Eddie Murphy 'Afariki Kwa Mara Nyingine' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eddie Murphy 'Afariki Kwa Mara Nyingine'

Discussion in 'Entertainment' started by MziziMkavu, Jul 26, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [TABLE="width: 491"]
  [TR="bgcolor: #E1E1E1"]
  [TD][​IMG]
  Eddie Murphy[/TD]
  [TD]Nyota wa filamu zenye kuvunja mbavu Eddie Murphy kwa mara nyingine tena

  amezushiwa kuwa amefariki dunia na habari kusambazwa na mtandao wa Twitter.[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Eddie Murphy kwa mara nyingine tena amezushiwa kufariki kama alivyozushiwa mwezi februari mwaka huu.

  Tovuti ya Global Associated News ilitoa taarifa kuwa Eddie Murphy amefariki dunia jana na habari hiyo iliingia kwenye mtandao wa Twitter na kusambaa duniani kama uyoga.

  Tovuti hiyo ilidai kuwa Eddie Murphy amefariki dunia kufuatia ajali kwenye michezo ya barafu nchini Uswizi.

  Tovuti hiyo hiyo ndiyo iliyozusha kifo cha Eddie Murphy mwezi februari mwaka huu kwa sababu hiyo hiyo ya ajali kwenye michezo ya kutereza kwenye barafu.

  Hata hivyo Eddie Murphy hayuko Uswizi kama ilivyodai tovuti hiyo na alionekana mwishoni mwa wiki nchini Marekani akiwa na mpenzi wake Rocsi Diaz kwenye shoo ya muziki ya ndugu wa Michael Jackson inayopewa jina la "Jackson Unity Tour".

  Msemaji wa Eddie Murphy alithibitisha kuwa habari za kufariki kwa Eddie Murphy ni za kizushi tu hazina ukweli wowote[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  Eddie Murphy 'Afariki Kwa Mara Nyingine'
   
Loading...