East Africa tuna cha kushukuru kwa 'ndugu yetu' Obama?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,233
12,508
Dunia ilipigwa na butwaa kuona mtu mwenye asili ya East Afrika kutaka kutawala taifa kubwa lenye nguvu za ushawishi, uchumi na kijeshi duniani. Sisi wana East Africa tulifurahi, kushangilia, kufanya tafrija na hata wengine kutoa mapunziko kwa wafanyakazi wasiende kazini kabisa wakati tukio lile linaelekea kwenda kutokea na hata lilipotokea. Bila shaka tulifanya hivyo tukiwa na akili zetu timamu na sababu zetu mbalimbali. Bila shaka miongoni mwa sababu hizo ni sifa tu ya u east africa, lakini kubwa zaidi ni kupata neema za taifa hilo kubwa za ki-diplomasia, kiuchumi na kisiasa kutoka taifa hilo kubwa.

Sasa amemaliza miaka yake mnane ya kutawala, Je, ile furaha yetu na matarajio yetu kwake ilikuwa sahihi? Tulichokipata kwake kinafanana kwa kiasi gani na kile tulichokitarajia kukipata kutoka kwake na Marekani? Kipo? ni kipi?
 
Kwanini utarajie kutoka kwake,yeye kachaguliwa na wananchi wa USA na sio East Africa. Na aliapa atawatumikia wananchi wa USA na kuitetea USA na sio East Africa ,kwenye sera zake za kuingia white house hakuna mahala alisema atakuwa msaada wa East Africa

Waliotarajia makubwa na kushangilia na kupumzika watakuwa hawana uelewa dunia ya kibepari inavyoendeshwa

Acheni uvivu ufisadi na utegemezi ..mkiwekewa masharti magumu mnaanza kulalamika mara hatutaki ushoga nk nk

Wale waliopanga mstari asubuhi mpaka mchana kumsbiiria obama aliyekuwa kwenye tinted hakika niliwasikitikia sana
 
africa tumepata misaaada kidogo zaid kutoka usa chini ya utawala wa obama kuliko chini ya utawala wa bush, miafrika ndivyo tulivyo connect the dot.
 
Kwanini utarajie kutoka kwake,yeye kachaguliwa na wananchi wa USA na sio East Africa. Na aliapa atawatumikia wananchi wa USA na kuitetea USA na sio East Africa ,kwenye sera zake za kuingia white house hakuna mahala alisema atakuwa msaada wa East Africa

Waliotarajia makubwa na kushangilia na kupumzika watakuwa hawana uelewa dunia ya kibepari inavyoendeshwa

Acheni uvivu ufisadi na utegemezi ..mkiwekewa masharti magumu mnaanza kulalamika mara hatutaki ushoga nk nk

Wale waliopanga mstari asubuhi mpaka mchana kumsbiiria obama aliyekuwa kwenye tinted hakika niliwasikitikia sana
unataka kusema tuliofurahia na kushangilia kuchaguliwa kwake tulikuwa majuha?
 
Tanzania tulifaidika mambo mengi kwa ujio wake alipo dhuru hapa...
Moja nilalo kumbuka ni barabara zetu kupigwa deki ukiiachilia mbali ule ufunguzi wa vituo vya uzalishaji umeme kinyerezi l, ll na lll nadhani.
 
Dunia ilipigwa na butwaa kuona mtu mwenye asili ya East Afrika kutaka kutawala taifa kubwa lenye nguvu za ushawishi, uchumi na kijeshi duniani. Sisi wana East Africa tulifurahi, kushangilia, kufanya tafrija na hata wengine kutoa mapunziko kwa wafanyakazi wasiende kazini kabisa wakati tukio lile linaelekea kwenda kutokea na hata lilipotokea. Bila shaka tulifanya hivyo tukiwa na akili zetu timamu na sababu zetu mbalimbali. Bila shaka miongoni mwa sababu hizo ni sifa tu ya u east africa, lakini kubwa zaidi ni kupata neema za taifa hilo kubwa za ki-diplomasia, kiuchumi na kisiasa kutoka taifa hilo kubwa.

Sasa amemaliza miaka yake mnane ya kutawala, Je, ile furaha yetu na matarajio yetu kwake ilikuwa sahihi? Tulichokipata kwake kinafanana kwa kiasi gani na kile tulichokitarajia kukipata kutoka kwake na Marekani? Kipo? ni kipi?

Obama aliingia Uraisi wa USA analia na anaondoka huku akilia pia, hii nimeitoa mahali ,,Obama enter crying and leaving crying"!

Zaidi ya kumuua Gadafi na kuipiga Mabomu Somali hakuna lingine alilofanya, na siyo Afrika tu hata huko USA Wamarekani weusi hakuna kilichobadilika!
 
faida ya Obama kuwa rais wa US ipo na isiyomithilika ,si kwa East Africa bali kwa dunia,usifikirie faida katika kupewa msaada tu,kama wewe ulifikiri katika upande huo pole
 
tumefaidika kwa kujua kuwa hakuna kikomo ikiwa mtu ana nia na kufanya kazi kwa bidii. kufikia urais wa US sio kitu kidogo.
 
Obama aliingia Uraisi wa USA analia na anaondoka huku akilia pia, hii nimeitoa mahali ,,Obama enter crying and leaving crying"!

Zaidi ya kumuua Gadafi na kuipiga Mabomu Somali hakuna lingine alilofanya, na siyo Afrika tu hata huko USA Wamarekani weusi hakuna kilichobadilika!
Wamarekani wanajuta kwa jamaa kuufufua upya ubaguzi wa rangi uliokuwa umeanza kufifia huko.
 
marekan ni mama wa dunia hivyo sioni sababu ya kumsema vibaya raisi huyo kwasababu nchini kama ili haiendeshwi kwa sera za watu wengi bali ni kwa kundi fulani na chama fulani hivyo nivigum kuamua jambo la kuwafaidisha wana east Africa bila kundi hilo kujua
 
Obama watamkumbuka wamarekani lakini sio
sisi. hivi tutamkumbuka kwa lipi? au kwa kutulazimisha waafrika tuwe mashoga.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom