Dunia ni uwanja wa vita za hatima

Dunia ni uwanja wa vita za hatima

Niko naandaa huo Uzi wa meditation so nitaushare... Maswali uliza tu Healer na nitajitahidi kuyajibu kwa kadri nitakavyo elewa na yale ambayo yatakosa majibu basi tutazidi kuyatafutia ufumbuzi.
Unitag ukiutoa
Kwa hapa siwez kuyauliza 😔
 
Somo limeeleweka bro, endelea..

Natumai mko salama.

Kama kichwa cha habari kinavyosema kwamba dunia ni uwanja wa vita za hatima kwahiyo kila mtu ambae yuko hapa duniani anapaswa kujua kwamba yuko vitani na swala la kushinda au kushindwa ni juu ya mtu mwenyewe.

Sasa iko hivi...

Kimsingi ni kwamba kila mwanadamu ambae yuko kwenye hii dunia hayupo hapa kwa bahati mbaya na inawezekana wazazi waliomzaa mtu huyo wanaamini wamemleta huyo mtu hapa duniani kibahati mbaya ila kiroho hakuna kitu kinachoitwa bahati mbaya.

Maadam umezaliwa na uko hapa duniani basi kaa ukijua kuna mission unatakiwa uitimize na hii mission ndio ambayo tunaita hatima na pindi utakapoitimiza mission hiyo basi hapo ndio utakapopata uhuisho wa roho yako na kuifanya iwe hai milele na roho ambayo iko hai ndio roho ambayo husikia inaposemeshwa na ndio maana katika asili za kiafrika hasa hapa nyumbani Tanzania unakutana na kitu kinaitwa mizimu.

Sasa mizimu ni nini? Mizimu ni roho ambazo ziliishi kwenye milli ya watu fulani kwa uadilifu kwa maana ziliweza kujua zipo hapa duniani kwa lengo gani yaani hatima yao na wakapigana vita ya kuiendea hiyo hatima na wakafanikiwa kwa kiasi kikubwa na pindi deadline yao ya kuishi hapa duniani ilipofika zile roho zao ziliweza kuuhishwa na kupata uzima wa milele.

Kwahiyo Sasa katika ile mitetemo ya mfumo nyota ya koo na koo ukiweza kujiungamanisha kiroho na roho za babu ambao unawajua walikua manguli katika upande wa kutibu au kwenye jambo lolote lile ambalo lilikua hatima ya babu huyo ila ilimradi tu uwe na uhakika kwamba alifanya kweli makubwa na sifa zake hadi leo bado zipo hapo kijijini basi ukijiungamanisha tu na roho za watu wa namna hii huwa zinasikia na zinatoa majibu papo kwa hapo.

Nimesema uwe na uhakika kwasababu usije ukaenda kujiungamanisha na mtu ambae huna uhakika nae na ukaenda kuvaa roho za ajabu zikakutesa kwenye maisha yako na hapa ndipo ambapo watu wengi wanachukia haya mambo ya mizimu kwasababu huwa ni ngumu kujua babu yako mzaa babu yako alichokifanya kama kilisaidia kuongeza positive energy hapa duniani au laa (hapa nitapazungumzia vizuri huko mbele na utajua kwanini watu wanakimbilia kwa Yesu au Muhammad huku wakiacha mizimu ya babu zao kule kijijini).

Kwasasa turudi hapa kidogo...

Kikawaida binadamu huwa yuko na pande kuu mbili yaani ya damu na nyama na ya kiroho.

Upande wa kiroho ndio Upande ambao umembeba mtu halisi na ndio upande ambao unamuunganisha mtu na ulimwengu wa asili yake na upande huu huu unapokuwa hapa duniani huwa unatumika kama redio call na kwanini kama radio call basi nitakwenda kukuelezea hapo mbele kidogo. Na upande wa damu na nyama ndio upande ambao unamuunganisha mtu na ulimwengu huu wa vita za hatima.

