Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,717
- 41,494
Kimsingi, matatizo yetu mengi, kuanzia kutokuwa na umeme wa uhakika, barabara za chini ya kiwango, ufisadi kwenye miradi, utawala holela usiofuata misingi ya utawala bora, ukiukaji wa katiba na sheria unaofanywa na watawala, mpaka uchafu mwingine mwingi, kwa kiasi kikubwa, chanzo ni Serikali.
Dunaini kote mabadiliko hufanywa na watu, siyo mbuga za wanyama, siyo udongo, siyo madini wala maziwa. Ila watu wenye upeo, maarifa, uadilifu na wabunifu, ndiyo huzitumia rasilimali hizo kuleta maendeleo.
Lakini ni ukweli mtupu kuwa mwananchi mmoja mmoja, pamoja na kuwa na nafasi kubwa katika kuleta maendeleo, kuna sehemu kubwa ya Serikali inayoamua jitihada za huyo mwananchi zilete mafanikio au ziishie kwenye hasara tupu. Kwa mfano:
Mwananchi anaweza kujenga kiwanda, anaweza kuweka mifumo ya umwagiliaji, lakini kama hakuna umeme, atafanya nini ili asiishie kwenye hasara?
Mwananchi anaweza kuzalisha vizuri mazao ya shambani au bidhaa zake kiwandani, lakini kama mifumo ya kodi ipo hovyo, hakuna barabara nzuri za kusafirishia mizigo yake, mwananchi huyu atapiga vipi hatua za maendeleo?
Wanafunzi na wanavyuo wanaweza kufanya bidii sana ya kujifunza, wakahitimu masomo yao, wakawa wapo tayari kufanya kazi kwa bidii, lakini kama kutokana na sera mbovu za nchi, watu wanaogopa kuwekeza, hao wahitimu wataajiriwa wapi?
Utofauti mkubwa wa maendeleo kati ya nchi na nchi, unategemea sana utofauti wa aina ya serikali zilizopo katika mataifa. Mkiwa na Serikali duni iliyojaza viongozi na watendaji wa serikali wenye upeo duni, maarifa duni, uadilifu duni, uelewa duni, LAZIMA nchi hiyo iwe na uwekezaji duni, ajira duni, maisha duni, huduma duni, mifumo ya kodi duni, mifumo ya utawala duni, mifumo ya demokrasia duni, na maendeleo duni kwa ujumla.
Kinachokatisha tamaa zaidi ni ukweli kwamba ni rahisi sana kuiondoa Serikali nzuri yenye viongozi wazuri madarakani kuliko kuiondoa Serikali mbaya yenye viongozi duni madarakani.
Kiongozi mzuri, kelele tu za wananchi dhidi yake, zinatosha kumfanya ajiuzuru, lakini kiongozi mbaya yupo tayari hata kuua wanaomkosoa ili tu aendelee kuwepo madarakani. Serikali mbaya zenye viongozi wasio na maono wala uwezo wa kuyahakikishia maendeleo mataifa yao, hakuna chochote kikubwa wanachohangaika nacho isipokuwa kufikiria na kupanga mbinu mbaya na nzuri kuhakikisha kwa vyovyote wanabakia madarakani, iwe kwa amani au kwa upanga.
Ndiyo maana utaona Serikali za namna hiyo hujiwekea kinga za kutoshtakiwa watawala (kwa sababu wanajua kabisa kuwa watafanya uovu), hawapo tayari kuwa na tume huru za uchaguzi (kwa sababu wanajua kukiwa na tume huru za uchaguzi hawawezi kushinda uchaguzi), ndiyo maana hata zoezi la uchaguzi wanapenda liwe siri (ndiyo maana wanazuia wananchi wasishudie zoezi la kuhesabu kura, wanawataka wananchi wakipiga kura waondoke).
Wanajua uwezo wa kuongoza hawana. Uwezo wa sera za kuwavuta wananchi wawachague haupo. Uwezo wa kutatua changamoto kubwa za msingi hawana. Kwa sababu wanajua hawawezi kuchaguliwa na wananchi, hivyo ni aheri kuweka taratibu za kiinimacho ambazo zitazuia wananchi kufanya maamuzi. Yaani ni watu ambao wameamua kuwa wananchi mpende msipende, sisi tutawatawala tu.
Kwenye nchi zilizostaarabika, kiongozi anataka awe na uhakika kama wananchi wanataka awaongoze. Kuna wakati kule Italy Waziri mkuu alikuwa na uhusiano na kimada, kelele zikawa nyingi dhidi yake. Waziri Mkuu alikiri kuwa alikuwa ametenda kosa, akaitisha kura ya maoni ili ajue wangapi, hata baada ya kosa hilo, wanapenda aendelee kuwa Waziri Mkuu, huku akiwa tayari kujiuzulu. Tujiulize hapa kwetu, ukimwacha Mzee Mwinyi na Lowasa, hawa waliopo sasa ndani ya Serikali, nani ana uwezo wa kufanya hivyo?
Kule UK, mwaka 1974, nchi ilipoingia kwenye umeme wa mgao, wananchi waliiondoa Serikali ya Conservative madarakani, na Waziri mkuu Edward Heath aliachia madaraka kwa amani akikiri kuwa Serikali yake ilizembea hadi nchi kufikia kwenye mgao wa umeme.
Sisi hapa kwetu licha ya mgao wa umeme usio na mwisho, achilia mbali Rais, mliwahi kusikia hata mkurugenzi wa TANESCO au waziri wa Nishati amejiuzulu?