Dunia - Rules of the game:

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
33,063
40,310
Dunia - Rules of the game:

1. Dunia ni mapito.... kila nafsi itaonja mauti-
2. Tenda wema upate kuishi miaka mingi zaidi...
3. Wape haki zao wanaokuzunguka......usithubutu kuipoka haki ya mwenzako.
4. Utaondoka na kuiacha dunia kama ulivyokuja - ukiwa mtupu.... acha majivuno..
5. Mazuri na vitamu huwa haviishagi duniani, kula kwa ustaarabu.....usiwe mrafi...
6. Tamaa ni sumu, usithubutu kumdhuru ama kumpora mwenzako yeyote kwani malipo yake ni hapahapa.....
7. Dunia si mali ya mtu, kila kitu ulichokichuma utakiacha hapa hapa......
8. Hakuna refa, bali matendo yako mema na ya haki yatakuweka salama,
9. Fanya kazi kwa bidii, toa sadaka kwa wasio kuwa nacho....hiyo ni hazina kwako...
10. Usithubutu kutoa roho ya mwenzako kwani itakusumbua kila upitapo hadi umauti ukukute..

Ukizifuata rules hizi, basi maisha yako ya muda hapa duniani yatakuwa na furaha na amani tele.

Amani na iwe kwenu.
 
Saw kabisa mkuu.ni vema sana kuish duniani kwa kufata mising hiyo madhubuti na imara kabisa.lakin binadamu tuna shida sana,vigumu sana kutekeleza yote hayo.ila inawezekana!
 
Hata ukifata hayo yote si kwel kwamba kazima uishi kwa furaha na amani tele kama ulivyosema. Sema ni muhimu tu kuishi hivyo ili kama kunathawabu basi tuzipate lakn narudia si lazima matokeo kuwa kama matarajio hayo uliyosema.
 
Kuna watu ukiwaambia wasiwe walafi hawatakuelewa..wewe hushangai embe ukiliona bichi ukilivutia muda wenzako wanalila na chumvi
 
Mtendee jirani wako kama vile upendavyo wewe kutendewa. Hii ni kanuni kuu, inaongoza kanuni zote za Asili. Jirani ni yeyote au chochote kile, ambacho kinaweza kikaathirika na matendo yako.

Miti, uoto, wanyama, watu, anga na kila kitu ni miongoni mwa majirani tunaotakiwa kuwatendea kama vile tupendavyo nasi kutendewa.
 
Dunia - Rules of the game:

1. Dunia ni mapito.... kila nafsi itaonja mauti-
2. Tenda wema upate kuishi miaka mingi zaidi...
3. Wape haki zao wanaokuzunguka......usithubutu kuipoka haki ya mwenzako.
4. Utaondoka na kuiacha dunia kama ulivyokuja - ukiwa mtupu.... acha majivuno..
5. Mazuri na vitamu huwa haviishagi duniani, kula kwa ustaarabu.....usiwe mrafi...
6. Tamaa ni sumu, usithubutu kumdhuru ama kumpora mwenzako yeyote kwani malipo yake ni hapahapa.....
7. Dunia si mali ya mtu, kila kitu ulichokichuma utakiacha hapa hapa......
8. Hakuna refa, bali matendo yako mema na ya haki yatakuweka salama,
9. Fanya kazi kwa bidii, toa sadaka kwa wasio kuwa nacho....hiyo ni hazina kwako...
10. Usithubutu kutoa roho ya mwenzako kwani itakusumbua kila upitapo hadi umauti ukukute..

Ukizifuata rules hizi, basi maisha yako ya muda hapa duniani yatakuwa na furaha na amani tele.

Amani na iwe kwenu.
Afadhali hujaweka ya usifanye uzinzi maana hapo tungejua unatutafuta
 
Tatizo kuu la wanadamu ni Tamaa na wivu - Kijana anaanza kazi leo kesho anataka amiliki gari, nyumba nk ni lazima amuibie mwajiri wake ama
Kuna watu ukiwaambia wasiwe walafi hawatakuelewa..wewe hushangai embe ukiliona bichi ukilivutia muda wenzako wanalila na chumvi
kaka urafi si kwa chakula tu, urafi ni kwa kila kitu tufanyacho hapa duniani, tufanye wa kiasi.
 
Afadhali hujaweka ya usifanye uzinzi maana hapo tungejua unatutafuta
kaka Uzinzi ipo kwenye number 6 (Tamaa); usiwe na tamaa inayokutuma wewe kutenda yasiyompendeza mwenzako; Tamaa ya mwili inaingia hapa hapa. Usifanye ngono kupita kiasi, tendo la ngono limeletwa duniani kwa minajili ya kuzaana tu na si kwa starehe. ukilitumia ngono kama starehe ukifanya na watu mbalimbali badi umevunja kanuni za kuishi duniani.
 
A game changed many years ago, those rules they don't work at the moment.
 
DUNIA NI SEHEMU SALAMA ZAIDI YA KUISHI KAMA TUTAONDOA TOFAUTI ZETU NA KUISHI KWA KUWAJALI WENGINE PIA
 
Uko vyema...umesahau ile ya Usipende kumfanyia mwenzako kitu ambacho wewe hupendi kufanyiwa!!
 
Back
Top Bottom