Naangalia tu democracy in action kwenye Republican Convention mjini Cleveland Ohio. Natamani Watanzania wangefuatilia jinsi chama cha siasa kinavyotakiwa kuendesha mkutano wake katika nchi zilizokomaa kidemokrasia. Sauti pinzani zinazimwa ama kwa maridhiano au kura na katu hazinyamazishwi kimizengwe. Kwa kweli tukubali tusikubali kuna mengi ya kujifunza ingawa si lazima tuyafuate.
VYOMBO VYA HABARI
Navyo vinaendelea na kazi zake.
Uchambuzi wa hotuba ya mke wa Trump Bi Melanie Trump imeonekana na matatizo.
Kuna mistari aliyobeba kutoka kwa Michelle Obama ya 2008
Katika mizania ya siasa za Marekani, hili linaweza kuleta mjadala utakaohamisha ujumbe aliokusudia Bi Trump.
Wapo wanaomlaumu mwandishi wa hotuba kwa kuchukua kauli ya Michelle.
Siyo big deal, lakini Melanie ni mke wa mgombea hivyo wapinzani wao Democrat wataigeuza hoja kufunika hoja nyingine.
Tayari wanaisema ni 'plagiarism' na kuhoji ule uaminifu wanaousema upo wapi?
Haya ni makosa ya kifundi ambayo kwa siasa zilizokomaa yanatumika.
Kwa nchi zinazoendelea, kusema mke wa mgombea 'kaibia' utalala mbali na nyumbani
Waandishi wa habari wanaitafuta timu ya Trump ya mawasiliano kueleza jambo hilo.
Melanie kama mke alikuwa akimwelezea mumewe dunia imfahamu.
Kwa hili, ile message yake inapoteza nguvu kwani vyombo vya habari vinatafuta habari kwa kile wanachosema 'habari si mbwa kumg'ata binadamu bali binadamu kumg'ata mbwa'
Tayari Trump keshamtangaza mgombe mwenza,Gavana wa jimbo la Indiana Bw Mike PenceWakuu Mag3 & Nguruvi3 naendelea kusoma bayana zenu Mungu awabariki si kila mtu ana nafasi ya kufuatilia siasa za USA lakini kupitia mabandiko yenu tunajikuta tuko karibu na taifa hilo kubwa duniani.
Sijui kama wagombea tayari wameshatangaza wagombea wenza wao au bado.Naamini wagombea wenza wana nafasi kubwa ya kuongeza chachu ya ushindi kwa wagombea urais.Itakuwa jambo la afya iwapo mtajadili nafasi za wagombea wenza na jinsi gani wana weza kusaidia ushindi wa wagombea URAIS.
Mkuu uliona ulinzi na heshima wanayopewa wagombea wa vyama vyote, huwezi kujua yupi ni mgombea wa chama tawala au chama pinzani. Bila shaka umemuona hata
Sheriff Clarke
(mweusi) anavyowaponda Rais Obama na Senator Clinton na kuwalaumu kwa kutokemea kauli ya
Black Lives matter
akidai hata
Blue Lives matter
akimaanisha polisi. Hapa Tanzania hata askari wa kawaida tu anaweza akamtisha mgombea Ubunge na hata mgombea Urais mradi tu anatoka Upinzani...inasikitisha!
Mkuu Nguruvi3, leo kaulimbiu ya GOP itakuwa make America work again lakini kinachojadiliwa hadi sasa ni purukusani iliyogubika Convention katika siku ya kwanza. Ilianza kwa baadhi ya wajumbe kutomkubali Trump na kutaka sheria zifanyiwe marekebiso, ikafuatiwa na hotuba aliyotoa Mama Trump ambayo imekuja kugundulika ni plagiarism ya ile ya Mama Obama mwaka 2008.Taratibu za uchaguzi wa Marekani
Mwaka 2008 mkutano mkuu wa kwanza kufanyika ulikuwa Democrat
Mwaka 2012 mkutano mkuu wa kwanza kufanyika ulikuwa Republican
Na mwaka 2016 mkutano mkuu wa kwanza ni Republican
Haya haytokei tu kwa chama kuamua kupanga. Ni utaratibu uliokubalika na vyama kwamba chama pinzani ndicho huanza mkutano mkuu kikifuatiwa na chama kilichopo madarakani
Hivyo, Rep kufanya mkutano wao sasa hivi ni sehemu ya utaratibu na utamaduni uliokubalika katika siasa za Marekani
Ni kama ilivyo uchaguzi mkuu. Huu hufanyika Jumanne ya kwanza inayofuatia Jumatatu ya kwanza ya mwezi November.
Hapa ieleweke kuwa si lazima iwe Jumanne ya kwanza ya mwezi November ambayo inaweza kuwa ni tarehe 1, bali Jumanne ya kwanza baada ya Jumatatu ya kwanza ya November
Kwa mantiki siku ya uchaguzi wa Jumanne hiyo ni kati ya tarehe 2-8 November.
Haya ni mambo yapo tu yanasubiri muda kutokea kila msimu
Hayahitaji tangazo la tume yoyote, ni utamaduni wa siasa zilizokomaa
Katika kipindi hiki, wagombea hupewa taarifa na Rais 'briefed' linapotokea jambo lolote lenye masilahi ya Taifa hasa dharura
Swali litakaloulizwa, mbona watu hawasikii tume ya uchaguzi ya Marekani?
Nani anakusanya matokeo na kujumlisha kama Tume yetu ya NEC?
tutajadili
Aliyekuwa kampeni meneja wa Trump aliyefukuzwa June Lewandowski amesema aliyehusika wajibishwe.Mkuu Nguruvi3, leo kaulimbiu ya GOP itakuwa make America work again lakini kinchojadiliwa hadi sasa purukusani iliyogubika Convention katika siku ya kwanza. Ilianza kwa baadhi ya wajumbe kutomkubali Trump na kutaka sheria zifanyiwe marekebiso, ikafuatiwa na hotuba aliyotoa Mama Trump ambayo imekuja kugundulika ni plagiarism ya ile ya Mama Obama mwaka 2008.
Kwa kweli Convention ya GOP imeanza vibaya na leo watu wanasubiri kuona mabadiliko katika ukomavu kiuendeshaji. Wengi wanajiuliza inakuwaje mtu ambaye amekuwa akijitamba na kuwaita mahasimu wake wa siasa wajinga anashindwa kuwapata watu makini wa kumsaidia. Je atazungukwa na watu wa aina gani wataokuwa washauri wake wakuu serikalini akishinda Urais?
NB: Hiyo ya Tume ya Uchaguzi Marekani ni habari nyingine kabisa ha ha haa...!
Lile kundi la never Trump safari imekwisha, Trump ndiye nomineeBreaking News!
Donald J. Trump is no longer the presumptive nominee for President of the United States but the GOP official nominee. He reached the threshold of 1237 delegates at 7:12 pm Eastern Time with votes cast by delegates from his home state of New York.