Duniani mengi yamepotoshwa

Ryan The King

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
2,788
2,690
Amani iwe nanyi Kama vile ilivyodesturi kwangu.

Historia ya dunia imegubikwa na mambo mengi ya kutia mashaka, imevishwa Koti la uwongo na propaganda za kibinafsi kwa kuwanufaisha wachache huku wengi wakikandamizwa.

Historia ya dunia ndio hufanya kizazi cha Leo kushindwa kuutambua ukweli ambao ulifukiwa katika makaburi ya kidini ambayo Leo hii yanatumaini ilhali dini hizo ndio chanzo cha mateso na mahangaiko ya Mwanadamu.

Huenda baadhi ya wasomaji watapenda kujua ushahidi wa haya niliyo yaandika lakini sitatoa ithibati yoyote kutokana na udanganyifu wa nukuu nyingi zilizopo Duniani.

Yapo makundi kadha wakadha Mathalan Wajiitao Atheist, Wakristo, Wahamadia(Waislam), Wabudha, Waprotestant listi ikiwa inaendelea. Makundi haya hakuna kundi lolote ambalo lipo katika njia salama. Wote hutumia maandiko yaliyojawa na ubinafsi katika kuelezea mambo yasiyo yakibinafsi.

Falsafa na itikadi za makundi haya ni matokeo ya njia panda za fikra za watangulizi wao. Hivyo wao huendeleza njia panda za watangulizi wao walioshindwa katika fikra zao katika zama zao.

Hakuna anayejua Dunia ilianza lini hivyo ni upumbavu wa mtu yeyote kudhani au kusema kuwa huu ni mwaka Fulani(Kwa mfano mwaka 2017) Wakati hujui miaka ya dunia ilianza lini. Hivyo Hakuna kilichosawa katika zama hizi kwani hata Mwanzo wa dunia haufahamiki.

Baadhi ya vitabu ambavyo makundi Fulani huviita vitabu vitakatifu, ambavyo huvipa utukufu usio na maana yoyote. Vitabu hivi vimejaa ubinafsi mkubwa, kinachoshangaza ni kuwa vitabu vyenyewe huelezea mambo yasio na ubinafsi.

Ukweli wa mambo katika Dunia hii ulizikwa zamani Sana kabla ya kiumbe wa kwanza kuumbwa. Kwa ujumla binadamu hawezi kuwa na historia yoyote kutokana na kuja na kukuta mambo yote yakiwa yapo katika mfumo.

Dhana ya ubinadamu yenyewe bado ni yakufikirika kwa watu wanaojua kufikiri haswa. Ikiwa Ubinadamu tuu waweza kuwa dhana telezi vipi kuhusu Dhana ya MUNGU, Shetani, malaika n.k.

Jambo linalofanya dhana ya binadamu kuwa telezi ni mianzo ya viumbe hawa katika dunia hii. Baadhi ya simulizi katika vitabu vya kale, kwa mfano Msahafu wa kikristo huleta maswali mengi Sana katika kisa cha Kaini aliyemtoto wa Adam kumuua mdogo wake Habil. Kitendo cha Kaini kuogopa kupigwa na kuuawa na watu ambao moja kwa moja si binadamu huweza kueleza kuwa Adam hakuwa mtu wa kwanza bali alikuwa miongoni mwa Watu walioumbwa awali.
Hii itaenda Sambamba na viumbe wengine ambao waliumbwa kwa aina zao kwa kufuata koo zao.

Mwandishi wa kitabu cha Biblia katika vitabu vya Mwanzo na kutoka iwe kwa kukusudia au laa alificha historia muhimu ya asili ya Watu wengine na kujikita kwa Adamu ambaye ni Asili yake. Jambo hilo amelirudia katika kuelezea historia ya taifa lake(Israel), na kuacha historia ya Watoto wengine Wa Abrahamu mfano Ishmael na watoto wengine wa Ketura.
Ni kusema Musa(kwa kudhani), huenda aliandika simulizi makini isiyo na mashaka lakini huenda kuna waliochakachua maandiko yake au yeye mwenyewe ndiye hakuandika simulizi zenye umakini usio na maswali.

Utofauti wa viumbe katika Tabia, lugha, maumbile, rangi, kimo n.k ndio umezidi kuleta taarifa zisizo zakweli kwani baadhi ya watu ambao hudhani na kudhaniwa kuwa wanaakili hutengeneza dhana nyingi za uongo kwa misukumo yao ya ubinafsi.

Yafuatayo ni mambo yenye uongo Mkubwa yaliochapizwa kwa watu kutoka zama zilizopita.:-
1. Dhana ya "Ubinadamu" na mambo ya Kiroho Kama Mungu, shetani.
UBINADAMU
-Asili ya binadamu
-lengo la kuwepo kwake.
-Kufa kwake na dhana ya kuishi tena.
-mabadiliko yake ya kiumaumbile, kitabia, kimaarifa n.k
MUNGU.
-Ni nani
-Alitokeaje
-anafananaje
-Yupo api
-yupo au hayupo
-aliumba au
-Kama yupo anafanya mini
SHETANI
Ni sawa na hayo ya Mungu.