Wakati mtu anapozaliwa huwa anakua anaishi zaidi kwenye ulimwengu wa kiroho kuliko ulimwengu huu wa damu na nyama ila kadri anavyokua na kujifunza mambo mapya ile mitetemo yake ya ulimwengu wa asili yake inapungua na ya ulimwengu huu inaongezeka hadi kufikia kwenye ukubwa toshelezi na hapa ndio mtu anaanza kuishi maisha ya ulimwengu huu wa damu na nyama na kusahau namna ya kuishi ulimwengu wa kiroho.

Na kutokana na kwamba binadamu anaishi zaidi katika ulimwengu wa damu na nyama kuliko ulimwengu wa kiroho hii imefanya wengi wetu tushindwe kuelewa lengo na dhumuni la sisi kuwa hapa duniani na badala yake tunaishi kulingana na mfumo wa kidunia na kushindwa kuelewa hatima zetu ni nini.

Na kitu cha kikuu na chaumuhimu zaidi kuhusu hatima ni kwamba kwenye hatima yako ndiko kuliko na bahati yako na vitu vyote ambavyo unapaswa kuvimiliki hapa duniani vipo kwenye hatima yako.

Kwahiyo watu wote ambao wanaziendea njia za hatima yao iwe kwa kujua au kwakutokujua huwa hawahangaiki kwenye swala la fedha kama ambavyo watu wanaoishi kwenye maisha yaliyo nje ya hatima zao hufanya.

Na ninaposema hatima kuna watu wanadhani nazungumzia kitu fulani ambacho ni maalumu sana yaani kitu ambacho hakiwezekani kugundulika kirahisi raising hivi, ila naomba nikutoe wasiwasi na nikwambie tu kwamba hakuna umaalumu wowote kwenye hatima kwasababu hatima ni mambo yote ambayo yanaweza kufanyika hapa duniani ili kuongeza nguvu chanya na kuifanya dunia iwe sehemu salama.

Kwa maana hiyo kuna watu hatima zao ni kuburudisha na kuna watu hatima zao ni kuvumbua mambo kadha wa kadha na kuna watu hatima zao ni kutibu watu wengine na kuna watu hatima zao ni kufundisha mambo mbalimbali na kadhalika.

Na ili uweze kufikia hatima yako lazima upite kwenye njia fulani na hiyo njia ndio huwa tunaiita kipawa au kipaji.

Ndio, ni kipaji kwahiyo wala usishtuke kwasababu hata wewe unachokipaji ambacho ukikitumia kitakupeleka moja kwa moja kwenye hatima yako na mara tu utakapofika kwenye hatima yako basi watu wote watajua kwamba yupo au alikuwepo mtu fulani ambae alifanya makubwa sana kwenye mambo haya ya burudani hasa upande huu wa mpira na mtu huyo aliitwa Leonel Messi au Christiano Ronaldo.

Au alikuwepo mtu ambae alifanya makubwa sana kwenye mambo haya ya uvumvuzi wa mambo ya kisayansi ambae aliitwa Isaac Newton.

Au alikuwepo mtu ambae alifanya makubwa sana kwenye haya mambo ya muziki wa rege ambae aliitwa Bob Marley.

Au alikuwepo mtu ambae alifanya makubwa sana kwenye upande wa mashoati na movie za kupigana za karate aliitwa Blue Lee.

Kwahiyo hii inakwenda zaidi na zaidi na kuwafikia vizazi na vizazi huku wakiishi na kuutukuza ufalme wako kwenye upande huo wa hatima yako bila kujali mwaka ambao deadline yako ilifika na wewe kurudi kwenye ulimwengu wa asili yako huku roho yako ikiuhishwa na kupata uzima wa milele.

Na lazima ujue pia kwamba ukubwa wa hatima baina ya mtu na mtu huwa umetofautiana yaani kuna watu wamebeba hatima za kidunia ila wapo waliobeba hatima za kibara na wapo waliobeba za kiukanda lakini pia wapo waliobeba za kinchi na wapo waliobeba hatima za kimkoa, kijiji, kiukoo na kifamilia.

