shamba la Bibi (siku hizi uwanja WA Uhuru) na kote nchini alipotia miguu akiwa na Uzi wake wa manjano Kwa kijani Uzi wa Dar Young Africans kabla ya kutimkia malindi ya Zanzibar na baadae akaja kumalizia mpira wake Kwa wapinzani wa jadi wa waajiri wake wa zamani Simba sports club.

Historia ya Lunya inashabihiana Sana na Ile ya Rashford ingawa mwisho wao ni tofauti kama mbingu na ardhi
mpira wetu umezungukwa na wajanja wengi ,wajanja wanaozima ndoto za vijana wengi Kwa ahadi zao tamu kama za wanasiasa wajanja ambao wanalipa bill zao Kwa jasho la watu wengine , wajanja wanaoishi Chini ya mwamvuli Kwa kujiita wadau wa Soka wakat nguvu kazi wanapigwa na jua wajanja ambao Kaka Yangu Dodi Mzee Wa Soka kijiweni pale Azam TV anawaitaga sungura wa mpira wetu

Aliwahi kuahidiwa nyumba ya kifahari pale Mikocheni, Gari ya kifahari ili atie saini kwenye moja klabu zetu penda na maisha yake yawe bora. Tatizo ahadi ilitolewa kupitia dirisha la gari. Kioo kilishushwa, akaitizama sura iliyomuahidi akakubali, gari ikayoyoma. Kesho inayokuja wanae na wajukuu watasimuliwa jinsi Tanzania ya miaka 90 ilivyoshuhudia Edibily Lunyamila aliyetapeliwa kipaji chake,. Bahati mbaya hakuna hata video zake nyingi, tutamkumbuka kwa maneno.

Nimewaza tu, watapatikana lini watu waliokuwa tayari kusimamia vipaji vya wanamichezo wetu kisasa na kitaaluma?
Kina Rashford wa shinyanga ,Mwanza Hadi Arusha na Mtwara zingatieni masomo yenu wanangu, huku kwenye Soka sungura bado wapo wapo Sana

Tchao
 
Nipangie na ile list ya Nzoisaba Tauzany iliyotwaa kombe Kampala kwa heshima ya akina Kizota, Fundi nk nk.
 
Kwa vipaji huwa vingi ila uchawi ni wapi umezaliwa, naimani kama samata angezaliwa england sasa hivi angekuwa anacheza hata everton jina lake likiwa kubwa, ila kuzaliwa huku kwetu safar inakuwa ndeefu mnooo!! Giroud angezaliwa chunya huko usikute angekuwa mkulima wa viazi tu.
 
Back
Top Bottom