Easter Bulaya apewa fomu ya Ubunge kwa mbinde

Easter Bulaya apewa fomu ya Ubunge kwa mbinde

TAMKO

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2011
Posts
1,090
Reaction score
763
Ester Bulaya, mshindi Wa Tatu kura za maoni CDM, Amepitishwa na chama kupeperusha bendera ya chama kama mgombea Wa Ubunge -BUNDA. Alipokwenda kuchukua Form yake msimamizi Wa uchaguzi akamgomea. Kisa .."kwanini uwe wewe badala ya mshindi Wa kwanza".

Mtanange haukuishia hapo, mwenyekiti Wa chama plus mshindi Wa kwanza kwenye kura za maoni wote wakavamia offisi ya msimamizi huyo kushinikiza Ester Bulaya apewe Form, bado msimamizi akagoma kwa madai Yale Yale kwanini wakupe wewe sio yule. Mtifuano ulipozidi akaachia form.

Watanzania hii Tafsiri yake nini? Kiongozi sampuli hii huko mbeleni itakuwaje.. Na wako wengi type hiyo..

TAFAKARI AISEE..
 
MUNGU amtangulie Esther Bulaya manake hapo kwa tyson majanga asije tu akampiga manake huyo jamaa hapendagi changamoto hakawii kumdunda binti wa watu.
 
Hii ni dhahiri ccm wanamwogopa Ester Bulaya kuliko kawaida. Wanaona ni afadhali wasira asimame na mtu mwingine yeyote na si Ester Bulaya.

Tangu lini tume ina mamlaka ya kuvichagulia vyama wagombea?

This is ridiculous!.
Ndiyo maana kwenye maoni ya wananchi yaliyokuwemo kwenye Rasimu ya katiba ya Tume ya Warioba, hilo suala la kuwa na Tume ya uchaguzi huru lilikuwemo, lakini kwa kuwa hao magamba wanajua kuwa kuwepo na Tume huru ya uchaguzi hapa nchini itakuwa ndiyo 'kichinjio' chao, walipokwenda kwenye Bunge Maalum la Katiba, hao maccm wakaamua kuinyofoa ibara hiyo na kuibakiza ibara ya kwenye Katiba ya sasa ambayo inampa mamlaka Rais aliyeko madarakani kuteua Mwenyekiti hadi wajumbe wote wa Tume ya uchaguzi.
 
Mambo kama haya unayaona Tanzania na pengine nchi za Kiafrika...

Kuna viongozi ni watumwa mno wa mfumo CCM kiasi kwamba mambo wafanyayo hata nyani huwezi ona akifanya...
 
Bulaya ni mwiba kwa wasira,hawakupenda ester apite make wasira atakalishwa.
yani yule mzee simpendi jamani!!
 
Kwa ambao mlikuwa hamjui esther ndiyo chagua la wana bunda
 
hizi tasisi za umma zinafanya kazi kimazoea...si polis,tiss,nec,tcra,tbc
 
Hii kweli kali eti CCM ndio walioweka pingamizi eti apewe aliyekuwa wa kwanza ajabu kweli.
 
Back
Top Bottom