Ebu Jifanye mzani alafu soma hapa!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ebu Jifanye mzani alafu soma hapa!!!!!

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by kashengo, Sep 9, 2012.

 1. kashengo

  kashengo JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 2,648
  Likes Received: 464
  Trophy Points: 180
  [h=6]JIWEKE KWENYE NAFASI YA MZAZI HALAFU SOMA KIPANDE HIKI
  KIJANA mmoja aliweka kipande cha karatasi chenye ujumbe chumbani kwa madingi zake kikiwa na haya yafuatayo;

  Baba na mama ni matumaini yangu kuwa mtasoma ujumbe wangu huu kwenye karatasi niliyoiweka juu ya meza. Nawaombeni msishtuke maana ni mambo ya kawaida tu kwenye maisha tunayoishi.

  Najua mtaumia kwa vile bado nasoma na ndo kwanza nipo kidato cha kwanza. Napenda kuwajulisha kwamba sasa hivi mnapoisoma barua hii, sipo nyumbani, nimetoroka. Nimegundua nina uwezo wa kujitegemea kwa sababu mimi ni kijana mwenyewe umri wa miaka 14, najua zuri na baya.

  Tangu mwezi mmoja uliopita, nimekuwa na uhusiano na dada mmoja aliyeitwa Roda, mwenye umri wa miaka 37. Tunaishi pamoja kwenye chumba tulichopanga karibu na makaburi ya maji machafu.

  Nilipokuwa nyumbani sikuwa napata hela zaidi ya alfu moja moja mlizokuwa mkinipa. Ila sasa nimeanza kushika noti za shilingi elfu kumi kumi, nainjoi kwa kweli. Mchumba wangu ni mrembo, mama hafui dafu.

  Roda amenifundisha njia za kutafuta hela. Amenipa mchongo wa kuuza ‘unga’. Yeye kabobea kazi ya uuzaji viwanja hewa hapa jijini. Ni mtaalam kweli kweli. Aliniambia ana digrii ya kuzaliwa nayo. Sio siri, kama ni hela tu tunazichanga.

  Mchumba wangu ana bidii sana ya kufukuzia hela. Kila siku analala masaa matatu. Mteja akija tu atahakikisha anazunguka nae mtaani mpaka amchomoe mavumba.

  Msiwe na hofu, nipo salama kabisa na nimeamua kumwoa Roda maana ni kila kitu kwangu.
  Pia amenunua mchuma wa kubebea kuni na biashara inaenda vizuuuuri.

  Hivi karibuni Roda alitiwa mkononi kwa kosa la utapeli, nikaenda kumwekea dhamana na sasa yuko nje. Juzi aliniambia ili kesi ife inabidi nifanye juu chini nimkabidhi hati ya nyumba mliyojenga, hilo nimetimiza jana.

  Kwa kuwa nimekufa na mahaba ya mchumba wangu, inabidi nimridhishe kila kitu. Huwa nafanya naye mazoezi ya viungo, namchomolea hela toka kwenye akaunti ya baba na tukialikwa harusini huwa ananiambia nitumie suti za baba kisirisiri. Si mnajua tena unapopenda unakuwa huambiliki. Sio inakuwa ndio, ndio inakuwa sio.

  Tumepanga tutawatembelea baada ya miaka 10. Natumaini muda huo ukifika tutakuwa na watoto wanne hivi. Tutawaleta wajukuu mkakae nao kwa sababu Roda anasema, hatoweza kulea watoto. Wazazi wangu sina la kuongeza, kwaherini. Mungu akipenda tutaonana.

  Baba na mama, mimi nipo chumbani kwangu. Mnachokisoma ni home work. Mwalimu wa kiswahili ametupa leo, katuambia tutunge hadithi fupi. Naomba muipitie muone kama ina makosa ili Jumatatu niipeleke shule.


  [/h]
   
 2. Chimbuvu

  Chimbuvu JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 4,403
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 145
  Hahahahahh hahahhaahhaahhaha
   
 3. Achahasira

  Achahasira JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nilijua unanipotezea muda lkn ni nzuri
   
 4. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #4
  Sep 9, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,155
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Imewahi kuja humu, lakini asante kwa kutukumbusha mkuu
   
 5. deni

  deni Senior Member

  #5
  Sep 10, 2012
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 182
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Aghh inaboaa...
   
 6. JJB

  JJB JF-Expert Member

  #6
  Sep 10, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 336
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Copy+Paste
  try again later
   
 7. AKILImuchknow

  AKILImuchknow JF-Expert Member

  #7
  Sep 10, 2012
  Joined: Sep 3, 2012
  Messages: 216
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Duh!.hyo kabla cjamaliz kuisom ntakua nshazimia.
   
 8. D

  DOTTO LAIZER Member

  #8
  Sep 10, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I cud die...............
   
 9. conveter

  conveter Senior Member

  #9
  Sep 10, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 119
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Presha ingepanda kabla sijamaliza kuisoma.
   
 10. MatikaC

  MatikaC JF-Expert Member

  #10
  Sep 10, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,200
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  siyo kwangu
   
 11. MatikaC

  MatikaC JF-Expert Member

  #11
  Sep 10, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,200
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  kwani ukimpa credits utakufa?
   
 12. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #12
  Sep 10, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Du hyo homework si anaweza akawaua wazazi hata kabla ya kuimaliza story nzimaaaa!!!
   
 13. a

  azizi daudi Member

  #13
  Sep 11, 2012
  Joined: Sep 5, 2012
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Ha ha ha ha ha!!nno maaa.
   
 14. Simba Mkali

  Simba Mkali JF-Expert Member

  #14
  Sep 11, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 591
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Kwa kweli ni nzuri sana, mi sikuwahi kuiona before
   
 15. Rjohn

  Rjohn JF-Expert Member

  #15
  Sep 11, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 599
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  very interesting!
   
 16. a

  alph Member

  #16
  Sep 12, 2012
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Inarusha roho
   
 17. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #17
  Sep 12, 2012
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  kabla hujamaluzi ni hoi hosp
   
 18. k

  kasiasa Member

  #18
  Sep 12, 2012
  Joined: Mar 15, 2012
  Messages: 13
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  duuuuuuuu! Mzee hafiki kwenye kipengele cha mwsho cku mingi kashazima..
   
 19. Wizzo

  Wizzo JF-Expert Member

  #19
  Sep 12, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  duh isee,chukua like zangu za kutosha,u made ma day
   
 20. 2k Genius

  2k Genius Member

  #20
  Sep 12, 2012
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  ni poa...ila kama we unasema imekopiwa c lazima u comment unaweza chuna tu bila kucomment maana c lazima
   
Loading...