mkuu wakenya wamekuwa hivyo sababu waliitengeneza kenya yao wenyewe, Hata sisi tunaweza kuitengeneza Tanganyika yetu wenyewe!
Mkuu,wamefika hapo walipo kwa sababu walipewa nafasi
ya kuonesha uzalendo kwa nchi yao,Tanganyika ukiwa mzalendo utakufa mapema
kweli tena bila kufikia ulicho taka kufanya!
Tuna chagua maraisi kuongoza watanganyika lakini maraisi wenyewe kumbe
hakuna hata mmoja ambae ni Mtanganyika,Nani yule alikua
mzanzibari,mwingine akawa Mzulu (wa afrika kusini),huyu wa sasa ni mmarekani,...
Tutapata lini raisi wa "kitanganyika" kweli kweli?
Wakenya wamesha wekeza tanganyika kama vile kila kitu ni chao,tafuta
sehem hata moja afu unambie hawaja wekeza hapo,....hadi kalamu tunatumia
kama sio za kenya ni za china,...nambie sasa,tuitengeneze Tanganyika kwa kwenda
kuwekeza wapi?
kwa kipi tulicho nacho cha kuwekeza huko?
Waganda wana kiwanda cha kusafisha dhahabu lakini hawana dhahabu,...
wana nunua dhahabu Tanganyika,wanasafisha kwao then wanauza nje,...
nambie,tukawekeze nini na wapi?
Nasikia serengeti imenunuliwa na bush,tuna cha kuwekeza bado?
Tuki kimbilia kwenda kutafuta riziki kwenye madini,kwenye migodi yetu,kwenye
ardhi tuliyo zaliwa tuna uliwa kama sisimizi,hakuna hata kiongozi mmoja wa serikali
anae ongelea hili,.... "Rejea hapo juu nimekwambia hatuna raisi wa kitanganyika"
Kenya,na nchi zingine zinazo jali raia wake,akiuliwa kizembe hivi utasikia kama
sio raisi basi kiongozi mkubwa wa serikali anakemea na kuruhusu uchunguzi,umewahi kulisikia hilo
Tanganyika?
kwanini kujenga nchi ambayo hakuna anae kujali?
hakuna anae thamini ubinadamu wako kama Mtanganyika ila rangi ya "mzungu"?
Kwanini nisitamani kua mkenya ambapo ukionesha talent yako basi
uta saidiwa na serikali katika uvumbuzi wa kitu unacho fanya (rejea kijana alogundua umeme wa biogas kenya)
Wakati Tanganyika nasikia kuna kijana alivumbua jinsi ya kurusha matangazo
ya redio nadhani mpaka leo yuko jela,...kisa,..."ana haribu mawimbi ya radio zingine"?
Kwanini nitembee nje ya Tanganyika nikiwa najivunia kua mtanganyika
wakati kila raia wa nchi nyingine anajua kua Tanganyika haiongozwi na watanganyika?
ooops,bora nisikize mziki mie