kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,428
- 13,936
Dunia ilipigwa na butwaa kuona mtu mwenye asili ya East Afrika kutaka kutawala taifa kubwa lenye nguvu za ushawishi, uchumi na kijeshi duniani. Sisi wana East Africa tulifurahi, kushangilia, kufanya tafrija na hata wengine kutoa mapunziko kwa wafanyakazi wasiende kazini kabisa wakati tukio lile linaelekea kwenda kutokea na hata lilipotokea. Bila shaka tulifanya hivyo tukiwa na akili zetu timamu na sababu zetu mbalimbali. Bila shaka miongoni mwa sababu hizo ni sifa tu ya u east africa, lakini kubwa zaidi ni kupata neema za taifa hilo kubwa za ki-diplomasia, kiuchumi na kisiasa kutoka taifa hilo kubwa.
Sasa amemaliza miaka yake mnane ya kutawala, Je, ile furaha yetu na matarajio yetu kwake ilikuwa sahihi? Tulichokipata kwake kinafanana kwa kiasi gani na kile tulichokitarajia kukipata kutoka kwake na Marekani? Kipo? ni kipi?