ROBERT MICHAEL
JF-Expert Member
- Oct 23, 2012
- 5,054
- 2,873
Afadhali waende huko SADC eastafrika tumechoka na usanii.
Kamwambie Kenyatta kuwa hamuhitaji Tanzania ili mbaki nyie muwe soko lao.
Afadhali waende huko SADC eastafrika tumechoka na usanii.
Huyu jamaa nadhani anaumwa sibule, manake kila kitu Tutsi,Tutsi...we interahamwe unafikiri watanzania wote ni wahutu?? yani uhutu umekujaaaa...kilasiku watusi watusi...damu uliyo mwaga ya watusi haitoshi?? please watusi ni watu kama wewe..aliyewaumba hakufanya kosa...hiyo turufu ya uhutu haita wafikisha popote unajaribu kuwa rubuni watanzania lakini hutaweza mtanzania ni mtanzania sio muhutu.
Nendeni lakini kumbukeni mbio za sakafuni....
Ukiona Kenya anaanzisha kitu kinaitwa Joint, ujue kuna sehemu hawapawezi ndo maana wanataka wafaidike kwa mgongo wa wenyewe. Somalia wamepashindwa, wanataka wasaidiwe kwa mgongo wa joint military force ya EA
Exactly. Kunawakenya walikuwa wakisema wao walikuwa wanjali maswala ya uchumi na hawajali kusaidia nchinyingine za africa. Sasa wamzingukwa na vita na sisi tuwaambie tunaangali maswala ya uchumi tu. Somalia na south Sudan ni zigo lao hilo.
Aisei shule kwenu zina matatizo, hivi unafahamu ni majeshi ya nchi ngapi yalio Somalia ndio utoe povu kuhusu Kenya. Huwa sielewi vipi muda wote mpo kwenye mitandao ya jamii mkiongea kuhusu Kenya na Somalia wakati ukanda huu ni nyie tu ndio hamjajihusisha na hili suala la Somalia. Kaeni kimya huko pepmbeni wengine tutaendela kuthibiti huu ukanda.
..hivi Kenya hamuoni aibu kwamba nchi masikini kama Burundi ilitangulia Somalia kabla yenu?
F
..Somalia ni jirani yenu, kwa hiyo Kenya mnawajibu mkubwa zaidi kuliko mataifa mengine.
..Tanzania is stabilizing DRC, we can not be everywhere. Tunachoweza kufanya ni intelligence sharing which we are already doing.
..hivi Kenya hamuoni aibu kwamba nchi masikini kama Burundi ilitangulia Somalia kabla yenu?
..Somalia ni jirani yenu, kwa hiyo Kenya mnawajibu mkubwa zaidi kuliko mataifa mengine.
..Tanzania is stabilizing DRC, we can not be everywhere. Tunachoweza kufanya ni intelligence sharing which we are already doing.
JokaKuu Burundi ilitutangulia, na hilo ni jambo nzuri kuona pamoja na umaskini wao, walijitolea kwa hali na mali. Nchi zingine ukandaa huu wote zikafuata na Kenya ikiwemo. Nyie mkanuna na ndio mna kiherehere zaidi ya wote kuhusu Kenya na Somalia. Mkae kimya wakati nchi zote zingine zinahangaika kuthibiti hiyo nchi, Wabongo sasa hivi wanavuka mpaka wakienda kujiunga na ugaidi wa Alshabaab huku mmeficha kichwa kwenye mchanga eti hayawahusu, nakuhakikishia yatawahusu wakati waliorudi baada ya kufurushwa kule watahitaji kutumia ujuzi waliofundishwa kule.
Hilo la DRC usilitaje maana imebainika nyie ni mojawapo wa matatizo kule, soma ripoti ya UN uone jinsi mnawalea FDRL ili waendelee kuzingua DRC.
Mimi nina uhakika DRC is a sleeping giant, na majirani ndio wamekua wakiwarudisha nyuma, ile siku nyie wote mtawaacha na nchi yao, ndio siku DRC itapepea na kuwa nchi bora sana Afrika.
..Wakenya mnapenda kulalamika.
..Sasa mnataka Afrika na dunia nzima ihamie Somalia kuwasaidia?
..Haya matatizo ya Somalia mngeyashughulikia tangu wakati ule wa Siad Barre, na Mohamed Faraan Aidid.
MK254,
..mlitakiwa muingilie kijeshi wakati ule wa Siad Barre na Faraa Aidid.
..hivi mlivyofanya sasa hivi ni kama mmechelewa vile.
..sisi mara nyingi huwa tuna-act haraka kabla mambo hayajawa mabaya.
..ila kwenye suala la DRC kwa kweli tumechelewa na ndiyo maana unaona mambo yamekuwa kama yalivyo.
..tunapaswa kutafuta sababu za watoto wetu kutaka kujiunga na Al-Shabaab, na siyo kwenda kupigana nao Somalia.
..Al-Shabaab inaweza kufa leo na bado wa-Tz wakatafuta kundi lingine la kigaidi kujiunga nalo. Tuna tatizo hapa nyumbani ni lazima tushughulike nalo sisi wenyewe ndani ya nchi yetu.
NB:
..Huyu binti wa ki-Tz alikuwa na mabinti wengine wawili toka Kenya wakienda Somalia.
JokaKuu huo ni uwongo na unafiki wa hali ya juu na unajua hivyo, nyie ndio taifa kubwa dhabiti lililopakna na Rwanda halafu mlikaa pembeni hadi wakachinjana laki nane. Historia itawahukumu tu hata mkiendelea kuficha huo ukweli kwa kujaribu kuzingua amani iliyopo sasa hivi huko Rwanda.
..umesahau Tz tulivyohangaika kwa kuandaa mazungumzo ya amani kati ya utawala wa Habyarimana na RPF?
..Maraisi wa Burundi na Rwanda waliouawa kwa ndege yao kutunguliwa wakati wakitokea kwenye mazungumzo ya amani yaliyofanyika hapa Tanzania.
..Tumefanya mengi sana kwa hawa ndugu zetu wa Burundi, na Rwanda. Tena wakati mwingine Kenya imekuwa ikihujumu juhudi za Tanzania kuleta amani.
..Kama utakumbuka nchi za Afrika Mashariki tuliwahi kukubaliana kuwekea vikwazo vya usafirishaji kwa utawala wa Buyoya wa Burundi. Lakini Kenya kwa unafiki wenu mkawa mnakiuka makubaliano hayo kwa kuondoa vikwazo hivyo.
NB:
..Hatuna matatizo na Rwanda. Sasa hivi Rwanda inatumia bandari yetu, na Raisi Kagame anajifunza kuongea Kiswahili ili aweze kuelewana na wa-Tz vizuri zaidi.
JokaKuu Wewe ndio umejigamba hapa eti huwa mnaingilia kijeshi, wakati mliacha Warwanda wachinjane nusra wafike milioni bila kuingilia kijeshi.
Sasa hivi mnawalea FDRL ili wazingue DRC na Rwanda, hata UN imewashutumu kwa hilo. Ni unafiki huo.
..Rwanda tulisuluhisha kupitia mazungumzo ya Arusha.
..pia genocide ile ilimshtukiza kila mtu, na Tz tulipokea wakimbizi wengi toka Rwanda.
..ile migration tu ya wakimbizi wakati ule ilikuwa ni jambo ambalo halijapata kutokea mahala popote, na Tz tuliweza kukabiliana nalo kwa resources zetu wenyewe kabla UNHCR hawajajitokeza kusaidia.
..zaidi, wakimbizi waliokua hapa Tz wote wamerudi kwao na wanaijenga nchi yao.
..sasa linganisha na nyinyi mlichofanya. Somalia imekuwa ktk mgogoro kwa miaka zaidi ya 20 sasa. Nyinyi mmetanguliwa na Burundi kwenda ku-stabilize Somalia.