unataka kusema tuliofurahia na kushangilia kuchaguliwa kwake tulikuwa majuha?Kwanini utarajie kutoka kwake,yeye kachaguliwa na wananchi wa USA na sio East Africa. Na aliapa atawatumikia wananchi wa USA na kuitetea USA na sio East Africa ,kwenye sera zake za kuingia white house hakuna mahala alisema atakuwa msaada wa East Africa
Waliotarajia makubwa na kushangilia na kupumzika watakuwa hawana uelewa dunia ya kibepari inavyoendeshwa
Acheni uvivu ufisadi na utegemezi ..mkiwekewa masharti magumu mnaanza kulalamika mara hatutaki ushoga nk nk
Wale waliopanga mstari asubuhi mpaka mchana kumsbiiria obama aliyekuwa kwenye tinted hakika niliwasikitikia sana
Walituvua nguo mchana kweupeTanzania tulifaidika mambo mengi kwa ujio wake alipo dhuru hapa...
Moja nilalo kumbuka ni barabara zetu kupigwa deki ukiiachilia mbali ule ufunguzi wa vituo vya uzalishaji umeme kinyerezi l, ll na lll nadhani.
Dunia ilipigwa na butwaa kuona mtu mwenye asili ya East Afrika kutaka kutawala taifa kubwa lenye nguvu za ushawishi, uchumi na kijeshi duniani. Sisi wana East Africa tulifurahi, kushangilia, kufanya tafrija na hata wengine kutoa mapunziko kwa wafanyakazi wasiende kazini kabisa wakati tukio lile linaelekea kwenda kutokea na hata lilipotokea. Bila shaka tulifanya hivyo tukiwa na akili zetu timamu na sababu zetu mbalimbali. Bila shaka miongoni mwa sababu hizo ni sifa tu ya u east africa, lakini kubwa zaidi ni kupata neema za taifa hilo kubwa za ki-diplomasia, kiuchumi na kisiasa kutoka taifa hilo kubwa.
Sasa amemaliza miaka yake mnane ya kutawala, Je, ile furaha yetu na matarajio yetu kwake ilikuwa sahihi? Tulichokipata kwake kinafanana kwa kiasi gani na kile tulichokitarajia kukipata kutoka kwake na Marekani? Kipo? ni kipi?
Wamarekani wanajuta kwa jamaa kuufufua upya ubaguzi wa rangi uliokuwa umeanza kufifia huko.Obama aliingia Uraisi wa USA analia na anaondoka huku akilia pia, hii nimeitoa mahali ,,Obama enter crying and leaving crying"!
Zaidi ya kumuua Gadafi na kuipiga Mabomu Somali hakuna lingine alilofanya, na siyo Afrika tu hata huko USA Wamarekani weusi hakuna kilichobadilika!