Ili ujue hatima yako ni ya ukubwa gani basi mambo utakayoyafanya kiwepesi sana yaani bila kutumia nguvu utaona yanaenda yanafika kwenye ngazi fulani ila utakapotaka uvuke hiyo ngazi uende ngazi nyingine utaona unatumika nguvu kubwa sana lakini matokeo yake hayawi kama pale awali ambapo ulikua hautumii nguvu nyingi ila mambo yalikua yanaenda parefu, hapo unatakiwa ujue kwamba wewe ukubwa wa hatima yako mwisho wake ni hapo.

Na hapa najua umeanza kunielewa pia ninaposema kwenye hatima yako ndiko kuliko na bahati yako na pindi utakapoigundua hatima yako na kuifuata ile njia inayoelekea huko basi moja kwa moja utaanza kuona wepesi wa mambo katika upande wa umiliki wa fedha na Mali.

Kwahiyo kumbe mateso ambayo watu wengi wanayapata kwenye upande wa kifedha huwa sababu moja wapo ni kuishi maisha yaliyo nje ya hatima zao na hii hufanya watumie nguvu sana kwenye swala la utafutaji huku wakiambulia kidogo kisicholingana na nguvu walizotumia.

Na unakutana na mtu anasali sana lakini bado mambo hayakai kwenye line, na hii sio kwasababu maombi yako hayafiki kule lahasha maombi yako yanafika ila nimekwambia kila roho iko na codes na hizi codes ndio hatima yako iko humo ndani na Kimsingi ulimwengu wa juu haukutambui wewe kwa sura na umbo lako la damu na nyama ila unakutambua wewe kwa codes zilizopo rohoni mwako, kwahiyo unavyoomba ile mitetemo inaenda moja kwa moja hadi kwenye ule mfumo nyota wa asili yako na majibu yanaporudi yanarudi kwakufuata ile code ambayo ipo ndani ya roho zako kwa maana hiyo kama maombi ni kubarikiwa kwenye utafutaji wako baraka itaongezwa kwenye ile hatima iliyopo ndani yako.

Kwahiyo ikiwa wewe hatima yako ni udaktari halafu ukashindwa kuifuata hatima hiyo na ukaamua uende upande mwingine labda wa ujenzi na mambo yakakuwia magumu huko hadi kufikia hatua ya kupiga goti chini ili ujiungamanishe mitetemo ya mfumo nyota ya asili yako basi kuwa na hakika kwamba maombi yako yatafika na majibu yatarudi ila wewe utakua unapishana mwenyewe, yenyewe yanaenda kwenye afya wewe upo kwenye ujenzi.

Sasa hili ndio lengo la uumbaji, ni kwamba roho ilitengenezwa kwa codes na kila kitu kikawa kimewekwa ndani yake kisha unaletwa hapa duniani na unapumbazwa na mambo ya dunia hadi unasahau roho yako imebeba kitu gani maalumu na chaupekee ambacho unatakiwa kukifanya ili uweze kuongeza nguvu za mitetemo chanya itakayosaidia kuifanya dunia kuwa sehemu salama.

Na ukumbuke kwamba kwenye kila hatima iliyopo ndani ya mtu huwa imewekwa na deadline yake na hiyo deadline ikifika basi muhusika anarudi kwenye ulimwengu wa asili yake yaani anakufa kama mnavyosemaga.

Sasa mpumbazo huu wa dunia ukikukumba kwa kiasi kikubwa na ikapelekea ukaenda hadi siku ya deadline yako, basi hapo ndio utakua upande wa zile mbegu ambazo si bora na mbegu ambayo si bora huwa mkulima anakua na option mbili either aitupe au aipe nafasi ya pili.

Ikitupwa haitoonekana tena shambani milele na milele ila ikipewa nafasi ya pili basi mkulima atajaribu kuipanda tena ili aone kama italeta matunda au laa na ndio hapa Sasa unakutana na roho ambazo zipo kwenye miili ya watu ila roho hizo zilishawahi kuwa hapa duniani hapo kabla (watu wenye roho za namna hii wapo wengi tu).

