Dunstan Tido Mhando Mkurugenzi Mpya Mwananchi Communications Limited

asha ngedere

Member
Nov 6, 2009
92
11
Wadau, taarifa nilizozipata punde ni kwamba, Mkurugenzi wa zamani wa TBC, Dunstan Tido Mhando ndiye amelamba ajira ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications limited na kwamba anatambulishwa rasmi kesho Ijumaa.Mhando anachukua nafasi ya Sam Sholei aliyemaliza muda wake mwaka jana.
 
Asianzishe tena kipindi cha MCHAKATO MAJIMBONI vinginevyo Mwananachi Communication itafungiwa na Dr. Nchimbi Waziri habari na utamaduni.
 
Kutoka Aljazeera (EA) to Mwananchi Com, anyway makao makuu yote yako Nairobi..............................
 
dah nimefurahi Jembe limerudi shambani
Mungu asaidie tu wasije wakammwakye!
 
Hongera zake kama ni Kweli. Ndio uzuri wa shule, mtu hawezi kukubabaisha jinsi anavyotaka yeye labda shule yako iwe ya kubebwa. Congrats bro!
 
Hawa jamaa si waliwahi kutangaza wataanzisha TV? Anyway, wale wanahabari walamba viatu vya JK/serikali wamepata ushindani
 
Wananchi communications..wow..majua Ally Mfuruki atakua amempigia chapuo since he's the chairman of Wanachi Group for the whole EA..
 
Alwasaidia vijana wa komedi sasa wanalia kupata tenda TBC, TBCCM ina rudi rivasi, kwenye taarifa ya habari wamebaki wanatangaza semina za viongozi tu, no substance kabisa kwenye hii TV, kweli inaboa sana. watangazaji hawana adabu, wapo kimagamba gamba tu, hadi hapo uhuru kamili utakapo patikana labda ndo itafufuka.

Hivi CiTIZEN TV ya kenya si ya watu bnafsi, mbina za za kwetu hovyo tu?????
 
hivi ile tv ya citizen ni mali ya mwananchi comm?
Hapana Citizen ni ya Royal Media chini ya mkikuyu Macharia,Mwananchi mmiliki wake ni Aghakhan kupitia kampuni ya Nation inayomiliki hilo gazeti,NTV,Daily Nation n.k
 
  • Thanks
Reactions: bht
Alwasaidia vijana wa komedi sasa wanalia kupata tenda TBC, TBCCM ina rudi rivasi, kwenye taarifa ya habari wamebaki wanatangaza semina za viongozi tu, no substance kabisa kwenye hii TV, kweli inaboa sana. watangazaji hawana adabu, wapo kimagamba gamba tu, hadi hapo uhuru kamili utakapo patikana labda ndo itafufuka.

Hivi CiTIZEN TV ya kenya si ya watu bnafsi, mbina za za kwetu hovyo tu?????
Du yaani TBC ni RTD nashangaa baada ya kuondoka Tido hata mitambo inagoma!! kwenye taarifa ya habari ndio usisema picha inasubiriwa utafikiri inabebwa mkononi kutoka pale Ambiance hadsi hapo Taasisi ya Vielelezo(vijana wa siku hizi hamjui hiyo taasisi)ni hapo Bamaga ilipo sasa TBC
 
Back
Top Bottom