DW: Ujerumani ilivyoanza historia ya magari

KIMOMWEMOTORS

JF-Expert Member
May 17, 2018
358
670
Kwa hisani ya DW
Masuala ya Jamii

Ujerumani ilivyoanza historia ya magari
Historia ya gari ilianza 29 Januari 1886, pale mhandisi Carl Benz kutoka Mannheim alipowasilisha ombi la kupatiwa kibali cha serikali kwa ajili ya gari yake ya magurudumu matatu, iliyoweza kutembea kilomita kumi nane.

Magari yanayotengenezwa Ujerumani

Magari yanayotengenezwa Ujerumani

Muda mfupi baadaye, Gottfried Daimler, ambaye alisomea kutengeneza mikebe, akatengeneza mjini Stuttgart chombo chake kilichokuwa na uwezo wa kusafiri kilomita 16 kwa saa, tena bila ya mhandisi Carl Benz.

Chombo hiki lakini kilikuwa na magurudumu manne. Ukiangalia unaweza kusema chombo hicho kinafanana na ringshoo. Daimler alishirikiana na fundi wa injini, Wilhelm Maybach, ushirikiano ambao mpaka leo hii unaendelea.

Gari ya kileo

Gari ya kileo

Mhandisi mwengine, Nikolaus August Otto, alitengeneza injini mnamo mwaka 1876 aliyoipa jina lake mwenyewe. Mwaka 1892, Rudolf Diesel akabuni injini iliyokuwa na nguvu kubwa zaidi.

Kiroja cha mambo ni kwamba chombo hicho cha mwanzo kilikuwa kinaendeshwa kwa umeme.

Mnamo mwaka 1901 ndipo gari lilipokuwa na kasi ya kilomita 100 kwa saa moja.

Gari linalokwenda kwa mafuta lilianza kutumika mwaka 1920. Sababu ya kupata umaarufu magari yanayaoendeshwa kwa mafuta ni mwendo wake wa kasi unaotokana na injini zake zikitajikana kuwa ni bora, bei rahisi ya mafuta na nguvu za injini ikilinganishwa na magari yanayokwenda kwa nguvu za umeme.

Mnamo mwaka 1926 makampuni mawili ya magari Daimler na Benz yakaungana.

Vyombo kadhaa vinavyoendeshwa kwa injini vikaanza kuundwa. Kampuni la kwanza la magari liliundwa mwaka 1890 barani Ulaya na marekani. Alikuwa Henry Ford aliyeweka rekodi. Katika wakati ambapo kwa muda mrefu magari yalikuwa kwa ajili ya matajiri tuu, Ford wakaanza kutengeneza magari ambayo kila mtu anaweza akumudu kununua. Gari ya mwanzo ya Ford ilianza kuuzwa mwaka 1908.

Nchini Ujerumani, gari dogo la kampuni la Volks Wagen, mashuhuri kwa jina "Käfer" lilijipatia umashuhuri na kuchangia pakubwa katika kuinua uchumi wa nchi hii.

Kati ya makampuni kadhaa ya magari yaliyosalia nchini Ujerumani baada ya vita vikuu vyote viwili vya dunia, matatu tu ndiyo yaliyosalia na umashuhuri wake. Nayo ni Volkswagen na matawi yake ya Audi na kwa siku za karibuni Porsche, Daimler na kitambulisho chake cha jadi, Mercedes na BMW.

Mwandishi:
Ulrich Krause/Hamidou Oummilkheir
Mpitiaji: Yusuf Saumu Ramadhani
 
Hayo yalifanyika miaka Mia iliyopita kwasasa hapa kwetu tuendelee na biashara ya kununua madiwani.
 
Mwandishi: Ulrich Krause/Hamidou Oummilkheir
Mpitiaji: Yusuf Saumu Ramadhani
 
Back
Top Bottom