Ngoja leo niishie hapa kwanza ila nimeanzia huku mbali kidogo ili nitakapounganisha ili niweze kukuelezea ni kwanamna gani dunia ni uwanja wa vita za hatima uweze kunielewa vizuri.
Thecoder vp mkuu, naomba umalizie uzi wako wako wa Dunia ni uwanja vita, wengi tunasubilia
 
Sawa mkuu... Nitaendelea kuweka muendelezo hivi punde.
Utanishutua mkuu, hayo mambo ya kiroho huwa navugiwa nayo sana, Mungu akubariki sana ujumbe mzuri, kama kuna nyuzi zinazofanana na hizo please nipe tilte zake
 
ANDIKO LA ZIADA.

Kuna watu hudhani mitetemo humsaidia mtu katika kukabiliana na mambo ya kiroho tu ila kiuhalisia ni kwamba mitetemo huwa inabeba taswira ya maisha kamili ya mtu.

Kwa maana ya kwamba jinsi ambavyo utatengeneza muingiliano na watu wengine, jinsi ambavyo utakwenda kukabiliana na changamoto mbalimbali za kimaisha na kadhalika.

Na kitu ambacho unatakiwa ujue ni kwamba kama unavyoona uwepo wa ndugu wa damu basi pia unapaswa ujue ya kwamba wapo ndugu wa kiroho.

Sasa, ndugu wa damu ni watu mnaotokea ukoo au familia moja ila ndugu wa kiroho ni watu ambao mnatokea kwenye mfumo nyota wa aina moja.

Achana na ile ya ndugu zangu katika imani ya kwamba ndugu zangu katika uislam au ndugu zangu katika ukristo, hiyo ipo kwenye upande huo wa kuamini ustaarabu mfanano wa namna ya kufanya ibada.

Ila ninaposema ndugu wa kiroho namaanisha utimilifu zaidi uliopo upande wa pili wa mtu kwa maana ya upande ule wa kiroho ukiachana na huu wa damu na nyama.

Okay, ndugu zako wa kiimani utawajua kwakua wote huwa mnashiriki ibada kwa pamoja kwa maana ya msikitini, kanisani au kilingeni na hata kwenye mahekalu mbalimbali lakini pia ndugu zako wa damu utawajua kupitia vinasaba mfanano vilivyopo kwenye damu zenu.

Ila ndugu zako wa kiroho huwezi kuwajua kwa njia hizo au kwa kuwaangalia bali kwa ishara za ndani ambazo huwa zinakawaida ya kubadili sifa ya mtu iliyozoeleka kwa watu wanaomzunguka kwenda kwenye sifa nyingine ambayo haijazoeleka sana kutoka kwake.

Na hili ni wewe mwenyewe unaweza kulisoma au watu wanaokujua wanaweza kulisoma ya kwamba kuna hali isiyo ya kawaida ya kitabia imeanza kujionyesha kwako juu ya mtu mwingine.

Labda ukiwa nae unajikuta unakua dhaifu sana kihisia au unajikuta unamjali isivyo kawaida na mambo kama hayo.

Angalia, kuna watu ambao wanasifika kuwa na roho ya kutokujali wengine na watu wenye utata mwingi kwa wengine kwa maana si watu wenye kunyenyekea watu ila ni watu fulani hivi ambao ni wakali wakali or wenye kutokuzoeleka sana kwa wengine.

Lakini utashangaa baada ya muda fulani anatokea mtu mmoja ambae anakuja hapo mtaani au nyumbani kwenu na anamfanya huyo jamaa mtata abadilike isivyo kawaida, kwahiyo utakuta anakua mnyenyekevu na mtu mwenye kusikiliza Kila neno analoambiwa na huyo mtu mpya hapo mtaani na unakuta ni watu ambao wakikaa wanapiga story na kufurahi isivyozoeleka (kwa hali hii watu husemaga Kila shetani na mbuyu wake)

Sasa hii ni ishara ya kwamba watu hao wanatokea kwenye mfumo nyota unaofanana na kinachofanya mmoja awe anasikiliza au mnyenyekevu sana kutoka kwa mwenzie ni utimilifu uliopo kwenye mitetemo yao.

