Dunia sio duara!

Dunia sio duara!

Je ni kwanini mshale upo kwenye saa ya mkononi au ukutani hlakini haugusi namba zote kwa wakati mmoja?? we elewa tunapata usiku na mchana kwa sababu jua ni taa ndogo haiwezi kumulika dunia kwa mpigo inamulika huku ikizunguka, yaan kama mshale unavozunguka kutupa majira ya saa na dk ndiyo jua hutupa siku week mwezi na mwaka.
Wanadanganya kwa faida gani mkuu
 
Ili waweze ku-establish new world order kirahisi. Yapo mabara katika north & south pole ambayo yapo duniani ila wanadamu tulio wengi hatuyajui!
...sijakuelewa hapo kwenye mabara yaliyopo duniani ila hatuyajui mkuu,..if you can mention plus ufafanuzi kidogo.
....thanks kwa maelezo mkuu
 
...sijakuelewa hapo kwenye mabara yaliyopo duniani ila hatuyajui mkuu,..if you can mention plus ufafanuzi kidogo.
....thanks kwa maelezo mkuu


Pitia hapa mkuu, hii ni mada pana kidogo.

Pia tafuta video ya admiral byrd aliyepaa na ndege to the north pole utakuta mambo ya kushangaza sana ambayo yameondolewa makusudi kwenye elimu yetu na wazungu.
 
hivi kuna yeyote kati yetu alie wahi kwenda nje ya dunia na kuipiga picha tukaiona ni ya duara, si tunaletewa tu picha kwamba ni duara.., mi nimeamua kugoma mpaka niende nikahahakishe mwenyewe.., dunia sio duara kabisa..!
Umepitia secondary kweli? usingeuliza swali hili maana ni topic ya form one na hata huko primary wanagusia vitu hivi darasa la nne.Hata hivyo tunashukuru umeleta mada nzuri kikubwa umeweza kuandika kimaandishi.
1.Uhakika wa zaidi ambao nchi yetu na bara la Afrika hatuna uwezo nalo ni kwamba ukitoka kwa chombo kwenda anga za juu let say kilometa kama 100 hivi ukiangalia ulikotoka dunia yetu unaiona tena kwa juu sasa ushangae sio chini unaiona ina rangi ya blue hii blue ni bahari na utaona vivuli vivuli hayo ni mabara na utaona ina umbo la mduara kama yai kidog.
2.Kama unasafiri na vyombo majini au hata boat ukiwa katikati ya maji kama kuna meli inakuja unaanza kuona mlingoti wa moshi kwa halafu baadae kidogo kidogo unaona meli nzima hii inathibitisha dunia ni duara
3.Chukua kitabu chako cha atlas au kitabu cha ramani.Fungua ramani ya dunia tawala.Angalia mahali marekani ilipo kisha angalia jimbo la Alaska lilipo.Utaona liko kushoto mwa ramani yako.Kisha angalia upande wa kulia kabisa wa Urusi.Utagundua utaona maumbo ya visiwa vinafanana upande huu na upande huu.Maana yake ni kwamba ukitokea Alaska au Marekani ukitaka kwenda Urusi huna haja ya kukatiza bahari ya Atlantic kisha ukate bara Africa kisha ukate bahari ya Hindi ukate nchi ya china ndio uiingie Urusi.Unachofanya wewe kule Alaska unaelekea zako magharibi utaona utafika urusi na ni njia fupi.
 

Attachments

  • Earth-donkeyhotey-596x596.jpg
    Earth-donkeyhotey-596x596.jpg
    50.4 KB · Views: 50
  • map.gif
    map.gif
    26.4 KB · Views: 61
Last edited by a moderator:
 
Back
Top Bottom