CottonEyeJoe
JF-Expert Member
- Jan 8, 2008
- 331
- 73
...wewe acha bandika bandua form just one code tax ukafikiri thats all for gaming taxes,zipo kibao ukiangalia at the end of the day its almost 70% ya income inaishia as taxes,kwa akili yako payroll tax ni kubwa kuliko gaming tax...na repo man wanakuja kuchukua gari yao sio kitu kingine lakini easy finance wanakuja kuchukua gari/nyumba yako(tofauti ni kubwa sana hapo)...nakuambia tena mikopo kama hii huwezi kumfanya chochote mtu kwa nchi kama States na huna cover yeyote kisheria wateja wako wakishindwa kulipa na hizi loans zimejaa sehemu za watu maskini wasioelewa kitu.
...Kivipi?? Toa maelezo yaliyonyooka tuthibitishe naweza kuwasiliana na Isaack Kassanga CEO wa Easy Finance tujue ukweli sio kuleta udaku hapa!!!ndugu zanguni, majambazi wako wa aina nyingi, easy finance ni kampuni la wezi, kaeni chonjo.
Mtoto akililia wembe mpe, ila ujumbe ndio huo, nendeni mkakope... Sikio la kufa halisikii dawa.
Hawa jamaa, wangekuwa nchi za kiarabu wangekuwa washanyongwa, walio jaribu wote watakuwa na maelezo mazuri, sio watu hata kidogo, ni majambazi walio jihalalisha, ipo siku itatokea, jaribu kwani asie sikia la mkuu huvunjika guu.
Ni wapigaji wa watanzania wenzao. Wanasaidia kuendeleza umasikini miongoni wa watu, fikra zao za udanganyifu zimezidi mawazo ya watu wasio na hatia wenye nia ya kujiendeleza.
Kuendelea na biashara ya wizi kama wanayoifanya nafikiri kutakuwa na nguvu zagiza wanatumia kuificha serikali.
Epukeni na hili jambazi, walio jaribu na wakakaa kimya pengine wengi wao watakuwa wamejinyonga.
Bora mafisadi wa EPA mia mbili kuliko hili moja.
Jambazi hili jamani msijaribu!
kero,
Naomba jaribu kutoa maelezo juu ya wizi ufanywao na Easy Finance kwa mapana kuwasaidia wana Jamii wengine wajue namna gani wanaweza kuukwepa wizi huo. Usiandike kwa kuwatisha ati 'sikio la kufa halisikii dawa' kwani huo si msaada kwao. Muhimu ni wewe kueleza namna wafanyavyo wizi wao na inaweza kuwasaidia wengi kung'amua kuwa malalamiko haya yana ukweli kwa kiwango gani.
Tafadhali mkuu
Nakuunga mkono kabisa Invisible.
Kwa kuangalia mabandiko ya hivi karibuni, kuna shutuma kadhaa zinarushwa kwa watu/taasisi bila takwimu zozote na hii inafanya JF ionekane kama mahali pa kutolea hasira kwa wale wenye chuki binafsi.Hii imepelekea kuwepo na mabishano makali baina ya wana JF hadi kuleta kero wakati mwingine.Slowly credibility ya hii forum itaanza kutiliwa mashaka.
Inabidi turekebishe hii hali.
Mkuu CottonEyeJoe,Tunaomba tujue ni njia gani Easy Finance ni matapeli na wanaliza watu lasivyo hii ipelekwe kwenye udaku....
It is very complicated scenario when it come to explain may be one day I will ask God to substantiate. Good news is for those who can just believe, Bad is for those who can just ignore.