Mtu aliye na utimilifu wa juu kwenye mitetemo huwa anakua na uwezo wa kuwacontrol wengine wote waliochini yake kiutimilifu kutoka kwenye huo mfumo nyota unaofanana kama vile ilivyo wewe na kaka yako au dada yako kwa maana yule mkubwa ndio anaeweza kuwacontrol wadogo zake.

Na hii huwa ni mbaya sana au nzuri sana hasa inapoingia kwenye upande wa mahusiano ya kimapenzi kwa maana watu wa namna hii wanapokutana ili kuanzisha mahusiano ya kimapenzi huwa muunganiko wao unakua ni wa kudumu.

Na atakaekua anamuendesha mwenzake kwenye hayo mahusiano ni yule ambae anakiwango kizuri cha utimilifu kwenye mitetemo yake.

Kwahiyo kama huyu mwenye utimilifu atakua ni mtu asiyejali basi huyu mwingine ndie ambae ataumia sana kimapenzi.

Anaweza akalia na kuapa miungu yote ya kwamba ataachana na huyo mtu wake ila once wakionana ana kwa ana anakua hana usemi na anajikuta tu anapoa isivyo kawaida na anasahau yote aliyotaka kuyafanya na badala yake ataanza kuskiliza tena na kufuata hizo orders anazopewa.

Hii hata kwa wale magwiji wa mapenzi yaani wale ambao hawajawahi kuumia kimapenzi au hawajawahi kupenda kihivyo wanapokutana na watu wa namna hiyo huwa wanaweza hata kujiua ikitokea wameachwa, kwa maana unajikuta unampenda mtu isivyo kawaida na hata kama ulikua hauongi ila unajikuta unahonga na unajikuta uko ladhi kufanya jambo lolote ili mahusiano yenu yaendelee kudumu.

Na ikitokea watu wa hivi wameachana basi sababu ni yule ambae mitetemo yake iko na utimilifu na siku akisema arudi basi penzi linarudi upya bila kujali chochote.

Kwahiyo ikiwa umeoa au kuolewa na mtu ambae alishawahi kukutana na mtu anaetokea kwenye mfumo nyota unaolingana na yeye na ikatokea wametengana kwasababu za hapa na pale Kaa ukijua hao wakikutana wanayafanya yote yale ambayo walizoea kuyafanya.

Na aliyerudi akiamua kutangaza ndoa basi wewe utaachwa kwenye mataa umetulia zako.

Kwa maana kimsingi na kiutaratibu hawa ndio watu ambao waliumbwa kuja kulifanya hilo agano la ndoa pamoja duniani, ule utimilifu unapatikana kwa watu wa namna hiyo hasa ikitokea ule utimilifu wao wa kimitetemo haujaachana sana.

Kwa maana hiyo basi, watu wa hatima yako huwa mara nyingi wanatokea kwenye hili kundi.

Katika namna yoyote ya kimaisha, iwe kirafiki, kimahusiano ya ndoa au kazi au kusaidiana na kadhalika.

(Si Kila mtu anaweza akakusaidia au si Kila mtu anaweza akasaidiwa na wewe, unaweza ukawiwa kumsaidia mtu mwenye uafadhali wa maisha na ukashindwa kumsaidia mtu ambae hana uafadhali wowote wa maisha, mtu ambae aliwahi kumsaidia rafiki yako kwa tatizo mfanano na lile ulilonalo wewe hivi sasa anaweza akashindwa kukusaidia wewe hata kama anao huo uwezo wa kukusaidia, kwahiyo usinune au kulalamika kwa maana huo ni utaratibu wa kawaida wa ulimwengu).

Kwahiyo ukiwa vizuri kimitetemo na ikatokea umepata changamoto au umekwama kwenye eneo fulani wakati unaendelea kupiga hatua za kuelekea kwenye hatima yako, hizo hisia zako za kuwaza Kila siku jambo hilo kinamna chanya itamuibua mtu fulani mnaetokea mfumo nyota unaofanana na ambae anaouwezo wa kukutatulia hiyo changamoto.

Na hii itakua kinamna ile ile ya kimawimbi kama ilivyo kwa mawimbi ya redio au simu inavyozingatia network ili iweze kuunganisha mawasiliano.

Kwahiyo kupitia hiyo changamoto yako ambayo huwa unaiwaza au kuimeditate kinamna chanya sana huwa inapelekea mtu mmoja aweze kutoka kwenye comfort zone yake au wewe mwenyewe uweze kutoka kwenye comfort zone yako ili aweze kukutana na wewe au wewe kukutana na yeye kwa lengo la kutatua hiyo changamoto yako.

Kuna hali fulani zisizotarajiwa huwa zinatokea kwa watu ya kwamba mtu anajikuta ghafla tu anaanzisha safari ambayo haina umuhimu wowote kwake, yaani unaweza ukajikuta uko nyumbani umetulia mara ghafla unajiwa na hisia za kwenda eneo ambalo hukuliwazia hapo kabla na hata ukiulizwa kwa nini unaenda au umeenda hapo huwi na jibu la kueleweka zaidi ya lile la kutembea tu.

Na unapokua kwenye hayo maeneo ghafla unaweza ukakutana na mtu ambae ako na changamoto fulani ambayo iko ndani ya uwezo wako na kweli unajikuta unawiwa kuitatua na ukishaitatua basi unakaa Kaa na unarudi ulikotoka.

Au yule mtu ambae ako na changamoto inayohitaji kutatuliwa anaweza akakaa na ghafla akapata hamasa ya kujianzishia safari au kuna jambo linatokea kwenye mazingira yake na kujikuta anakua kwenye safari fulani na anapokua kwenye hiyo safari anakutana na mtu ambae wanaconnect kwa haraka sana na kupitia huyo mtu changamoto zake zinapata utatuzi.

Kuna watu wamelia sana juu ya kuoa au kuolewa ila siku isiyojulikana wakajikuta tu ghafla wanaanzisha safari na kwenye hiyo safari wanakutana na watu ambao pengine waliwachukulia kuwa kama watu wakawida kama walivyokua wengine ila mwisho wa siku katika hali isiyotarajiwa wanajikuta vile vilio vyao vya kuoa au kuolewa vinapata ufumbuzi kupitia watu hao.

Kwahiyo kuna nyakati ambazo vitendo hivi huwa vinapendeza ila pia kuna nyakati ambazo vitendo hivi havipendezi kwa maana kuna nyakati ambazo wewe na ndugu yako wa kiroho mnajikuta mnatimiza hatima zenu kwa pamoja ila kuna nyakati mmoja anajikuta anatumika kutimiza hatima ya mwingine bila kupenda au kujua.

Kuna watu ambao wako na utimilifu imara sana kwenye mfumo nyota wao, hawa watu wamekua wakiwatumia sana watu wengine ili wao waweze kusonga mbele pasipo wao wenyewe kujua.

Kwa mfano, kuna watu walikua na maisha mazuri, kazi nzuri au biashara iliyosimama ila kuna sintofaham ikatokea kwenye maeneo yao ya kazi au biashara iliyowafanya wao wenyewe waichukie hiyo kazi au biashara na kujikuta wanakimbia kwenda kwenye mji mwingine na huko wanaenda kukutana na mtu fulani atakae watumia kutekeleza hatima yake.

Na mambo haya yote huwa yanatokea kwenye msimu wa mabadiliko ya kihatima ambayo mtu hukutana nayo pale anapohama kutoka kwenye stage moja kwenda kwenye stage nyingine itakayomsogeza karibu ya hatima yake zaidi au kumrudisha nyuma zaidi.

