Duterte: Nimeisikia sauti ya Mungu

Duterte: Nimeisikia sauti ya Mungu

amygdala

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2016
Posts
1,082
Reaction score
997
_91523868_mediaitem91037905.jpg


Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte, ameahidi kuacha kutumia lugha ya matusi baada ya kile anachosema kuwa ni kupata ujumbe wa moja kwa moja kutoka kwa Mungu.

Rais huyo, alliyemwita Rais Barack Obama "mwana wa kahaba" na akasema kiongozi huyo anaweza "kwenda jehanamu", amesema amefikia uamuzi huo baada ya kupata ufunuo alipokuwa safarini kutoka Japan.

Amewatusi pia watu wengine mashuhuri. Alimwita kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis "mwana wa kahaba" (Ufilipino ni taifa lenye Wakatoliki wengi).

Amewahi kumtusi pia waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry kwa kumuita "mwendawazimu" na majuzi alimweleza balozi wa Marekani nchini Ufilipino kama "mpenzi wa jinsia moja ambaye ni mwana wa kahaba".

Bw Duterte amesema kuwa alipokuwa kwenye ndege, na watu wengine wote walikuwa wamelala, alisikia sauti ikimuonya: usipokoma, nitaiangusha ndege hii.

Amesema sauti hiyo ilijitambulisha kuwa ilitoka kwa Mungu.

Amewaahidi watu waliokusanyika mji wake wa nyumbani wa Davao kwamba ahadi kwa Mungu ni sawa na ahadi kwa Wafilipino.

Rais Duterte ni kiongozi ambaye msimamo wake na matamshi yake huzua utata mara kwa mara.

Amesomea taaluma ya sheria na alipanda cheo hadi kuwa mwendesha mashtaka kabla ya kuteuliwa kuwa naibu meya wa Davao wakati wa mapinduzi yaliyomuondoa madarakani Ferdinand Marcos mwaka 1986.

Alikuwa meya mwaka 1988 na kushikilia wadhfa huo kwa kipindi cha miaka 10, kabla ya kushinda kiti cha ubunge katika Bunge la Congress halafu akarejea kwenye kiti cha umeya mwaka 2001.

Alijijengea umaarufu kwa kupiga vita baadhi ya matatizo makubwa yanayowakabili Wafilipino - uhalifu, makundi ya uasi, na ufisadi. Yote haya yalipungua kwa kiwango kikubwa wakati alipokuwa kiongozi wa Davao, na kufanya mji huo kuwa mmoja wa miji salama zaidi nchini Ufilipino.

Duterte ambaye utawala wake ni wa kipekee kwa kuwa kiongozi mwenye sera za Kijamaa na mwanamageuzi kwa pamoja, sera zake za uchumi zilikuwa si za kuaminika wakati wa kapeni.

Majuzi, alilinganisha vita vyake dhidi ya walanguzi wa mihadarati na mauaji ya Wayahudi wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Alisema anaweza kuua walanguzi wengi wa dawa hizo za kulevya sawa na alivyofanya Hitler akiua Wayahudi.

"Hitler aliua Wayahudi milioni tatu ... kuna waraibu milioni tatu wa dawa za kulevya. Ninaweza kufurahia sana kuwaua," amesema.

Wayahudi zaidi ya milioni sita waliuawa na Wanazi chini ya Hitler..

Chanzo: BBC Swahili
 
Mhhhh!!.....Mungu gani anamuonya kuwa aache kutukana watu ila hamuonyi kuacha kuua watu???
 
Nimemuelewa huyu bwana.Kaisikia sauti ya 'Mungu' na SIO 'Mwenyezi Mungu'. Mwenyezi Mungu hazungumzi na watu wa hovyo.
 
Mataifa ya Magharibi yanampimia tu huy jamaa. Soon atakipata anachokitafuta.
 
Huyu Rais ni kichaa kamili, sauti ya Mungu kaisikia wapi?
Angelikuwa ameambiwa aache dhambi hapo sawa lakini anadai kasikia tu... huyu lazima wamarekani watamuua tu....

Na iwe hivyo. Nchi inaongozwa na kichaa, kichaa kabisa
 
Huyu Rais ni kichaa kamili, sauti ya Mungu kaisikia wapi?
Angelikuwa ameambiwa aache dhambi hapo sawa lakini anadai kasikia tu... huyu lazima wamarekani watamuua tu....
Wasiwasi wake tu. Unaweza kuta wakati yupo ndani ya ndege alipata hofu Kama ndege ikianguka au kutunguliwa atakufa na akifa anaenda wapi? mahesabu yake yakampeleka jehanamu akaona nikitua salama nimsifu MUNGU.
 
Msidharau Maneno ya Mtu akiamua kutamka maneno kutoka mdomoni Mwake.. na wala Msimdhihaki... ni Maamuzi ambayo humtokea yeyote akipata ufunuo... Tumejifunza mengi sana na kusikia watu watoao ushuhuda wengi huwa hawajitungii... na mara zote matamko yao huwa ni furaha kwa wafia dini... hupatwa na faraja sana... na Most wale wamkoseae Mungu ndio huwa Mashuhuda Wakuu... Trust Me
 
Those mystic believes are part of delirium...........anaelekea kwenye uchizi huyo rais
 
Nimemuelewa huyu bwana.Kaisikia sauti ya 'Mungu' na SIO 'Mwenyezi Mungu'. Mwenyezi Mungu hazungumzi na watu wa hovyo.
Ukisema watu wa hovyo unamaanisha nini? Mungu haongei na watakatifu tuu....ila yupo pia kwa ajili ya kuwa-collect hata wale watenda dhambi wakubwa kuliko hata yeye ili kuwaweka ktk right direction.
 
Watakuwa wauza madawa wameshaanza kumroga maana naonaga hata kwenye tamthilia zao wachawi sana wale jamaa
 
Duh huyu kichaa kama yule muzee kakiwanja wote ni janga yule hujiita kiongozi wa malaika na mungu mtu alau huyu kasikia sauti
 
Back
Top Bottom