Boniphace Kichonge
JF-Expert Member
- Jul 31, 2017
- 1,605
- 1,958
Rais Donald Trump ataungana leo na viongozi wa nchi 16 katika kuadhimisha miaka 75 tangu kuanza kwa operesheni ya kijeshi iliyoikomboa Ulaya kutoka mikononi mwa Wanazi wa Ujerumani, maarufu kama D-Day.
Trump atakuwa pamoja na wenyeji wake, Malkia Elizabeth II na Waziri Mkuu Theresa May, na pia Kansela wa Ujerumani Angela Merkel katika maadhimisho hayo yanafanyika katika mji wa Portsmouth Kusini mwa Uingereza. Wakongwe 300 walioshiriki katika operesheni hiyo watahudhuria pia.
Tarehe kama ya leo mwaka 1944, wanajeshi 170,000 wa nchi washirika walivuka bahari na kutua kwenye fukwe za Normandy nchini Ufaransa, ikawa mwanzo wa mwisho wa utawala wa Wanazi wa Ujerumani waliokuwa wameyakalia maeneo makubwa ya Ulaya katika vita vikuu vya pili.
Wazee 300 walioshiriki katika operesheni ya D-Day wameshiriki maadhimisho hayo
Rais Donald Trump anatarajiwa kutoa heshima kwa wanajeshi waliouawa katika vita hivyo, kabla ya kuondoka Uingereza akielekea Ireland.
Katika mkutano na waandishi wa habari jana mjini London, Trump alisema anayo heshima kubwa kwa wanajeshi hao, aliowataja kama 'mashujaa waliojitolea maisha yao kuunusuru ustaarabu'. Alisema urafiki uliotengenezwa wakati wa operesheni hiyo, na kuimarishwa na damu iliyomwagika, utadumu milele.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau na Rais wa Ufaransa ni miongoni mwa viongozi wengine watakaoshiriki katika maadhimisho hayo yanayoongozwa na Waziri Mkuu Theresa May na Malkia Elisabeth II.
DW