Sasa, kuna watu ambao wanatoka kwenye comfort zone zao na kwenda kwenye maeneo mengine wasiyoyatarajia kwasababu hatima zao zinahitaji njia za namna hiyo ili ziweze kutokea ila kuna watu ambao wanahama kwa kutoka kwenye comfort zone zao na kwenda kwenye maeneo wasiyo yatarajia kwasababu kuna mtu kwenye hilo eneo hatima yake inamuhitaji huyo aliyetoka kwenye comfort zone yake na kwenda kwenye hilo eneo, kwahiyo yeye amepatikana wakati mitetemo inatafutana kiasi cha kumfanya aweze kutoka kwenye eneo lake la kujidai kwenda kwenye eneo asilolitegemea ili mtu fulani kwenye eneo hilo aweze kupiga hatua kupitia yeye.

Na unapoingia kwenye kipindi hiko cha mabadiliko ya kihatima, huwa hasi na chanya zinakua karibu sana.

Na ikiwa lengo ni kukutoa kwenye eneo lako la kujidai basi lazima sababu iwepo itakayosababisha wewe uweze kutoka kwenye hilo eneo bila kulazimishwa na mtu yeyote yule.

Na kwenye hizo sababu huwa zinaweza zikatokea upande chanya au upande hasi kutegemeana na nguvu ya usababishi itakua ipo upande gani kati ya pande hizo mbili.

Sababu hizo za kukufanya utoke kwenye eneo lako la kujidai kwanza zitaanza kutafutwa ndani yako kisha nje yako kwa maana kwa watu ambao wamekuzunguka au vitu ambavyo vimekuzunguka na ile ambayo iliandaliwa au wewe mwenyewe uliiandaa kwaajiri ya hayo mabadiliko pasipo wewe kujua basi itatumika kukufanya utoke kwenye hiyo comfort zone yako bila kupenda.

Nilisema hatima ni kama puzzle na puzzle hii ya hatima huwa inatatuliwa kwa mambo madogo madogo ambayo mtu anakabiliana nayo Kila siku.

Na ndio maana nikasema haupaswi kuchukulia mambo poa poa kwasababu duniani hakuna jambo linalompata au kukabiliana na mtu kibahati mbaya.

Kila jambo ambalo linakutokea Kila siku huwa linaathari fulani kwenye puzzle yako ya kuelekea kwenye hatima.

Inawezekana ikaja kuwa athari chanya au athari hasi na ndio maana swala la uhuiswaji si swala ambalo ni rahisi kuweza kulifikia.

Haijalishi unataka uhuishwe kinamna chanya au kinamna hasi ila kwenye namna zote hizo huwa uhuiswaji haupatikani kirahisi.

Kwahiyo, mambo yote ambayo umeyatunza ndani yako kama siri kwa maana mengine ni mambo ya aibu na siku yakija kujulikana basi unaweza kuonekana mtu wa hovyo kuwahi kutokea kuna siku moja hayo mambo yanaweza kuja kutumika kama chambo ya kukutoa kwenye eneo lako la kujidai ili uweze kwenda kwenye eneo lingine kwaajiri ya kupiga hatua zaidi ya kihatima au kwenda kumpigisha mtu mwingine hatua za hatima yake.

Kwenye misimu ya namna hiyo huwa hakuna kubembelezana, bila kujali ni hatua yenye faida kwako au yenye faida kwa mwingine ni kwamba universe ikisema unatakiwa utoke kwenye comfort zone yako ni unatoka tu tena bila hata kubembelezwa ila ni wewe mwenyewe utahaha sana ili uweze kutoka hapo kwa maana kutoka hapo ndio unafuu wako.

Ingawa kuna wengine huwa wanapitia hizo hatua kiugumu ugumu sana kutokana na ukosefu wa visababishi vingi ambavyo viko ndani yao kwahiyo mazingira ya nje huwa yanalazimishwa kuingilia kati ili visababishi viweze kupatikana kwaajiri ya kuwafanya watoke hapo.

Na mazingira ya nje yanapolazimishwa ili yaweze kuleta visababishi yanaweza yakaleta kwa namna yenye kuleta maumivu au ya kumfanya mtu akose uhuru wa kuishi kwenye hayo mazingira aliyoyazoea.

