Leo naona umejitahidi kuongea kiufasaha... Lakini vilevile bado haujajibu swali la mkenya, yeye kakuuliza hayo majigambo yote mmbona hamkuweza kwenda kuwadhibiti kina jMali kipindi kile walipo kuwa wakiteketeza jamii? Kama suala ni kuhusu kupokea wakimbizi basi hata Kenya inastahiri sifa kwani tokea zamani imekuwa ikipokea wasomali na wengine wengi kutoka mataifa mengineyo... Kwa kifupi mpaka dakika naona tukubaliane ya kwamba RPF inastahiri tuzo lisilo na kifani kwa kuwatuliza wauwaji kina jMali ndani ya miezi 3 na vilevile nijambo ambalo halijawahi kufanywa na yeyote yule duniani ukizingatia mda walioutumia kuwatuliza.
..hili suala Raisi wetu, Mzee Ali Hassan Mwinyi, aliwahi kulitolea maelezo.
..hii ni baada ya Mwalimu Nyerere kuishutumu serikali ya Tz kwa kutokuchukua hatua kuzuia mauaji kule Rwanda.
..Mzee Mwinyi alieleza nafasi yetu kama msuluhishi wa mgogoro wa Rwanda wakati ule ilikuwa inatubana tusiingilie kusaidia upande wowote.
..Vilevile alieleza kwamba jinsi mauaji yale yalivyoanza haikuwa rahisi kutofautisha kwamba yalikuwa mapigano ya wenyewe-kwa-wenyewe au ilikuwa ni genocide.
..suala lingine ni kwamba vyombo vyetu vilijielekeza ktk kushughulika na refugee crisis iliyotokana na mapigano/mauaji yaliyokuwa yakiendelea Rwanda. Ukumbuke kwamba mafuriko yale ya wakimbizi yalikuwa ni tukio la kipekee kupata kutokea ktk eneo lolote dunia.
NB:
..sasa ukirudi kwa hawa wenzetu Kenya, hivi wana sababu gani haswa ya kuulea mgogoro wa Somalia kwa miaka 20++?
..Pia kuna wakati Kenya walikuwa wanatamba kwamba wao wako business savvy kwa kuruhusu somali pirates wawekeze ransom money ktk real estate development in Nairobi.
..Zaidi Kenya imekuwa ikilaumiwa kwa kutotoa ushirikiano ktk kuwakamata key suspects wa genocide ya Rwanda.