2. Asili ya Dunia.
-chanzo chake.
-Umri wake.
-Mmiliki.
-matukio yake.
- kuisha kwake.

3. Asili ya matukio Dunian
Kama Magonjwa, majanga na mabaa,

4.Matukio ya hali na michakato na hali za viumbe hai na visivyo hai.

Mambo hayo ndio huwafanya wale wajuao kuandika na kushawishi kuudanganya Ulimwengu.

Hata kuzuka kwa Wasio amini Mungu ni Mpango maalumu wa watangulizi.
Lengo la kuudanganya ulimwengu ni kuwafanya watu wachanganyikiwe kuhusu ukweli na mwishowe kutokuamini kabisa
 
Na wewe ndiyo unazidi kuchanganya kabisà . ungesema umeyafanyia kazi hayo na unaanza kupata majibu ya maswali yako ningeanza kukuelewa.
 
huenda hakuna yeyote anaeujua ukweli maana kote kuna mkanganyiko!
ila tafiti za kweli ndizo hutoka namajibu yenye uthibitisho ila tafiti nyengine ni ngumu hasa ya kujua mwanzo wa kila kitu!
human we are so kind ulimwengu ni mkubwa mno kuufahamu ukweli ni kazi.
 
Ni kweli Mkuu. Ndio maana bado sijaweka Ukweli zaidi ya kuonyesha dhana mbali×2 ambazo zimefanya ulimwengu kuwa na historia ya uongo. Sifa ya uongo kubwa ni kuzua maswali mengi akilini.
 
ningependa uweke ukweli huo tuujadili
 
Sawa Mkuu.

Ngoja nikamilishe andiko ambalo litapunguza maswali kwa kiasi kikubwa
 
Uovu ni mvamizi, uovu ni mawazo mabaya ndani ya moyo wa kiumbe, MUNGU huichunguza mioyo ya viumbe wake na hukiamlia kadri ya uovu wake, mara nyingi hukumu ya uovu ni kifo yetu macho na masikio
 
Mtoa mada kwan leo tarehe ngap?
Leo huweza kuwa tarehe yoyote kwa kiumbe yoyote kwa kuzingatia umri wa kiumbe husika.

Aidha ni vigumu kujua tarehe ya kiumbe husika ikiwa umri wa dunia ukiwa haufahamiki.
 
Mtoa mada me nakushauri hebu jaribu kusoma kitabu kinachoitwa Quran.Kitabu hiki kina majibu yote uliyohoji hapo juu na pia utapata kuelewa mengine usiyoyajua.Ni kitabu ambacho hakina wasiwasi wowote na hutajuta kukisoma.Note:Wakati unakisoma hakikisha akili yako iko huru...utaelewa tu Mkuu.Na kumbuka majibu yako yanapatikana ndani ya kitabu hicho tu na si pengine.
 
Wewe una asubuhi yako na jioni yako kulingana na saa yako ya kuzaliwa
 
Mtoa mada me nakushauri hebu jaribu kusoma kitabu kinachoitwa Quran.Kitabu hiki kina majibu yote uliyohoji hapo juu na pia utapata kuelewa mengine usiyoyajua.Ni kitabu ambacho hakina wasiwasi wowote na hutajuta kukisoma.Note:Wakati unakisoma hakikisha akili yako iko huru...utaelewa tu Mkuu.Na kumbuka majibu yako yanapatikana ndani ya kitabu hicho tu na si pengine.
Mkuu Ntafwatilia.

Ila kwa nijuavyo ni kuwa Quran ni muhutasari wa Biblia.
 
Amani iwe nanyi Kama vile ilivyodesturi kwangu.

Historia ya dunia imegubikwa na mambo mengi ya kutia mashaka, imevishwa Koti la uwongo na propaganda za kibinafsi kwa kuwanufaisha wachache huku wengi wakikandamizwa.

Historia ya dunia ndio hufanya kizazi cha Leo kushindwa kuutambua ukweli ambao ulifukiwa katika makaburi ya kidini ambayo Leo hii yanatumaini ilhali dini hizo ndio chanzo cha mateso na mahangaiko ya Mwanadamu.

Huenda baadhi ya wasomaji watapenda kujua ushahidi wa haya niliyo yaandika lakini sitatoa ithibati yoyote kutokana na udanganyifu wa nukuu nyingi zilizopo Duniani.

Yapo makundi kadha wakadha Mathalan Wajiitao Atheist, Wakristo, Wahamadia(Waislam), Wabudha, Waprotestant listi ikiwa inaendelea. Makundi haya hakuna kundi lolote ambalo lipo katika njia salama. Wote hutumia maandiko yaliyojawa na ubinafsi katika kuelezea mambo yasiyo yakibinafsi.

