Duwasa Dodoma Kazi Imewashinda

MGOGOHALISI

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
1,984
2,586
Ni wiki ya tatu sasa kuna baadhi ya maeneo ndani ya viunga vya jiji la Dodoma hayana maji kabisa. Mnyetishaji wangu anaiambia maeneo kama Chidachi, kinyambwa, itega na kielekea Michese hayana maji kabisa licha ya kuahidiwa kuwa yatapatikana.

Mnyetishaji huyu anazidi kunidodosolea kuwa Duwasa wanasema wana shida ya umeme kwenye mashine zao shida ambayo hawajafafanua kuwa ni nini hasa.

Lakini wakati wanachi wanaendelea kukosa maji kuna maeneo hasa yale ambayo viongozi na wabunge wanaishi yameendelea kupata maji kwa mass 24 siku 7 zote za wiki. Duwasa wameamua kufanya hivi ili kuficha ukweli kwamba sasa hivi kuna Tatizo kubwa la maji linaloukabili mji wa Dodoma. Waziri wa maji tafadhali tembelea Duwasa maana watu wanapata tabu hapo makao makuu ya nchi
 
Mimaji yenyewe ni ya chumvi, lakini bado upatikanaji wake ni wa shida. Maeneo mengi ya Jiji yanapata maji kwa mgao ulio changamka kweli kweli!
 
Si useme wewe ndo mnyetishaji si kwa kuongea kwa uchungu ivo kuzidi wahusika.
 
Mkuu achana na mnyetishaji ingia idara ya maji wewe mwenyewe utapata jibu kuhus kwenye iyo sababu yao ya umeme maana siku hiz ukanjanja mwingi hadi wanakela Dadek,,, mim nikionaga miyeyusho napiga simu ad kw mkurugenz
 
Back
Top Bottom