Hii kwenye psychology inaitwa bystander effect, mtu akiwa na shida mnabaki kuangaliana nani atakua wa kwanza kujaribu kumsaidia, au kama wote mtasimama tu mnajifanya kusubiri mamlaka husika. Hapo moja tu angetamka tumsaidie kila moja angekomaa kumsaidia huyo mtu.
Simshangai sana huyo mama kabeba mtoto kuliko navyomshangaa huyo kijana pembeni na yeye anaonekana kama kashika simu, na aliyepiga hii picha naye walewale, hawa followers wa kim kardashians kweli wanatupeleka pabaya.
Sema pia tuconsider hilo pozi la huyo mtu, kama bado mzima unaweza kuta hilo chuma limeingia ndani ya mwili, maana yake hicho chuma ndo kitu kinachompa uhai wakati huo, wangesema wamtoe damu ika~leak, kulingana na eneo waliopo lazima angekufa hajafika popote, hata kama kuna doctor ndani ya bus sidhani kama angeweza kumsadia kuzuia blood leakage kwenye mazingira kama hayo.