Falsafa na itikadi za makundi haya ni matokeo ya njia panda za fikra za watangulizi wao. Hivyo wao huendeleza njia panda za watangulizi wao walioshindwa katika fikra zao katika zama zao.

Hakuna anayejua Dunia ilianza lini hivyo ni upumbavu wa mtu yeyote kudhani au kusema kuwa huu ni mwaka Fulani(Kwa mfano mwaka 2017) Wakati hujui miaka ya dunia ilianza lini. Hivyo Hakuna kilichosawa katika zama hizi kwani hata Mwanzo wa dunia haufahamiki.

Baadhi ya vitabu ambavyo makundi Fulani huviita vitabu vitakatifu, ambavyo huvipa utukufu usio na maana yoyote. Vitabu hivi vimejaa ubinafsi mkubwa, kinachoshangaza ni kuwa vitabu vyenyewe huelezea mambo yasio na ubinafsi.

Ukweli wa mambo katika Dunia hii ulizikwa zamani Sana kabla ya kiumbe wa kwanza kuumbwa. Kwa ujumla binadamu hawezi kuwa na historia yoyote kutokana na kuja na kukuta mambo yote yakiwa yapo katika mfumo.

Dhana ya ubinadamu yenyewe bado ni yakufikirika kwa watu wanaojua kufikiri haswa. Ikiwa Ubinadamu tuu waweza kuwa dhana telezi vipi kuhusu Dhana ya MUNGU, Shetani, malaika n.k.

Jambo linalofanya dhana ya binadamu kuwa telezi ni mianzo ya viumbe hawa katika dunia hii. Baadhi ya simulizi katika vitabu vya kale, kwa mfano Msahafu wa kikristo huleta maswali mengi Sana katika kisa cha Kaini aliyemtoto wa Adam kumuua mdogo wake Habil. Kitendo cha Kaini kuogopa kupigwa na kuuawa na watu ambao moja kwa moja si binadamu huweza kueleza kuwa Adam hakuwa mtu wa kwanza bali alikuwa miongoni mwa Watu walioumbwa awali.
Hii itaenda Sambamba na viumbe wengine ambao waliumbwa kwa aina zao kwa kufuata koo zao.

Mwandishi wa kitabu cha Biblia katika vitabu vya Mwanzo na kutoka iwe kwa kukusudia au laa alificha historia muhimu ya asili ya Watu wengine na kujikita kwa Adamu ambaye ni Asili yake. Jambo hilo amelirudia katika kuelezea historia ya taifa lake(Israel), na kuacha historia ya Watoto wengine Wa Abrahamu mfano Ishmael na watoto wengine wa Ketura.
Ni kusema Musa(kwa kudhani), huenda aliandika simulizi makini isiyo na mashaka lakini huenda kuna waliochakachua maandiko yake au yeye mwenyewe ndiye hakuandika simulizi zenye umakini usio na maswali.

Utofauti wa viumbe katika Tabia, lugha, maumbile, rangi, kimo n.k ndio umezidi kuleta taarifa zisizo zakweli kwani baadhi ya watu ambao hudhani na kudhaniwa kuwa wanaakili hutengeneza dhana nyingi za uongo kwa misukumo yao ya ubinafsi.

Yafuatayo ni mambo yenye uongo Mkubwa yaliochapizwa kwa watu kutoka zama zilizopita.:-
1. Dhana ya "Ubinadamu" na mambo ya Kiroho Kama Mungu, shetani.
UBINADAMU
-Asili ya binadamu
-lengo la kuwepo kwake.
-Kufa kwake na dhana ya kuishi tena.
-mabadiliko yake ya kiumaumbile, kitabia, kimaarifa n.k
MUNGU.
-Ni nani
-Alitokeaje
-anafananaje
-Yupo api
-yupo au hayupo
-aliumba au
-Kama yupo anafanya mini
SHETANI
Ni sawa na hayo ya Mungu.

2. Asili ya Dunia.
-chanzo chake.
-Umri wake.
-Mmiliki.
-matukio yake.
- kuisha kwake.

3. Asili ya matukio Dunian
Kama Magonjwa, majanga na mabaa,

4.Matukio ya hali na michakato na hali za viumbe hai na visivyo hai.

Mambo hayo ndio huwafanya wale wajuao kuandika na kushawishi kuudanganya Ulimwengu.

Hata kuzuka kwa Wasio amini Mungu ni Mpango maalumu wa watangulizi.
Lengo la kuudanganya ulimwengu ni kuwafanya watu wachanganyikiwe kuhusu ukweli na mwishowe kutokuamini kabisa
Uzi wako unafikirisha sana lakini pia kuna wajanja wachache ambao wametengeneza mfumo unaojiendesha wenyewe ukiwa na uongo mwingi. Wao ukweli wanaujua wametulia tuli wanawaangalia mnavyotifuana!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom