Mtazamo wangu Mimi LOWASA kujiunga CDM itaisaidia CHADEMA ila lengo la Lowasa kwenda Ikulu halifanikiwi itabaki kuwa ndoto isiotimia,ataleta ushindani sana KATIKA Urais, kura zitoongezeka,wabunge pia,faida kwa upinzani,ila Lowasa haiwezi kushinda,sababu CCM ina mtu mwenye record KATIKA utendaji
Hayo kayaongea baada ya kukatwa.
Lembeli, naye anasema alitakaa kuongwa milioni 200.
Ester, naye anasema aliahadiwa uwaziri akakataa.
Usihesabu siku zifanye siku ndiyo zihesabu
Mkuu pengine huelewi jinsi gani Lowassa alikuwa na power ndani ya CCM hiyo ya Mtandao kiasi kwamba kujiuzuru kwake kulichukuliwa kama kujitoa mhanga. Na ndio maana alikuja kuwa bado mwenyekiti wa kamati ya usalama bungeni, mjumbe wa kamati kuu kitu ambacho hakuna waziri yeyote alokatwa na JK alirudi kuwa na madaraka.. Wako wapi kina Msabah na Karamagi! sii bungeni wala ndani ya chama wana sauti tena..Hapana Mkuu naona umechangaya dawa, aliyekubaliana na japo machache na kutilia mshaka 7, 8 na 9 ni Waberoya. Mimi sijatoa comment yoyote isipokuwa nimeomba tu comment kutoka kwa wadau niliowataja. Bado nayatafakari hayo madai yako na nikiwa tayari utanisikia loud and clear...hata hivyo kuna kitu kimoja kinanishangaza, unataka kuniambia kwamba hata baada ya kujiuzulu Lowassa aliendelea kuwa master mind muda wote wa ufisadi ccm? Kwamba aliendelea kuwachagua mawaziri? Kwamba aliendelea kuchukua 10% ya kila deal nchini? Aliendelea kuwa kinara wa miradi mingi ya kuuza ardhi na majumba?
Duh Mkandara, je katika muda huo tulikuwa na Raisi? Tulikuwa na serikali? Tulikuwa na cc ya kina Mkapa na Mwinyi na wazee wa kamati kuu na madili? Je kwa wakati huo tulikuwa na watu ambao walijua siri kubwa ya huyu mtu kuliko hata sisi wengine? Ila kwa sababu ya Lowassa wote wakakunja mikia, hakuna aliyethubutu kumgusa hata pale alipochaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya usalama bungeni au alijichagua!
Jamani tuache mambo ya kipuuzi kwenye issue kama hizi. Hizo nguvu Lowassa alizipata wapi! Kwa nini hazikuweza kuzuia asikatwe? Mwinyi aliwahi kujiuzulu akiwa waziri wa mambo ya ndani na hakuna aliyeuliza kwa nini alikubali kujiuzulu kama hakuhusika? Mwalimu Nyerere mwenyewe wakati anampiga biti Waziri Mkuu Malecela alionya, Waziri Mkuu anaweza kuchukuliwa hatua nchi ikabaki salama lakini si Raisi. Lowassa alikuwa kondoo wa kafara kwenye issue ya Richmond kama walivyokuwa Msabaha na wengine.
Kesho CCM wameitisha mkutano, CCM ina nguvu, ina serikali, ina vyombo vya usalama ambavyo naviita vyombo vya kulida usalama wa genge lililoko kwenye utawala na kuwatesa wananchi...waangalie tu wasifungue pandora box!
Kitu ambacho najiuliza na sipati jibu ni kwanini Lowassa ana wafuasi wengi? Hivi ni pesa au ni ushawishi wake alionao kwa vijana au au?
Maana tukatae tukubali ndani ya CCM hakuna mtu mwenye wafuasi wengi kama Lowassa nasema hivyo kwa kuangalia mikutano yake mbali mbali (rejea mkutano wa Dar na vijana wa boda boda na mtu huyu hana record ya kusomba watu kwa mabasi) au wakati wa kutafuta wadhamini.
Hawa watu wanatafuta nini kwa Lowassa? ni kitu gani alichofanya ndani ya miaka 8 ambacho kinawavutia hawa watu?
Swala la pili, ni mgumu kumeza lakini ndizo siasa tunabadilika kutokana na wakati na kutona na watu wa jamii yako. Nafikiri watanzania uelewa wetu ni mdogo kuhusu swala zima la ufisadi na madhara yake.Hivyo basi watu walio wengi vijijini ukiwambia mambo ya ufisadi hawaelewi kabisa maana wao walishaona kuwa kuishi kwenye nyumba ya tope ni halali yao,kuna watu hata hawafahamu umeme ni nini au una umuhimu gani, kuna watu ambao hawaoni umuhimu kuwa na maji ya bomba wameridhika na maji ya visima ambayo utumia muda wa 1 mpk 6 kufuata maji. Visima vikakauka kwa ajili ya ukame wao hizo ni laana kutoka kwa mwenyezi Mungu. Na mtu wa jinsi hii kumpa elimu kuelewa kuwa umaskini wake unachangiwa na ufisadi au matumizi mabaya ya madaraka au rushwa ni ngumu. Na kwa bahati mbaya au nzuri hawa watu ndo wengi na ndo wanatuchagulia viongozi.