Ila kama uko na siri zako nzito za aibu ambazo umezitunza humo ndani yako na ikiwa zinafaa kutumika kukuondoa hilo eneo basi haraka sana siri inafichuka unajikuta uchi mtaa mzima au ofisi nzima na unaanza kuhaha na kujikuta unapata wazo la kuhama hapo uende eneo fulani ambalo litakua hapo kichwani mwako na hilo ndio litakua eneo lengwa kwako.

Yes, najua ni mambo yanayoshangaza ila huu ni utaratibu wa kawaida wa dunia kwasababu Dunia ni uwanja wa vita vya hatima kwahiyo ni lazima ubongo wako uwe active muda wote kwa maana tupo hapa kwaajiri ya mission maalumu kwahiyo Kila siku unapaswa ukabiliane nayo ukiwa ubongo wako unafanya kazi kwa utimamu wa juu sana.

Kuna hadithi za kihatima kwenye maandiko, ile ya Yakobo(Yakubu), ile ya Yusufu, ile ya Ayubu na hata ile ya Musa.

Ukiangalia hadithi ya Yakobo au Yakubu utaona kwamba ni mtu ambae hakuwa na exposure yoyote na ulimwengu uliomzunguka kwa maana alikua ni mtoto wa mama sana, ila msimu wa mabadiliko ya upigaji hatua kuelekea hatima yake uliposogea na kutakiwa atoke kwenye comfort zone yake basi ile hali ya uongo iliyopo ndani mwake ikatumika kuweza kumtoa kwenye hilo eneo baada ya kuzuka ugomvi wa kutaka kuuana kwa mapanga yeye na kaka yake kwahiyo ikabidi akambilie kwa mjomba wake na huko alienda kutumika kwaajiri ya hatima ya mjomba wake lakini pia na yeye hatima yake ilihitaji njia hiyo.

Yusufu alijikuta kwenye nchi ya mbali bila yeye kutarajia na hii yote ni kutokana na ule msimu wa hatima yake ulipohitaji mabadiliko ya kutoka kwenye comfort zone yake ulipofika, basi ndugu zake wakatumika ili yeye hatima yake itimie.

Musa alifanya jambo jema kutoa msaada baada ya kuua mtu aliyekua akimuonea mwingine na hilo likawa ni agano la siri baina yake na yule aliyemsaidia ila mabadiliko ya kihatima yalipofika ile siri ikafichuka na kujikuta anakwenda eneo la mbali bila kupenda ila huko ndiko ambako hatima yake ilienda kuanza.

Ayubu, mtu tajiri ambae ilitakiwa atolewe kwenye comfort zone yake ili ile hatima ya unyenyekevu iliyo ndani yake iweze kufikiwa.

Kwahiyo jitahidi sana uwe chanya siku zote ili uendelee kuimarisha mitetemo yako kwa maana bila hivyo unaweza ukatumika sana kutimiza hatima za watu wengine bila ya wewe mwenyewe kujua au kupenda.

Lakini pia usisahau ya kwamba msimu wa mabadiliko unapokuja huwa hauchagui siraha kwahiyo jitahidi kubalance hizo siri unazozirundika ndani yako kwa maana kuna siku moja usiyoijua zitatumika kwaajiri yako wewe mwenyewe.

NITARUDI…
 
Utanishutua mkuu, hayo mambo ya kiroho huwa navugiwa nayo sana, Mungu akubariki sana ujumbe mzuri, kama kuna nyuzi zinazofanana na hizo please nipe tilte zake
Angalia kwenye profile yangu, kuna ule Uzi wa namna historia ya kwenu inavyoweza kukupa picha ya hatua unazopaswa kupiga kuelekea kwenye hatima... Nenda kasome labda unaweza kupata kitu.
 
Angalia kwenye profile yangu, kuna ule Uzi wa namna historia ya kwenu inavyoweza kukupa picha ya hatua unazopaswa kupiga kuelekea kwenye hatima... Nenda kasome labda unaweza kupata kitu.
Thanks mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom