May 29 2016
VIONGOZI WA WABUNGE WA CCM(CAUCUS) CHUKUENI HATUA
AIBU HII KWA TAIFA HADI LINI?
NDIO AIBU ILIYOFICHWA KWA 'BUNGE LIVE'
Tunakushukuru
chinchilla coat kwa video hii inayoeleza mambo mawili
1. Kwamba, mpango wa waziri Nape kuzuia matangazo umeshindwa na unawarudi CCM
Kuficha kinachoendelea bungeni kumejenga
curiosity kwa wananchi, na video au recorded sound zinapatikana mitaani kwa urahisi sana. Zuio lime backfire vibaya na kuwaumiza CCM
2.Tuliwaeleza CCM na viongozi bungeni kujenga nidhamu ya kuongea kwa utafiti na utaifa.Mnadhimu wa wabunge wa CCM aangalie caucus yake kama ipo sawa
Tulisema kwasababu video ya Mbunge Gekul kama inavyoonekana, inajenga hoja nzito.
Hata kama hatukubaliani na hoja, kitu kimoja tunakubaliana, Gekul anajenga hoja kama mbunge, anajua anaongelea nini na kwa nani na wakati gani.
Bila kujali maudhui, ukweli au upotoshaji, tumsifu kwa namna alivyojenga hoja
Bunge lipo kimya Gekul akieleza anachokiona. Si kuwa wananchi wanafarajika bali wanajengewa imani Dodoma wanaelewa matatizo yao na kuyajadili kwa lengo la utaifa.
Tunarudia tena ,Viongozi wa CCM Bungeni wafike mahali wafanye jambo la maana.
Kuwafunza wabunge maana ya bunge, uzungumzaji, uchangiaji, mantiki na Utaifa
Wasipofanya hivyo wakitegemea waziri Nape ataficha uozo kwa marufuku ya bunge live, ni kujidanganya. Kinachoendelea sasa kinaonekana mitaani.
Wala CCM wasije tafuta mchawi au kupiga ramli.
Tusemezane