East Africa Airways

MAKANJAMNA

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
1,138
1,510
Kama kuna uzi kama huu basi mods wauunganishe.

Nilikuwa nawaza.. kufuatana na hizi sarakasi zinazoendelea kuhusu kununuliwa kwa ndege ili kuliamsha tena shirika la ndege la Tanzania (ATC).

Ukiangalia mashirika ya ndege ya ukanda huu yanapumulia mashine (KQ, precision etc) hasa kutokana na ushindani mkubwa wa kibiashara kwenye tasnia hii.. na kuishia kugombania wateja hao hao ambao ni kidogo.. Je kwa nini nchi za Afrika Mashariki zisifikirie kuunganisha nguvu na rasilimali zao ili kulifufua shirika la ndege la Afrika Mashariki?

Kwanza.. faida kubwa itakuwa distribution ya risk.. kueliminate ushindani na kujenga shirika imara ambalo litakuwa likitawala eneo hili lote hili.

Najua suala la wapi patakuwa kitovu cha safari nyingi (hub) litaibuka.. kila mtu akivutia kwake lakini hili linajadilika..

Kwa mfano.. badala ya kuwa na hub moja.. basi tugawanye safar katika miji mikuu mitatu..

Nairobi- Kitovu cha safari za Ulaya na Amerika

Dar es Salaam- Kitovu cha safari za Asia, Asia pacific na Australasia

Kigali- kitovu cha safari za Africa zote.

Entebbe- Matengenezo, Training na ndege za mizigo.

Hii nimeconsider pia geographical location ya miji ingawaje sipo sahihi sana.

Ningependa tulijadili hili swala ndugu zangu wote wa Afrika Mashariki bila mihemko au kejeli.. kwa kuwa mimi naona lina faida zaidi kuliko hasara.

Cc: MK254 Gezaulole
 
Maono safi.
Sawa ni vizuri, lakini daaaa"""huo mkanganyiko wa kisheria?Maana Kila mmoja ana madeni yanayomzidi kimo.bora tuangalie East African Railways.Reli haina mikanganyiko mingi ya kisheria mpaka sasa.
 
Mkuu wazo lako ni zuri sana lakini gumu kutekeleza hasa ukiwa na viongozi kama Kenyatta ambao wanaamini kila kitu lazima kiwe chini ya himaya ya wakikuyu.

Labda Rais M7 na mwenzake Magufuli wangekutana na kujadili hili swala kwasababu Uganda na Tanzania hazina mashirika ya ndege ya umma.Badala ya kila nchi kuanzisha shirika lake ni bora nguvu zikaunganishwa baina ya nchi hizi mbili ambazo tayari ziko katika harakati za ujenzi wa bomba la mafuta.

Uganda To Revive National Airline – Red Pepper Uganda
Serikali kuinunulia ATCL ndege mbili | Magazeti ya leo| Tanzania News |Tanzania Today
 
Back
Top Bottom