Sasa basi inapotokea watu wa jinsi hii wakataka mtu ambaye watu wengine wenye uelewa wa mambo wanaona huyu mtu hafai kwa sababu moja au nyingi, kuna kuwa hakuna ujanja tena bali kuwapa yule mtu ambaye wanaona anawafaa wao.
Na hiki ndicho kinachotokea Tanzania, na baadhi ya nchi za kiafrika.
Nachelea kusema uchaguzi wa mwaka huu kama Chadema wangemsimamisha DR,Slaa na CCM Magufuli, basi Mafuguli alikuwa anapata ushidi tena asubuhi ingawaje utendaji wa Dr. Slaa kwa hapa Tanzania hauna mfn. Record zake ziko safi kwa kila sehemu alipopita. na huu ndio ukweli na hii ndio gharama ya demokrasia,
Kwa maana hiyo watanzania hatupendi watu waadilifu tunapenda mafisadi, hivyo basi sisi sote ambao tunapingana na ufasidi na wale ambao hawana habari na ufisadi hatuna budi kuchagua kati ya fisadi mmoja (Lowassa) au mfumo wa kifisadi ambao ni CCM. Kwa bahati mbaya sana hata vyama vingine vya siasa vikaamua kumsimamisha malaika hakuna hatayempigia maana kama watu wangekuwa wanachukia ufisadi basi leo hii Kikwete hasingekuwa madarakani..
Wapeni watu mtu anayemtaka maana wao ndio wapiga kura husipowapa utashindwa katika sanduku la kura.
Kama watanzania wanamtaka Lowassa au la ngoja tuone huku mbeleni maana kwa ili sina uhakika kama ni mapenzi tu au ni nguvu ya pesa
Kwenye link hii hapa chini kuna clip yake akisema maneno hayo ni kuanzia dakika 23.40Ukienda mkoa wa Kilimanjaro wana barabara mpaka vijijini ndani.
Kuna mwaka nilienda Kilimanjaro kuna mzee alisema kuna shule 50 za sekondari,lakini sisi Kigoma tulikuwa nayo moja tu.
Wale wenzetu wako mbali kimaendeleo...
Yeah, nimeuona uzi, naomba yoyote mwenye comment, swali au chochote aeleze kwanza. Nipo na nitazungumzia suala na hoja zote kwa undani, kina na uyakinifuNguruvi3. Can you tell us now who's killing the opposition? Is that ACT or an invisible hand >
Nguruvi3. Can you tell us now who's killing the opposition? Is that ACT or an invisible hand >
Naam una mshindo! Nilichokisema nasimama nacho kwa ushahidi bila shaka.Mkuu,
Swali lako ni fupi lakkni limebeba mjadala mpana sana.
"Mtaalam" wetu wa masuala ya kisiasa Nguruvi3 nadhani anaogopa urefu wa kina cha swali lako!Tuendelee kusubiri labda anakusanya vielelezo!Wahenga walisema "ukimya una mshindo"
Kama kuna eneo tulilorudi nyuma kama Taifa ni kushindwa kutumia siasa kwenda pamoja na uelekeo mmoja. Siasa imekuwa uhasama, chuki na hata kufikia kuondoa utu.Hakika siasa za Tanzania ni ngumu..
Miaka minne baadaye yametokwa mambo ambayo hakuna mtu yeyote angeweza kufiiria kama yanaweza kutokea..Siasa imekuwa ni uhasama. Watanzania tumepoteana..
Kuondoa UTU. Na hilo ndilo kusudio Kuu la aina yoyote ya Umagharibi pale unaposhadadiwa kwa pupa. Ni kututoa katika UKUU WETU ili tubaki kuwa wanyonge tutawalike. Haya si Mapya ni Matokeo tarajiwa.Kama kuna eneo tulilorudi nyuma kama Taifa ni kushindwa kutumia siasa kwenda pamoja na uelekeo mmoja. Siasa imekuwa uhasama, chuki na hata kufikia kuondoa utu.
Remnat wa mtaa wa Lumumba, kama maana ya remnat ni kuwahi kufanya kazi Lumumba, ndiyo wameingia kwa kishindo na sasa ndiyo injini ya ACT ingawa Zitto bado anaonekana kuendelea kushika usukani.Naiangalia kama future opposition party endapo hakutakuwa na 'remnant' kutoka mtaa wa Lumumba